Niliwahi kumwambia Hayati Magufuli, leo narudia kwa Rais Samia ili asipoteze muda wake

Kweli utajiri upo sana nchini ila hatujui namna ya kutumia fursa
Kauli za kusema Walituchelewesha zilikuwa ni siasa tu
Sauti ilikuwa moja

Matunda na Mazao mengi yamejaa na kauli tulizisikia sana kuwa tutawauzia majirani chakula wakiwa na njaa
Ila sijawahi kusikia vibali vitoke sana ili watu wapeleke bidhaa zetu Ulaya na Middle East kwenye hela huko ili tupate za kigeni

Tunahitaji hela za nje kujenga nchi na sio kukusanya kodi za ndani tu

La mwisho Dual citizenship inahitaji sana kwa wazawa waliopo nje
Hili limeingelewa sana ila waameweka pamba na hakuna sababu za msingi zaidi ya kutokuangalia faida zake
Tz hatuna utajiri bali tuna rasilimali za asili nyingi. KUWA na rasilimali si kwamba wewe ni tajiri. (Ufafanuzi)
 
NILIWAHI KUMWAMBIA HAYATTI MAGUFULI, LEO NARUDIA KWA RAIS SAMIA, ILI ASIJEPOTEZA MUDA WAKE.

Na, Robert Heriel

Niliwahi kuandika hapa miaka mitatu iliyopita, niliipa makala ile kichwa kisemacho "Rais Magufuli unapoteza muda wako tuu" katika makala ile watu wengi walinitukana, wengine walinitishia, sikuwalaumu kwani niliwaelewa lakini wao hawakuwahi kunielewa.

Leo hii narudia baadhi ya maneno yaleyale niliyoyasema siku zile.

Niliandika Magufuli anapoteza muda wake nikiwa na hoja zifuatazo;

1. Magufuli nilimuona anapoteza muda kwa sababu alikuwa na mtazamo kuwa, nchi ni tajiri na itapata maendeleo kwa sababu ina Rasilimali nyingi akizitaja kama madini, mbuga, ardhi kubwa yenye Rutuba, maziwa na mito yenye viumbe maji kama samaki, vivutio vya utaliii, bahari, kuzungukwa na mataifa mengi yasiyo na bahari, n.k.
Niliona anapoteza muda kwa sababu, nchi haiendelei kwa wingi wa Rasilimali isipokuwa inaendelea kwa ya kuwa na WATU WENYE AKILI. Watu wenye akili ndio wanaleta maendeleo nchini sio uwepo wa Rasilimali nyingi.

2. Magufuli aliamini, nchi itajengwa kwa kuwanyonya wananchi wake pekee, ndio maana alishindwa kuongeza mishahara miaka yake yote aliyotawala, pia akashindwa kutoa ajira mpya.
Kama hiyo haitoshi, sio ajabu aliongeza vikodi vya hapa na pale ili kuendesha serikali yake, lakini bado mambo yalimuwia magumu hali iliyomfanya ajiingize katika hatari ya kugombana na wafanyabiashara, wengi wao aliwaita wahujumu uchumi, wapo walioisoma.

Mimi nilimwambia nchi yoyote iliyoendelea haijawahi kuendelea kwa kutegemea unyonyaji kwa watu wake pekee, bali ni lazima ivamie mataifa mengine. Nilitoa mifano kwa baadhi ya mataifa yaliyoendelea yaliyojipatia utajiri kwa kunyonya watu wake na mataifa mengine.. Biashara ya utumwa, Ukoloni, na ukoloni mamboleo vyoote vinaangukia hapa.

Taifa kama la Korea ya kusini loo, liliamua kualika mataifa mengine hasa Mataifa ya Magharibi kuja kuwekeza Korea kusini. Kwa sasa Korea ni moja ya nchi zilizopo ulimwengu wa pili.

3. Magufuli aliamini kuongoza nchi kibabe ndio suluhu ya maendeleo, wakati mbinu hiyo ilishapitwa na wakati, na kwa vyovyote lazima ingelala upande wake na angeshindwa, licha ya kujitutumua kuchelewesha muda wa anguko lake.

Mimi nilimwambia kuwa kizazi cha sasa kinaongozwa kwa akili, ujanja, maarifa na mambo yote yahusuyo akili. Ubabe ungeweza kutumika machungani kwenye mbuzi, ng'ombe, na kondoo ambao hawana utashi kama binadamu.

Hakuna uhusiano wa karibu baina ya Ubabe na biashara, hivyo kivyovyote vile anguko la kiuchumi lilikuwa ni uhakika. Kwani hakuna mfanyabiashara ambaye angependa aishi kwa hovyo wakati pesa ni zake mwenyewe.

4. Magufuli aliamini kuwakaripia wengine mbele ya halaiki na wengine kuwatukana ndio namna ya kuleta nidhamu ndani ya serikali yake.
Wakati nidhamu ndani ya serikali hutokana na jinsi sheria zinavyofuatwa na kutelekezwa. Kama mtu ni mwizi basi sheria ingechukua mkondo wake,

Masikini wengi na watu walioshindwa walifurahishwa na magufuli kwa sababu ni kawaida ya masikini kuona mwenye nacho akianguka.

5. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye matamko kuliko kuweka mfumo imara ili hata yeye akiondoka mambo yatajiendesha vyema.
Niliwahi mwambia kuwa One manshow ni kama mbio za sakafuni ambazo lazima ziishie ukingoni. Nilimwambia anapoteza muda wake.

Maendeleo ni mfumo kama mnyororo unaounganisha seti nyingi ya vitu.
Maendeleo ya nchi za Afrika niya kubahatisha kwa sababu hakuna mfumo unaoeleweka.

6. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye kujipa promo kwenye vyombo vya habari na kujisifu, na kuwazima wengine ili kuchota akili za watu wenye upeo mdogo na kuzuia wale waliokuwa wanampa challenge kwa mitazamo yao.
Hii pekee ingetosha kuonyesha kuwa anapoteza Muda wake.
Hakuwa mtu kama Anthony Mtaka ambaye hafanyi manipulation lakini matendo yake yanaonekana.

7. Magufuli alifanikiwa zaidi katika kutekeleza na kusimamia maendeleo ya miundombinu, kwa hili nampa heko, lakini nilimuambia kuwa taifa masikini linawekeza kwenye watu na sio vitu,
Hii watu walinipinga lakini huo ndio ukweli mchungu, masikini kuwekeza kwenye vitu zaidi ya watu ni kupoteza muda na kuwatesa watoto.

8. Magufuli alijitahidi kujifanya hawapendi Wazungu na kila mara alitoa maneno ya kupata ushawishi kwa watu ili wawachukie wazungu. Ndio maana hata Mambo ya Corona aliyaona kama mchezo wa kuigiza na njama za wazungu kutuangamiza.

Jambo ambalo hata mtoto mdogo akifikiri anaona ni uongo wa mchana.
Nilimuunga mkono kwenye suala la kutokuweka Lockdown, lakini masuala mengine nilimpinga.

Magufuli angepoteza muda kwa vyovyote kwa kupinga mambo ya wazungu ambayo hata huo Urais aliokuwa nao ni mfumo wa kizungu, masuala ya jeshi ni mifumo ya kizungu, jina lake lakizungu, dini yake yakizungu na hata alipokufa alizikwa kizungu, hata elimu yake ni yakizungu, hata magari na vifaa vyote alivyokuwa akivitumia ni vyawazungu, achilia mbali madawa na miwani aliyokuwa akivaa. Sijazungumzia silaha na wana usalama waliokuwa wanamlinda ambao ili wawe wa kimataifa inapaswa wapewe mafunzo ya kizungu.

Kama wazungu wangetaka kutuua wangetuua tangu miaka ya 1900 huko walipokuja kututawala. na hata wakiamua kutuua uwezo huo wanao, na hatuna uwezo wa kufurukuta.

Sasa mambo hayo hayo, nayasema kwa Rais Samia, kuwa aangalie asije akapoteza muda wake kwa kushindwa kuendana na wakati.

Maendeleo ya nchi ya USA sio lazima yawe maendeleo kwa Tanzania. Hiyo ni muhimu kuzingatiwa.

Hata hivyo Rais Samia lazima azingatie haya ili naye asijikute katika kucheza Nage na kupoteza muda wake.

1. Maendeleo ni kuwekeza kwenye watu
2. Kuwekeza kwenye watu ni kuwapa Uhuru
3. Uhuru wa watu ni pamoja na kuwapa nafasi ya kuyafurahia maisha yao kwa kutumia rasilimali za nchi yao au kuvamia mataifa mengine. Passport zitolewe watu wakahangaike huku na huko.
4. Serikali isifikiri kunyonya wananchi wake pekee(kodi na ushuru) bali pia ifikiri namna ya wananchi wake kuenda nchi zingine kunyonya mali na utajiri wa nchi zingine.

5. SHeria na utawala bora zisiachwe
6. Ubabe wa kipumbavu uachwe maana palipo na ubabe au udikteta lazima kuwa na uasi/usaliti na palipo na usaliti lazima pawe na mapinduzi.

7. Serikali isijikite kwenye matamko ya kipuuzi puuzi. Kwani kwa kufanya hivyo itaathiri vijana wengi ambao wao kila kitu watataka tamko la serikali.

Sishangai kwa nini watu wanamlaumu Mama kuwa kwa nini ni mpole, ni kutokana na kuathiriwa na matamko yasiyo na kichwa wala miguu.

Sio kila kitu kitolewe tamko kwa kutafuta sifa za kijinga kwenye Kamera ili ionekane kazi inafanyika wakati hakuna kitu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dar es salaam
Hata mimi nilimwambisa sana akashupaza shingo.
 
Ukijiona una kichefuchefu usipapatike,

Huo Ni ujauzito aliokuachia mwendazake
 
Ukifanya maendeleo ya vitu utarahisisha maendeleo ya watu.

Kwa nchi kama Tanzania ilifaa sana kuongozwa kibabe maana tulifikia pabaya sana.


Kwa sisi tuliokuwa kutwa tunahangaika na ofisi za umma tuliweza kuona tofauti kabla yake, wakati wake na baada yake
 
Kwa Tanzania katiba sio tatizo,tatizo kubwa na watu bado ni wajinga pamoja na hii katuba mbovu mengi yamefanyika pasipo kuifata but sote tunaona ni sawa tumelala usingizi wa pono.
Mimi nashangaa naposikia kwamba wananchi wanataka katiba mpya hali ya kuwa katiba ya sasa iliyopo hawana uelewa nayo.
 
Kitakacho kera zaidi kwa utawala huu ni kuendeleza chaguzi za kibabe, kutekana, watu kuumizwa, kufa na hakuna hatua zinazochukuliwa.
Toka kwa Ulimboka huko hadi leo, haya mambo kutesana yapo tu siku zote.
 
Nawaza nao wazungu wangesema msipelekee misaada wale nyani wa africa maana wao ni mabeberu jpm aliwaita na wao wangemuita nyani daaa
Nadhani wazungu wana roho nzuri sana hutoa tu misaada ili wapate malipo kwa Mungu.
 
Mmmmh! Asingeweza kuwafukuza maana ingeleta diplomatic problem. Kila siku alikuwa anawaimba mabeberu mabeberu!!! Huo wimbo mpaka leo kuna watu wanauimba hasas kwenye taarifa ya wataalamu wa kumshauri raisi kuhusu covid 19. Wanasema wametumwa na mabeberu hao madaktari! Na hii mi naona ni sumu kaiacha mwendazake!!!! Na sumu hii itatutafuna sana. Hata hivi tunavyochat ni wazungu. Sasa tunawaonaje wabaya? Kila kitu chetu tunachofanya kama alivyosema mwandishi ni wazungu. Na tutaendelea na vya wazungu tu!!!!
Kuchat ni matokeo ya teknolojia.
 
Kabla ya daraja la sasa hivi, kuna ndugu yangu mmoja aliwahi kupoteza mtoto katika foleni ya ubungo wakati akiwa anampeleka hospitali.

Jamaa ana pesa nzuri tu (maendeleo ya watu) lakini miundombinu mibovu (maendeleo ya vitu) ilifanya apoteze mtoto.
Kwa kuwa hakukuwa na maendeleo ya vitu, mtu akapoteza uhai! Bila maendeleo ya vitu hakuna mtu!
 
Ukifanya maendeleo ya vitu utarahisisha maendeleo ya watu.

Kwa nchi kama Tanzania ilifaa sana kuongozwa kibabe maana tulifikia pabaya sana.


Kwa sisi tuliokuwa kutwa tunahangaika na ofisi za umma tuliweza kuona tofauti kabla yake, wakati wake na baada yake


Upo sahihi.

Ila maendeleo ya kweli hujengwa akilini mwa mtu.
 
Back
Top Bottom