SoC 2022 Nilivyoweza kuongeza kipato kutoka milioni 1 hadi milioni 14 kwa mwezi

Stories of Change - 2022 Competition

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
823
2,079
Huu ni uzi kwa ajili ya wale ambao wameajiriwa hasa katika sekta binafsi kwa ajili ya kuwatia moyo wa kukuza uchumi wao.

Mimi ni mhitimu wa degree ya masuala ya Sayansi.Miaka 6 iliyopita, nilikua nimeajiriwa sehemu ambapo nilikua nalipwa kiasi cha shilingi milioni 1 tu kwa mwezi. Sikuridhika kabisa na kipato hiki, na nilikua na njaa sana kali sana ya mafanikio.

Hivyo pale kazini nilikua mtu wa kujifunza vitu vingi sana na kwa haraka mno, ndani ya miezi 6 tu, nilikua najua vitu vingi sana na nikawa kati ya mihimili pale kazini, ilikua ni kawaida kabisa mimi kuingia saa moja kamili asubuhi na kutoka saa kumi na moja na nilikua napiga mzigo hasa.

Baada kama ya miezi 7 tangu nianze kazi, nikaanza kuomba kazi sehemu mbalimbali, ilinichukua kama miezi 5 hivi, nikapata shavu lingine, ambapo kazi mpya nilipanda mshahara mara mbili na nusu, na kuanza kulipwa milioni 2.5. Siku nimeandika e mail ya ku resign ilikua ni balaa na nusu.

Nilipigiwa simu na maboss waliokua juu yangu zaidi ya watatu kila mmoja akitaka kujua kwa nini naondoka na nini wafanye ili nisiondoke.

Jibu langu ambalo nilishaliandaa maana nilijua haya yatatokea, lilikua tu ni kwa sababu tu ya kukua kikazi na hakuna ubaya wowote, na sio kwa ajili ya ubaya wowote. Na niliwaeleza kuwa huko niendako nimepata cheo zaidi na nimekua zaidi pia kiuchumi.

Baada ya majadiliano mengi sana na marefu, hatimaye waliniachia, ila walisikitika sana na wakanitakia kila la kheri.

Baada ya kuanza kazi kampuni namba 2, mwendo ulikua ni ule ule, nilikua nachapa sana kazi na kujifunza mambo mengi sana, na hii kampuni pia ilikua na wigo mpana zaidi wa kujifunza mambo mengi kama ukiwa ni mtu mwenye hamu ya kujifunza.

Niliendelea na uchapa kazi, baada ya kuona sasa nimekusanya uzoefu na ujuzi wa kunitosha kusonga mbele, baada ya kama miaka miwili hivi nilianza kuomba kazi sehemu zingine kama kawaida yangu, ilinichukua kama miezi 7 hivi tangu nianze ku apply nikawa nimepata kazi sehemu nyingine tena. Kama kawaida, nikaandika barua ya kuacha kazi, habari ikawa ile ile ya kuitwa na kuulizwa imekuaje tena, nami jibu langu likawa lile lile kama ile kampuni ya mwanzo kuwa ni kukua tu kikazi, nikachapa zangu lapa, nikaanza kazi kampuni namba 3. Hii kampuni ya 3 niliyoingia niliingia kwa mshahara wa milioni 4.5.

Nikaingia mzigoni kama kawa. Hapa nilifanya kazi kama mwaka mmoja na miezi mitano hivi, nikawa nimepata nafasi sehemu nyingine tena kwa nafasi kubwa zaidi, na hii kampuni namba 4 niliingia kwa dau la mshahara wa shilingi milioni 7.6.

Hii kampuni namba 4 nilikua pia napiga mzigo kweli kweli.... Yaani sio mzigo wa kitoto aisee, mimi ni aina ya watu ambao wakiipenda kazi wanaifanya kutoka moyoni kweli kweli, na kama mnavyojua Watanzania wengi ni wavivu, kwa hiyo akitokea "jembe" mmoja kwenye nafasi fulani akawa anapiga mzigo, basi kazi nyingi anakua anasukumiwa huyo ambae sio mzinguaji.

Basi ndivyo ilivyokua kwangu, wenzangu ambao nilikua nao level moja ikawa kazi nyingi wanazisukumia tu kwangu, na ambae tulikua tunaripoti kwake na yeye kwa sababu pia alikua anaona akinipa kazi naifanya vizuri na kwa wakati kuliko wengine, kazi nyingi pia akawa ananitupia mimi, ikiwa pia na baadhi ya kazi zake yeye, akibanwa basi ananitupia tu mimi. Hii ilinipa faida moja kubwa sana, nilijikuta najifunza vitu vingi na vikubwa sana ndani ya muda mfupi mno, japokua ilinifanya kuwa na kazi nyingi sana.

Kwa sababu bosi wangu alikua kwenye nafasi za juu, ile kunipa baadhi ya majukumu yake ikanipa ujuzi na uzoefu adimu sana wa kiuongozi.

Fitna za hapa na pale kama mnavyojua tena sehemu za riziki hazikosekani, yakaanza maneno kuwa jamaa anapendelewa sana, hivi na vile. Ila yule bosi wangu aliniambia, usijishughulishe na majungu, wewe piga kazi utafika mbali sana.

Basi, imepita kama mwaka na miezi 5 hivi, sina hili wala lile, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni moja hivi kanicheki LinkedIn paaap...!! Akaniuliza tu utakua interested kwa nafasi fulani hapa kwetu, kuna mtu ameku recommend kwangu kwa hii nafasi, na nimeangalia profile yako nimeona utatufaa, kama uko tayari nikuunganishe na HR apange siku ya usaili tukusikilize. Na hiyo nafasi aliyoisema ni nafasi kubwa, sio ndogo.

Moyo ukashtuka sana, ila nikasema sawa, niko tayari ku explore hiyo nafasi. Akasema sawa haina shida, baadae HR wao akanicheki, akanipangia usaili wiki inayofuatia.

Nikapiga raundi 5 za usaili ndani ya miezi miwili, na bila kutarajia nikawa nimefaulu usaili na kupata hiyo nafasi, ambayo ndio naitumikia hadi sasa, ambayo mshahara wake ni Shilingi za Kitanzania milioni 14, na marupurupu kibao (posho ya nyumba laki 5, posho ya mafuta laki 5, posho ya mawasiliano laki 2). Kumbuka kuwa nina degree moja tu hadi sasa (Bachelor), na classmates wangu hakuna hata mmoja ambae amefikia level ya nafasi niliyonayo pamoja na kwamba wengi tayari wana Masters.

Kufanya kazi kwa bidii kubwa na kuipenda kazi unayoifanya kunalipa sana. Vijana mlioajiriwa msijibweteke, pigeni kazi na kujifunza mambo kwenye kazi zenu kila siku, ila usikae sana sehemu moja muda mrefu, kwani kuna uwezekano wa kuzoea kazi na hivyo kutojifunza lolote jipya.Unakuta kijana kakaa kampuni moja ya binafsi miaka 5 sijui 8 au wengine 10+. Unatafuta nini? Hapo unakua huna jipya tena, unaenda kazini kupasha moto siti tu wala huna jipya lolote.

Pia, msiogope kuwa risk takers hata ukiwa umeajiriwa, usiache kuomba kazi sehemu zingine kila mara kwani kila unapohudhuria usaili ni nafasi ya kujinoa zaidi makali yako sokoni na kujiuza zaidi. Msishau pia "kuji-brand", mimi ukiona profile yangu ya LinkedIn ni hatari namna ilivyo, mtu akiingalia tu anajua huyu yupo serious na anaipenda kazi yake.

Mwisho, hakikisha unaondoka kwenye kampuni huku kila mtu akiwa anatamani kuwa ungeendelea kubaki, na si kinyume chake.
 
Upvote 101

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
2,873
5,998
Asante kwa mtazamo wako. Uzuri sina control na mtazamo wako, huo ni utashi wako binafsi. Natamani ningeweka screenshot za mikataba yote hapa. Endelea tu kutoamini.
Nishakupigia kura mkuu.. kama hutojali naomba unitajie jina la kampuni unayofanyia kazi nije nikupe hi tubadilishane hata mawazo kidogo.
 

Attachments

  • Screenshot_20220827-082053.png
    Screenshot_20220827-082053.png
    246.9 KB · Views: 53

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
823
2,079
Mchawi mwingine huyu. Jina la nini.

Huyu jamaa Kwa kipato chake sidhani kama anashida ya kura. Japo nitagusa pale ku vote.

Anyway. Nimejifunza jambo kubwa Sana. Nilianza kazi 2000 Mwaka mmoja baadae nikahama, minne badae baadae nikahama, sita baadae nikahama tena, baada ya 10 nikahama tena. Baada ya 2 nikapigwa chini cheo pwaaaaaa nipo Kwa kunywa kabisa huku Kwa kajamba nani.

Nilikuwa nafanyakazi Sana nilikuwa mtu ambaye pale bosi anapohitajikazi ifanyike haraka akiniita mimi.

Ilikuwa, kama ilivyokuwa kwako mleta Uzi kazi zote natupiwa Mimi. Sikujali nilifanya kwa bidii, usiku na mchana. Lakini baadae nimekuwa nikilia. Kwa Umri wangu ndg msomaji utagundua nimeshafika 50. Kumbuka Nina spidi ya jutosha tu sijachuja pamoja na age yangu
Asante sana mkuu. Kuwa extra ordinary sio rahisi sana, ndio maana wengi wanachagua kuwa ordinary.
 
85 Reactions
Reply
Top Bottom