Habari Watanzania wenzangu,
Kuna jambo ambalo naamini viongozi wetu huwa wanalipuuza wakifika kwenye viti hivyo.
Japo Tanzania ina utajiri mwingi sana, lakini Watanzania asilimia kubwa ni fukara sana.
Hii ni kuanzia kwa Mawaziri, Makatibu wakuu, viongozi wa Taasisi mbalimbali, Majaji, Bunge na Wabunge, Wawakilishi, Waziri Mkuu, Makamu na Rais; wote hawahisi kabisa magumu wanayopitia wananchi wengi waliopo ktk umaskini wa kutupwa.
Ukitaka kuthibitisha hili, angalia sera mbalimbali zinazotungwa na serikali. Haziakisi kabisa hali ya maisha ya Watanzania wengi!
SWALI: Shida ni nini?
Tuna sera za kijinga sana, tuna maamuzi mengi ya kipumbavu kweli kweli. Nchi imejaa mikorogano tu.
Ukiulizwa hii sera alitungiwa Mtanzania, hadi unahisi uchungu hadi moyo unataka kuchomoka.
Hawa akina Mwigulu, na Rais wetu Mh. Samia wana shida gani hasa?! Au shida ni vile ving'ora, au saluti wanazopigiwa, au misafara mikubwa mikubwa ile, Mbona hawaelewi kabisa uhalisia wa maisha ya WaTz wengi!
Niliwahi kusafiri hadi Bukombe, Geita huko. Nilimkuta Mwananchi mmoja, ameugua kweli, lakini kwa sababu alikuwa na Sh. 2000 tu. Hiyo hiyo anaitegemea kula, kuhudumia watoto, na kila kitu. Yule ndugu alichukua uamuzi wa kwenda kununua paracetamol (dawa za maumivu) za sh. 400/- ili ameze japo atulize maumivu ya mwili.
Watanzania wa aina hii wapo chungu mzima nchi hii. Mtu anaumwa, hana hela ya kumuona daktari, hana fedha ya vipimo, na wala uwezo wa kununua dawa. Anaamua kununua tu dawa za maumivu.
Si kwamba hapendi kutibiwa, la hasha, kipato kinakataa.
Nikuulize Mh. Rais Samia, huyu Mtanzania akitumiwa na ndugu yake sh 25,000/- aende hospital, mtumaji anakatwa tozo, na yeye akienda kutoa ana tozo. Rais wangu na wewe Dr. Mwigulu mnatengeneza Uchumi wa watu gani? Huu sio wa WaTz, labda mna watu wenu wengine mnaowawaza na kuwahudumia.
Ni wakati sasa Mh. Rais Samia ukate matumizi yote yasiyo ya lazima ndani ya serikali yako.
Haiwezekani Waziri, Naibu Waziri, Katibu mkuu, Wakuu wa Taasisi, Mamlaka mbalimbali, mkuu wa mkoa, n.k, atembelee gari ya thamani ya Tsh. 400 million, huku kuna Kijiji kizima hakina Zahanati, Kuna shule haina choo, kuna shule hawana madawati. Halafu unaweka Tozo kwenye sh. Elfu 10, unajiita Mzalendo, na tai ya rangi ya Tanzania unavaa. UNAFIKI!
KATA MATUMIZI YOTE YASIYO YA LAZIMA, KABLA HATUJAKWAMA KAMA TAIFA.
Watanzania ni fukara sana. Isipokuingia akilini hii, 2025 watakulazimisha upishe mwingine.