Niliwahi kumwambia Hayati Magufuli, leo narudia kwa Rais Samia ili asipoteze muda wake

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,863
NILIWAHI KUMWAMBIA HAYATTI MAGUFULI, LEO NARUDIA KWA RAIS SAMIA, ILI ASIJEPOTEZA MUDA WAKE.

Na, Robert Heriel

Niliwahi kuandika hapa miaka mitatu iliyopita, niliipa makala ile kichwa kisemacho "Rais Magufuli unapoteza muda wako tuu" katika makala ile watu wengi walinitukana, wengine walinitishia, sikuwalaumu kwani niliwaelewa lakini wao hawakuwahi kunielewa.

Leo hii narudia baadhi ya maneno yaleyale niliyoyasema siku zile.

Niliandika Magufuli anapoteza muda wake nikiwa na hoja zifuatazo;

1. Magufuli nilimuona anapoteza muda kwa sababu alikuwa na mtazamo kuwa, nchi ni tajiri na itapata maendeleo kwa sababu ina Rasilimali nyingi akizitaja kama madini, mbuga, ardhi kubwa yenye Rutuba, maziwa na mito yenye viumbe maji kama samaki, vivutio vya utaliii, bahari, kuzungukwa na mataifa mengi yasiyo na bahari, n.k.
Niliona anapoteza muda kwa sababu, nchi haiendelei kwa wingi wa Rasilimali isipokuwa inaendelea kwa ya kuwa na WATU WENYE AKILI. Watu wenye akili ndio wanaleta maendeleo nchini sio uwepo wa Rasilimali nyingi.

2. Magufuli aliamini, nchi itajengwa kwa kuwanyonya wananchi wake pekee, ndio maana alishindwa kuongeza mishahara miaka yake yote aliyotawala, pia akashindwa kutoa ajira mpya.
Kama hiyo haitoshi, sio ajabu aliongeza vikodi vya hapa na pale ili kuendesha serikali yake, lakini bado mambo yalimuwia magumu hali iliyomfanya ajiingize katika hatari ya kugombana na wafanyabiashara, wengi wao aliwaita wahujumu uchumi, wapo walioisoma.

Mimi nilimwambia nchi yoyote iliyoendelea haijawahi kuendelea kwa kutegemea unyonyaji kwa watu wake pekee, bali ni lazima ivamie mataifa mengine. Nilitoa mifano kwa baadhi ya mataifa yaliyoendelea yaliyojipatia utajiri kwa kunyonya watu wake na mataifa mengine.. Biashara ya utumwa, Ukoloni, na ukoloni mamboleo vyoote vinaangukia hapa.

Taifa kama la Korea ya kusini loo, liliamua kualika mataifa mengine hasa Mataifa ya Magharibi kuja kuwekeza Korea kusini. Kwa sasa Korea ni moja ya nchi zilizopo ulimwengu wa pili.

3. Magufuli aliamini kuongoza nchi kibabe ndio suluhu ya maendeleo, wakati mbinu hiyo ilishapitwa na wakati, na kwa vyovyote lazima ingelala upande wake na angeshindwa, licha ya kujitutumua kuchelewesha muda wa anguko lake.

Mimi nilimwambia kuwa kizazi cha sasa kinaongozwa kwa akili, ujanja, maarifa na mambo yote yahusuyo akili. Ubabe ungeweza kutumika machungani kwenye mbuzi, ng'ombe, na kondoo ambao hawana utashi kama binadamu.

Hakuna uhusiano wa karibu baina ya Ubabe na biashara, hivyo kivyovyote vile anguko la kiuchumi lilikuwa ni uhakika. Kwani hakuna mfanyabiashara ambaye angependa aishi kwa hovyo wakati pesa ni zake mwenyewe.

4. Magufuli aliamini kuwakaripia wengine mbele ya halaiki na wengine kuwatukana ndio namna ya kuleta nidhamu ndani ya serikali yake.
Wakati nidhamu ndani ya serikali hutokana na jinsi sheria zinavyofuatwa na kutelekezwa. Kama mtu ni mwizi basi sheria ingechukua mkondo wake,

Masikini wengi na watu walioshindwa walifurahishwa na magufuli kwa sababu ni kawaida ya masikini kuona mwenye nacho akianguka.

5. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye matamko kuliko kuweka mfumo imara ili hata yeye akiondoka mambo yatajiendesha vyema.
Niliwahi mwambia kuwa One manshow ni kama mbio za sakafuni ambazo lazima ziishie ukingoni. Nilimwambia anapoteza muda wake.

Maendeleo ni mfumo kama mnyororo unaounganisha seti nyingi ya vitu.
Maendeleo ya nchi za Afrika niya kubahatisha kwa sababu hakuna mfumo unaoeleweka.

6. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye kujipa promo kwenye vyombo vya habari na kujisifu, na kuwazima wengine ili kuchota akili za watu wenye upeo mdogo na kuzuia wale waliokuwa wanampa challenge kwa mitazamo yao.
Hii pekee ingetosha kuonyesha kuwa anapoteza Muda wake.
Hakuwa mtu kama Anthony Mtaka ambaye hafanyi manipulation lakini matendo yake yanaonekana.

7. Magufuli alifanikiwa zaidi katika kutekeleza na kusimamia maendeleo ya miundombinu, kwa hili nampa heko, lakini nilimuambia kuwa taifa masikini linawekeza kwenye watu na sio vitu,
Hii watu walinipinga lakini huo ndio ukweli mchungu, masikini kuwekeza kwenye vitu zaidi ya watu ni kupoteza muda na kuwatesa watoto.

8. Magufuli alijitahidi kujifanya hawapendi Wazungu na kila mara alitoa maneno ya kupata ushawishi kwa watu ili wawachukie wazungu. Ndio maana hata Mambo ya Corona aliyaona kama mchezo wa kuigiza na njama za wazungu kutuangamiza.

Jambo ambalo hata mtoto mdogo akifikiri anaona ni uongo wa mchana.
Nilimuunga mkono kwenye suala la kutokuweka Lockdown, lakini masuala mengine nilimpinga.

Magufuli angepoteza muda kwa vyovyote kwa kupinga mambo ya wazungu ambayo hata huo Urais aliokuwa nao ni mfumo wa kizungu, masuala ya jeshi ni mifumo ya kizungu, jina lake lakizungu, dini yake yakizungu na hata alipokufa alizikwa kizungu, hata elimu yake ni yakizungu, hata magari na vifaa vyote alivyokuwa akivitumia ni vyawazungu, achilia mbali madawa na miwani aliyokuwa akivaa. Sijazungumzia silaha na wana usalama waliokuwa wanamlinda ambao ili wawe wa kimataifa inapaswa wapewe mafunzo ya kizungu.

Kama wazungu wangetaka kutuua wangetuua tangu miaka ya 1900 huko walipokuja kututawala. na hata wakiamua kutuua uwezo huo wanao, na hatuna uwezo wa kufurukuta.

Sasa mambo hayo hayo, nayasema kwa Rais Samia, kuwa aangalie asije akapoteza muda wake kwa kushindwa kuendana na wakati.

Maendeleo ya nchi ya USA sio lazima yawe maendeleo kwa Tanzania. Hiyo ni muhimu kuzingatiwa.

Hata hivyo Rais Samia lazima azingatie haya ili naye asijikute katika kucheza Nage na kupoteza muda wake.

1. Maendeleo ni kuwekeza kwenye watu
2. Kuwekeza kwenye watu ni kuwapa Uhuru
3. Uhuru wa watu ni pamoja na kuwapa nafasi ya kuyafurahia maisha yao kwa kutumia rasilimali za nchi yao au kuvamia mataifa mengine. Passport zitolewe watu wakahangaike huku na huko.
4. Serikali isifikiri kunyonya wananchi wake pekee(kodi na ushuru) bali pia ifikiri namna ya wananchi wake kuenda nchi zingine kunyonya mali na utajiri wa nchi zingine.

5. SHeria na utawala bora zisiachwe
6. Ubabe wa kipumbavu uachwe maana palipo na ubabe au udikteta lazima kuwa na uasi/usaliti na palipo na usaliti lazima pawe na mapinduzi.

7. Serikali isijikite kwenye matamko ya kipuuzi puuzi. Kwani kwa kufanya hivyo itaathiri vijana wengi ambao wao kila kitu watataka tamko la serikali.

Sishangai kwa nini watu wanamlaumu Mama kuwa kwa nini ni mpole, ni kutokana na kuathiriwa na matamko yasiyo na kichwa wala miguu.

Sio kila kitu kitolewe tamko kwa kutafuta sifa za kijinga kwenye Kamera ili ionekane kazi inafanyika wakati hakuna kitu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dar es salaam
 
7. Magufuli alifanikiwa zaidi katika kutekeleza na kusimamia maendeleo ya miundombinu, kwa hili nampa heko, lakini nilimuambia kuwa taifa masikini linawekeza kwenye watu na sio vitu,
Hii watu walinipinga lakini huo ndio ukweli mchungu, masikini kuwekeza kwenye vitu zaidi ya watu ni kupoteza muda na kuwatesa watoto.
Kabla ya daraja la sasa hivi, kuna ndugu yangu mmoja aliwahi kupoteza mtoto katika foleni ya ubungo wakati akiwa anampeleka hospitali.

Jamaa ana pesa nzuri tu (maendeleo ya watu) lakini miundombinu mibovu (maendeleo ya vitu) ilifanya apoteze mtoto.
 
8. Magufuli alijitahidi kujifanya hawapendi Wazungu na kila mara alitoa maneno ya kupata ushawishi kwa watu ili wawachukie wazungu. Ndio maana hata Mambo ya Corona aliyaona kama mchezo wa kuigiza na njama za wazungu kutuangamiza.
Angekuwa hawapendi wazungu, angewafukuza mabalozi basi. JPM alikuwa anataka fair play kati ya Tanzania na nchi zingine.
 
1621443035529.png
 
Mwanangu umenikosha Sana , hii nchi ya jabu Sana , kwanini haijaruhusu malipo ya PayPal till now? Visa ni ngumu Sana kwenye hii nchi , Ila wakenya hawana hzo mambo wanatoboka kirahsi Sana , na nje ndo kuna hela Yani ili upate hela lazima jirani umnyonye, umpore au akulipe, ndo mana tunashangaa Leo majamaa kuwekeza hapa nchini Zaid ya makampuni 500 why ? Mitaji wanayo na akili wanayo wameitoa wapi ? Nchi Yao ipo connected na dunia ....

Maghufuli alikuwa anaididimiza sana hii nchi kwenye masuala ya uchumi ....

Mama Samia hawezi kufanya lolote la maana , kete yake ya mwisho ni kuruhusu kusukwa katiba mpya ......Kwa katiba hii hataweza lolote Sana Sana tutakuja kumlaumu , miaka miwili ni mingi Sana atakuwa tayar exhausted... Kama ana sikio la uelewa aruhusu mchakato wa katiba mpya quickly as possible before haijawa toolate .....
 
Well said brother!!Huwa najiuliza "kama ni deep state iliamua jpm ndio awe Raisi nadhani ni maamuzi ya hovyo sana na yameitia unajisi deep state yetu!kwa kuwa haitoaminika tena!!hivi unawezaje kumpa jpm nchi ukijua ni mgonjwa wa nafsi,mwili na roho???huwa nafikiria hadi machozi yananitoka!!"Deep state ifanyiwe reshuffle aiseeh!!!
Hao hao wabovu ndiyo wameishikilia hiyo deep state.

Kimsingi tunahitaji KATIBA ambayo itaweka misingi ya taifa ambayo lazima Rais yeyote ataifuata haijalishi anatoka chama gani.

Tofauti na Sasa kila rais anakuja na mambo yake,hakuna consistency kutoka Rais mmoja hadi mwingine.Kila Rais anakuja na mambo yake kutafuta sifa au legacy.

Mambo hayo mapya lazima yaendane na mipango ya taifa iliyopo katika utekelezaji.
 
JPM hakuwa malaika yule. Yeye pia ni mwanadamu na ana mapungufu yake mengi tu.
Sawa hakuwa malaika, lakini unapokuwa kiongozi wa nchi(raisi) huwezi kuropoka hovyo hovyo kwa kisingizio eti siyo malaika ana upungufu kama binadamu wengine. Kiongozi lazima ajiheshimu. "Baki na mavi yako nyumbani" hayo siyo maneno ya kusemwa na raisi wa nchi hadharani tena kwenye umati wa watu.
 
Sawa hakuwa malaika, lakini unapokuwa kiongozi wa nchi(raisi) huwezi kuropoka hovyo hovyo kwa kisingizio eti siyo malaika ana upungufu kama binadamu wengine. Kiongozi lazima ajiheshimu. "Baki na mavi yako nyumbani" hayo siyo maneno ya kusemwa na raisi wa nchi hadharani tena kwenye umati wa watu.
Hata mimi kuna wakati alikuwa ananikwaza sana kwa kauli zake. Tumsamehe tu mzee baba ndio maisha yalivyo.
 
Back
Top Bottom