Rose Mayemba
JF-Expert Member
- May 7, 2012
- 721
- 1,017
Siasa za Tanzania zimekaa kisanii sana,kila mtu anayejiona ana uwezo wa kulaghai hujitafutia tiketi ya kuingia Ikulu ama Bungeni.Hakuna sheria yoyote kwa ajili ya hawa watu hasa inapotokea wamekwenda kinyume na matakwa ya waliowachagua.
Nilitoa mapendekezo yangu kwenye tume ya Warioba kwamba katika katiba wanayoiandaa mbali na wananchi kuwa na mamlaka ya kumwondoa pale wanapoona hatendi sawa na walivyomtuma lakini pia iwepo sheria ya kuwaadhibu pale wanapoonekana kutokutekeleza yale waliyoyaahidi wakati wa kuomba kura pindi wamalizapo muda wao wa uongozi.
Baba wa taifa aliwahi kusema" ili Tanzania iwe IMARA ni lazima tuwe na UONGOZI BORA,ARDHI PAMOJA NA SIASA SAFI"
Lakini sasa hatuwezi kuwa na UONGOZI BORA kwani viongozi wengi tulionao tuliwapata kwa siasa CHAFU,zilizojaa UONGO na ukiukwaji ya maadili.
Mimi nitaendelea kusema hatutapata kuendelea TANZANIA hata tukibadilisha vyama kila siku hadi hapo tutakapopunguza hii idadi ya watu wanaokwenda kuneemesha matumbo na familia zao huku wakiancha wananchi wanateseka.Na mbaya zaidi huachwa tu kama wafalme huku wakiwa wamekengeuka maadili ya kitaifa.
THINGS WILL CHANGE BUT WE NEED TO CHANGE OUR SELVES FIRST