Nilivyosave Milioni 10 kwa miezi 6 na kujenga nyumba mbili na kununua gari zuri

Hongera sana. Mie nimekuelewa kua ukiwa na malengo flani ni vizuri kujibana na kuongeza njia zingine za kipato ili uyafikie.

Halafu nyie mnaoshangaa kusave 10 millions kwa miezi sita angalieni maisha aliyokua anaishi kwa hesabu za haraka hakua anatumia zaidi ya laki 3. So kwenye mshahara pekee aliweza kupata million 6.

Na hizo side hustle kumletea million 4 kwa miezi sita ni sawa mbona sio kitu cha ajabu. 4 millions kwenye biashara/deals nzuri kwa miezi sita? Inawezekana.
 
Hongera sana. Mie nimekuelewa kua ukiwa na malengo flani ni vizuri kujibana na kuongeza njia zingine za kipato ili uyafikie.

Halafu nyie mnaoshangaa kusave 10 millions kwa miezi sita angalieni maisha aliyokua anaishi kwa hesabu za haraka hakua anatumia zaidi ya laki 3. So kwenye mshahara pekee aliweza kupata million 6. Na hizo side hustle kumletea million 4 kwa miezi sita ni sawa mbona sio kitu cha ajabu. 4 millions kwenye biashara/deals nzuri kwa miezi sita? Inawezekana.
Asante sana, yale maisha yainifunza mambo mengi sana kwa muda mchache, jambo ambalo ningelifanya kwa miaka 15 nililifanya kwa miaka pungufu ya sita.

Ninausoma upepo wa nini cha kubana hapa kwangu nilipohamia hasa nauli za kufika kazini na matumizi ya familia pamoja na kuongeza njia zaidi za kupata kipato nje ya ajira ili nifikie lengo lingine kubwa. Inawezekana!
 
Wakuu salaam,

Nimeona kuna mada ya mambo ya kusevu nikaona nishee story yangu inaweza kuwa msaada kwa mtu fulani sehemu fulani..

1. Take home ilikuwa ni 1,300,000 baada ya makato yote kazini pamoja na benki wakati wa kutoa

2. Tulishusha maisha tukawa tunaishi nyumba ya kupanga ya chumba kimoja elfu 35000 kwa mwezi, jirani kabisa na kazini, ninatembea kwa miguu saa moja nimeshafika. Mwanzo tulikuwa ninakaa nyumba ya 900,000 kodi ya miezi sita bado na umeme juu.

3. Nikaacha kula bia na nyama kila siku, nikawa ninakunywa mbili mwisho wa wiki na nyama nusu

4. SIkupanga nyumba ya umeme, nilikopa sola ya Zola ule mtambo mdogo wa kulipia 10000 kwa mwezi

5. Bima, pampers na vyakula special vya mtoto (maana sometimes wanachagua sana vyakula wakiwa wadogo) nikaweka bajeti ya 150,000 hapo pamoja na bima yake

6. Ikitokea shida sikuwa ninakopa kwa benki, ninakopa kwa marafiki

7. Nikawa nina kazi za mishemishe na dili za hapa na pale ukijumlisha udeiwaka na udalali mida ya jioni na wikiendi na nje ya Ofisi

Nilipofanya hayo yote niliweza kusevu milioni 10 ndani ya miezi sita ya mwanzo na kuendelea, IKAWA NDIYO DESTURI YANGU kwa miaka kadhaa mbele, hapa ninavyoandika hivi sasa nina gari ya kifahari SUV na nina nyumba ya zaidi ya milioni 30 ninayoishi na familia yangu (bado haijaisha finishing) na mama yangu nimemjengea nyumba ya milioni saba huko Kijijini kwetu.

Nimejifunza: FANYA IBADA, punguza bajeti za kifamilia, kama umepanga kakae jirani na Ofisi, ongeza njia za kupata kipato, sevu, wekeza. Utafikia lengo.
Kumbe wewe una vyanzo vingine vya mapato ila inatutajia tu mshahara wa 1.3M.

nyie inspirational speakers mna matatizo gani.
Mnafaidika nini kqa kusema uongo?

1.3M - 35000 kila mwezi - 15000 za mtoto
 
Kazi ya kuajiriwa: Casino Manager
Kazi za nje zote ni halali kabisa: ninaandikia makala kampuni ya utalii, nina mashine ya dubu, sometimes watu wanataka niwasaidie kufanya maboresho ya kasino zao siku za wikiendi, nimo humo, hizo zote haziathiri kazi yangu ya mkataba.

Nilipanga Kigogo Sambusa, Dar, na Ofisi zipo Posta. Nikitembea taratibu sana nilikuwa ninatumia masaa mawili kufika kazini. Kwa mwendo wangu ni saa moja nimeshafika.

Kwa sasa siishi maisha hayo sababu lengo langu lilikuwa kujenga haraka ndani ya miaka mitano au sita na kupata usafiri. Nilifanikiwa.
Mmh casino manager, kazi za casino zinakuaga za shift sana na weekend kupata off casino ni ndoto za alinacha maana ndo siku za kazi,sasa ulikua una manage vipi huo mda? maana kuna mda unaingia night inabid upumzike mchana em nieleweshe mkuu na kigogo kulivo mida ya night pia ulikua unatembea wajuba wanakuacha salama
 
SUV ni ya kununua kwa mtu kwa milioni 6 hivi pamoja na ufundi kidogo kuirekebisha, siyo miaka 3, ni zaidi ya sita sasa mkuu
So, ni 6M… sio “approximate 20M”?

But story yako inajenga. La msingi mtu ni kuwa na GOALS zenye timeframe then kustrategize the HOW to reach malengo hayo

Kupendapenda starehe na kula bata kwa sana hakuwezi kumfikisha mtu kwenye malengo yake
 
Kumbe wewe una vyanzo vingine vya mapato ila inatutajia tu mshahara wa 1.3M.

nyie inspirational speakers mna matatizo gani.
Mnafaidika nini kqa kusema uongo?

1.3M - 35000 kila mwezi - 15000 za mtoto
Sijaelewa kwanini umefocus kwenye mshahara. Lengo halikuwa kuelezea mshahara. Nimeelezea namna nilivyofikia ndoto yangu ya kusevu milioni kumi. Rudia kusoma
Mmh casino manager, kazi za casino zinakuaga za shift sana na weekend kupata off casino ni ndoto za alinacha maana ndo siku za kazi,sasa ulikua una manage vipi huo mda? maana kuna mda unaingia night inabid upumzike mchana em nieleweshe mkuu na kigogo kulivo mida ya night pia ulikua unatembea wajuba wanakuacha salama
Kigogo Sambusa unaijua? Ipo Ilala Msimbazi. Siyo Kigogo unakosema wewe.

Off yangu ni Jumapili na Jumatano. Siku nyingine zote ni night shifts.
 
So, ni 6M… sio “approximate 20M”?

But story yako inajenga. La msingi mtu ni kuwa na GOALS zenye timeframe then kustrateguze the HOW to reach malengo hayo

Starehecna kula bata kwa sana hakuwezi kumfikisha mtu kwenye malengo yake
Hakika mkuu. Malengo yanafikiwa kwa kuzipa talaka starehe na bata. Sikuwa na uwezo wa kuwaza kununua gari ya m20.
 
Sijaelewa kwanini umefocus kwenye mshahara. Lengo halikuwa kuelezea mshahara. Nimeelezea namna nilivyofikia ndoto yangu ya kusevu milioni kumi. Rudia kusoma

Kigogo Sambusa unaijua? Ipo Ilala Msimbazi. Siyo Kigogo unakosema wewe.

Off yangu ni Jumapili na Jumatano. Siku nyingine zote ni night shifts.
Mkuu unaelewa maana ya kuserve? Total minus consuption, Kinacho baki ndio kusevu. Sasa wewe unachukua A+ B unasema umeserve??😅😅
 
Hahaha, mkuu ningeendelea na yale maisha muda huu ningekuwa ninaongea mambo mengine, ni kwa vile tu malengo yangu ya miaka mitano yalitimia, ninashukuru Mungu hii haikuwa ndoto. Ingawa ni ndoto kwa wengine lakini ninawasihi kuwa inawezekana hata kwa kipato cha laki nne.

Ndiyo mkuu, mimi ni mtaalam wa mambo ya kasino, hivyo ninafanya udalali huo wa mambo yote ya kasino na kazi zinalipa kweli, pia kuna udalali mtu amepewa kazi aandike makala fulani anakwama ninakuwa ninazifanya, kazi zinatokea kuzidi za mishahara ila ni kwa misimu. SHukrani kwa kumfungua akili mdau huyo
Mkuu nipigie shavu la kazi kazini yoyote ata kama ni usafi ntashukulu sana nipo dar
 
Back
Top Bottom