Niliwahi kuandika" Ni muda wa Mahabusu kupewa heshima malangoni pa watesi wao"

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Siasa za Tanzania zinazidi kuwa ngumu kila uchwao. CCM ilidhani uimara wa chama nikushinda uchaguzi wakasahau hata ushindi wa uchaguzi ni sayansi.

Leo hii wanawake wa CHADEMA walioteswa bila hatia kwa kutiwa ndani nakutolewa kwa miaka wanadaiwa ni wanawake wa shoka na hivyo wanakaribishwa CCM. Leo hii hakuna kwenye hotuba na mazungumzo ya CCM wanapowasifia wanachama wao. Hii inatoa tafsiri kwamba ccm imeshindwa kuandaa viongozi hadi watoke upinzani.

Kitendo Cha wapinzani kupewa nafasi kinadhihirisha Wana watu sahihi na wanaongea yaliyosahihi.

Swali, je wakienda huko watafanya kile kinachokusudiwa? Wataendelea kuwatetea wananchi chini ya mfumo wa ccm ambao hauruhusu kukosoa wakubwa?

Je, waliotuaminisha Hawa Ni wapinga kila kitu nakukataa kupokea mawazo yao wamelikwamisha Taifa kusonga mbele kwa kiasi gani?

Hakuna chama Cha siasa kinachokuzwa kwa kusajili safu kutoka upinzani, chama Cha siasa ujengwa kwa kuandaa watu ndani ambao wataaminika.

Dr Bashiru na Polepole mnaamini mlikuwa mnaongoza CCM kwa mfumo wa ccm au mliongoza ccm kwa mfumo wa CHADEMA kwa kusaidiwa na dola? Hongereni wakinamama kwa kuendelea kuchanja mbuga kupokelewa na watesi wenu, kumbukeni hadithi ya Esta kwenye Biblia.....mnalojukumu lakutuokoa mkipata nafasi yakufanya hivyo.
 
njaa kali ubinafsi na ujuwaji ni tatizo kwa kila mtanzania hasa walio viongozi
 
Back
Top Bottom