Niliwaonya wana CCM wenzangu mkanitukana sana, uchaguzi huu si lelemama

BALAGASHIA

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
392
383
Niliwaambia uchaguzi Huu si lelemama. Kwa ujio huu wa Lissu unadhihirisha kabisa CCM tumekuwa dhaifu sana. Chama sasa kimejaa wanafiki, watu wa kusifia tu wasiojua kujenga hoja.

Jukwaa likiwa huru tumekwisha. Siamini kwa namna wapinzani walivyobanwa miaka 5 sikutegemea kama wananchi wangekuwa na presha ya kumpokea Lissu kiasi hiki.
 
Wamefanya kila kitu cha maendeleo ambacho hakikuwahi fanywa toka Tz ipate uhuru, sifa na majina hata matakatifu wamepachikwa, wazalendo hawajapata tokea Tz kama wao, wanyonge wakapata wapaza sauti, upinzani wakaambiwa kwisha habari yao, mahakama ya mafisadi ikaandaliwa, yaani kwa ujumla mambo ni mengi sana muda wa kuyaainisha hautoshi. Zaidi fomu ilitoka 1 tu ngachoka hoi mie, hata kuonyesha unafiki tu kwa wagombea chamani wawe wengi achaguliwe 1 hakuna.

Hayo yote sawa nakubaliana na wao!

Swali langu huwa ni KWA NINI KUUHOFIA UPINZANI?

Apinzani ambao haujafanya cho chote kwa watanzania achilia mbali mambo yao ya ndani au nje (vikao/mikutano)
 
Niliwaambia uchaguzi Huu si lelemama. Kwa ujio huu wa lissu unadhihirisha kabisa CCM tumekuwa dhaifu sana. Chama sasa kimejaa wanafiki, watu wa kusifia tu wasiojua kujenga hoja.Jukwaa likiwa huru tumekwisha. Siamini kwa namna wapinzani walivyobanwa miaka 5 sikutegemea kama wananchi wangekuwa na presha ya kumpokea lissu kiasi hiki.
Wapinzani tutawadhibiti kwa nguvu zetu zote, ikiwezekana watafanywa kama wale wa Januari 2000
 
CCM kama chama cha siasa kimeshapitwa na wakati, huu ni wakati wa kizazi kipya, mawazo na fikra mpya, hata kama CCM ikiachwa ifanye siasa peke yake for ten years, bado upinzani hata wakipewa miezi sita wafanye siasa wanaifutilia mbali CCM.

Siku hizi nguvu ya CCM kama chama cha siasa imebaki kutegemea polisi na tume feki ya uchaguzi, ukweli ni kwamba, hawana uungwaji mkono wowote na wananchi.
 
Back
Top Bottom