Nilivyouziwa msaada kwa Tsh 28,000 nikaubadili na kupata zaidi ya milioni 3 ndani ya siku 35

Ashukuriwe Mungu muweza wa yote. Siyasemi haya kwa kujikweza bali kwa manufaa ya kujifunza kwa wale wanaotafuta mitaji au biashara ya kufanya .

Msaada ni kitu cha bure (ukimsaidia mwenzio ni sawa na umemkopesha Mungu) ila kwenye upande wa biashara haikua rahisi ilibidi ninunue msaada kwa jumla ya 28000 Tsh. Kutoka kwa watu watatu. Mtu wa kwanza aliniuzia kwa 10000tsh wa pili aliniuzia kwa 10000tsh na wa tatu aliniuliza kwa 5000tsh pamoja na 3000tsh niliyo mpa ya lunch.

JINSI WAZO LILIVYO ANZA
Ilikua tarehe 06 mwezi wa 02 siku ya jumamosi mida ya saa tano asubuhi ..nilikutana na kijana mmoja alie shikilia biashara yake mkononi ( mzigo wa boxer ..chupi za kike pamoja na mikanda ya kiume )ilikua katika pitapita zangu kariakoo kufanya manunuzi ya kawaida ... alinisimamisha sikusimama, huwa wanatabia ya kumfata mtu huku wakitaja bei ...ilibidi nisimame baada ya kunitajia chupi moja anauza 3500 tsh,, chupi ambayo nilinunua duka la mtaani kwa 6000tsh ...nilimuambia nitanunua ila nina maongeze nae ya dakika 5 , bila hiana akakubali !! Swali langu lilikua rahisi sana ila sikutegemea kuwa jibu lake ningelinunua ...

Nilimuuliza KWANI HIZO CHUPI UNANUNUA DUKA LIPI KWA JUMLA? alinijibu hiyo ni biashara nyingine tumalize kwanza biashara hii ya kwanza tuingie biashara nyingine ..sikumuelewa mwanzo ila nilitoa 10000tsh akanipa chupi tatu ..alafu akaniambia niulize upya huku akinyoosha mkono wake kuashiria anataka jero yake iliyo baki ,, nililialia kwa maneno ya mnunuzi akapotezea ile jero .... nilivyo muuliza mara ya pili alisema kama nataka kuelekezwa nitoe 5000tsh na kama nikitaka kupelekwa nitoe 5000tsh nyingine nilicheka sana ila hakuonesha dalili hata ya kupepesa macho ikabidi nikubali ... nifupishe tuu story alinipeleka duka husika anapo nunua reja reja na akanionesha maduka mawili mengine ya ziada. Niliulizia bei nikakuta ananunua kwa 1500 mpaka 2000 pia ziko quality nzuri zaidi na bei pia inakua kubwa ila siyo kubwa ya bei ya mtaani pia alikua anauza sidiria na vitu vingine vingi kwa bei ya jumla...

Siku inayo fuata 07/02 jumapili niliitumia kurudi kariakoo kuelewa zaidi sehemu nitapo pata mahitaji yangu kwa bei ya jumla .... nilimkuta kijana mmoja yuko na kitolori flani kwa juu ameweka perfume na bodypray ...nilimuuliza swali lile lile KWANI UNANUNUA WAPI KWA BEI YA JUMLA ? ..jambo la kunisaidia ALINIUZIA JIBU KWA 5000tsh na muda wa kurudi tulikaa sehemu na yule kijana tukanywa soda na yeye alikula miogo ya buku jumla nililipia 3000tsh.... mtu wa tatu alikua mtu wa nguo nae linifanya hvyo hvyo na aliniuzia taarifa kwa 10000 ...

JINSI NILIVYO BADILISHA MSAADA NILIO UZIWA KUWA SEHEMU YA KITEGA UCHUMI CHANGU NA KUTENGENEZA MILIONI TATU (3M)
Njia niliyo itumia hata wewe unae soma hivi sasa unaweza kuitumia sehemu yeyote ile na muda wowote ule. BIASHARA NI UAMINIFU miongoni mwa story tulizo ongea na kijana yule alie nipeleka kwenye duka la vipodozi vya jumla aliniambia mara nyingine huwa anaacha simu yake kwa muuza duka anapewa mzigo anaenda kuuza akifanya mauzo anarudi kuikomboa simu yake akishindwa kuuza basi anarudisha bidhaa ( ila inategemea na aina ya bidhaa na uaminifu ulio jijengea kwa muuzaji)

Hatua ya kwanza niliyo tumia
ilikua tarehe 07/02 jumapili nilinunua mzigo wa nguo za ndani wa thamani ya 30000
Mchanganuo wa mzigo.... 20000 nilikua nayo cash
10000 nilipewa chupi tano ziada nikaweka na simu yangu ndogo rehani (nilifanya makusudi ili yule mwenye duka asinisahau na ili nitengeneze uaminifu ) ... nilichukua chupi zenye ubora wa kati kwa 2000tsh kwa chupi moja niliondoka na mzigo wa chupi 15 ... nilivyo fika zote niliziuza kwa wadada wa kazi nyumba za jirani chupi moja niliuza kwa 4000 ... ziliisha zote nikapata 60000tsh ...30000 bei ya mzigo na 30000 faida ( soko langu lilikua wadada umri wa miaka 15 -30 )

Hatua ya pili niliyo tumia kukuza mtaji
Siku iliyo fuata 08/02 niliomba udhuru kazini nikaenda duka nililo acha simu nikakomboa simu yangu ndogo ... ila nikasema nataka mzigo mkubwa kidogo wa kama laki mbili na sikua na hela zaidi ya 40000 pamoja na simu yangu kubwa ( simu yangu ilikua na thamani ya laki tano na ushee ) alikubali nikachukua mzigo wa laki mbili ..nilirudi mtaani nikauza baadhi na nikatembeza kwa marafiki zangu salon nikauza kwa marafiki zangu kazini ...ndani ya siku tatu mzigo uliisha wote na nilikua na cash ya 467000 ukitoa laki mbili ya mtaji nilibakiwa na 267000 kama faida nilirudi nikakomboa simu yangu

Nilichukua mzigo mwingine wa 120000 duka la kwanza ... duka la vipodozi nilichukua mzigo wa 50000 na nilichukua baadhi ya nguo za jumla za 70000 ... nilipambana sana kuanzia 12/02 mpaka tarehe 16/02 nilinaliza mzigo wote sikukopesha hata mia ... CHA MUHIMU SI KUMALIZA MZIGO BALI KUTENGENEZA WATEJA WENGI NILIO JUANA NAO NA BAADHI YAO NI WANAFUNZI WA CHUO ... kwa mzigo wa pili nilitengeneza faida ya zaidi ya 340000 pamoja na mtaji nilio kuwa nao nilikua na jumla ya 580000tsh
Nilitafuta dada mmoja atae nisaidia kazi kipindi ambacho nakua kazini kwa makubaliano ya 20000 kwa week akimaliza mzigo nitao muagiza sehemu za kupeleka

Mzigo wangu wa tatu ulikua mkubwa kidogo (500000) kwa mfanya biashara mdogo kuzungusha mzigo wa laki tano si kazi rahisi ... ila wale wateja wa chuo walikuwa watetezi wangu nakila alie niletea mteja mpya sikusita kumpa kazawadi ... nilichukua mzigo wangu wa tatu tarehe 22/02 na nilimaliza tarehe 04/03 faida ilikua zaidi ya laki 500000 pamoja na mtaji husika nilikua na zaidi ya milioni moja ...

MUNGU ALIKUA PAMOJA NA MIMI NIKAPATA WATEJA WA MIKOANI PIA ... baadhi ya wateja walikua wanachuo na wengine ni ndugu niliwauzia mzigo wa kutosha nao baadhi wanafanya biashara kama hii huko kwa mzigo ninao watumia

MAZINGATIO

1. MWAMINI MUNGU

2. Kila unae muona anauza bidhaa kunayo faida anapata ( MUULIZE HAKIKISHA UNAFAHAMU NI WAPI ANANUNUA MZIGO WAKE KWA JUMLA )

3. Kwenye swala la hela USIAMINI MTU YEYOTE ..NARUDIA YEYOTE YULE

4. Tengeneza fursa mwenyewe ..fursa itayokupa hela huitiwi Mungu atakukutanisha nayo ... wanasema UKIITWA KWENYE FURSA BASI WEWE NDIE FURSA hawajakosea

4. Biashara ya KUKOPESHA ITAKUSIMAMISHA KAMA SI KUKURUDISHA NYUMA .. nimeliona hilo ndani ya siku hizi nilizo fanya biashara hii .. usikopeshe kama hauko tayari kupoteza

NIMEFANYA LEO MAJUMUISHO NIMEJIKUTA NINAYO ZAIDI YA MILIONI 3 PAMOJA NA MIKOPO ILIYO MIKONONI MWA WATU ASHUKURIWE MUNGU

Usimdharau mtu yeyote yule. kama 20000 pamoja na simu rehani inaweza kumpa mtu zaidi ya milioni 3 ndani ya siku 35 .. MAALUMU KWA WAFANYA BIASHARA NDOGO WENYE MITAJI YA SIMU UNAYO TUMIA MPAKA LAKI NASEMA INAWEZEKANA.

Kwa hii speed baada ya mwaka utakuwa haukamatiki. Hongera sana Mo ajae.
 
Umeniinspire ngoja niandae mtaji nianze biashara. Nisisubiri ajira
 
Back
Top Bottom