Niliyashuhudia Tanga

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,193
Wana JF, nina hakika wengi watakaosoma kisa hiki watadhani ni cha kutunga, lakini ni kisa cha kweli ambacho kilitokea kwenye miaka ya 80 hivi eneo la makorora mjini Tanga. Na kilimtokea mtu ambaye alikuwa ni rafiki yangu wa karibu. Kisa chenyewe ni kama ifuatavyo;

Nilipokuwa Tanga miaka hiyo ya 80 kuna jamaa mmoja alikuwa anatembea na mke wa mzee mmoja. Huyo mzee akamtumia watu kumuonya hakusikia. Siku moja wakati ametoka kuvunja amri ya sita na huyo mama mke wa mzee, akafika nyumbani akaenda bafuni kuoga. Baada ya kuoga akiwa anajifuta maji kwa taulo, akamuona paka akielekea mlangoni mwa bafu amebeba "vifaa" vyote (kamjamaa na majirani zake). Kujichungulia huko chini akakuta pako flat kabisa

Kijana akachanganyikiwa asijue la kufanya. Amekaa siku 2 akashindwa kuvumilia, akaenda kuwatafuta wazee akawasimulia yaliyomkuta, nao wakamshauri wampeleke kwa mwenye mali kuomba radhi akaafiki bila kupinga. Alipofika akajieleza kila kitu bila kuficha chembe yoyote ya ukweli. Mwenye mke akakataa kata kata kwamba hajui lililotokea na hajamfanyizia kijana wa watu. Basi wazee wakamsihi sana yule mzee, hatimaye akampiga faini yule kijana ya shilingi elfu 10 (wakati huo pesa nyingi sana) na akakubali kumrudishia mali zake.

Mzee akamwagiza mke wake amletee kapu lake. Lilipoletwa kapu kijana alikuta limejaa "vifaa" vya kila aina akaambiwa achague vya kwake akashindwa. Basi yule mzee akamwambia kama umeshindwa leo, basi urudi kesho asubuhi. Kijana akaondoka kwa majonzi sana. Kufika njiani akajisikia hamu ya kutaka kukojoa, kuchungulia akakuta vifaa vyote vyake vimerudi. Kuanzia wakati huo mwenzetu aliamua kuokoka kwenye dhehebu la Kulola.

Wana JF wale wanaopenda kunyemelea mali za watu angalieni yasije yakawakuta kama yaliyomkuta rafiki yangu.
 
naijua hii story....kwenye kapu pia wakati wa kuchagua kifaa chake,akaona ya albino pia ipo ...lol
 
safi sana kumbe afrika tunaweza kwa utaalamu tukiamua.
ntafurahi mzungu akifanyiwa hivo ili waache kuidharau afrika.
 
Hivi vi2 kaulize Mafia kuna zaidi ya hii, kuna jamaa alishawahi kuamka akakuta '' Mipira yake na Fimbo ya gofu'' inaning'inia juu ya paa kisa alikuwa anatembea na mke wa mtu. Acha kabisa
 
Back
Top Bottom