Nilivyosave Milioni 10 kwa miezi 6 na kujenga nyumba mbili na kununua gari zuri

Hiyo namba 7 haiywezi tosheleza vitu ulivyosema ulivyosema umekamilisha. Na hapo bado hujahudumia kwa wakwe. Nao wakwe uliwajengea nyumba pia?
Wakwe sikuwajengea. Focus ilikuwa nyumbani kwangu kwanza, kisha mzazi wangu na huenda miaka ya mbele nikafanya kitu kwao. Mungu Mwema Atasaidia.

Namba 7 nikitoa mfano kuna mwaka mmoja nilikuwa ninafanya udalali wa mazao ya shambani kwenye masoko siku za wikiendi hivyo nilikuwa kwa mwezi ninapata zaidi ya hata mshahara. Ndiyo maana nikasema kule juu kuwa kazi za nje (side hustle) ndizo zilizonitoa zaidi.
 
If at all this is true..Hapo kwenye "side hustles" ndio msingi wa Maendeleo yako..na wala si hiyo takehome..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Naam, hakika na kweli. Umuhimu wa take home ni kitu cha uhakika kila mwezi. Kazi za pembeni ni za msimu, kuna nyakati sipati faida na kuna nyakati faida ni mara nyingi kuzidi take home. Ndiyo maana ninapenda sana wote tujifunze kufanya mambo mengi bila kudharau kazi za kuajiriwa.
 
Kwanza hongera sana mkuu kwa nidham ya ku save na juhudi.

Pili, hata kama ni kwa juu juu, unaweza kuwaambia raia hizo kazi za nje ni za aina gani? Ni clean money? Yaani mihangaiko halali na bado kazi yako ya kuajiriwa unaifanya kwa ufasaha?

Mwisho umebahatika kupata chumba cha bei rahisi karibia na kituo cha kazi. Kwa huo mshahara wa take home 1.3M, ilitakiwa ofisi iwe maeneo yaliyochangamka kidogo kiasi kwamba gharama za makazi ziwe juu. Lakini wewe umepata chumba cha 35,000/- tena hakina umeme na ni mwendo wa kutembea kwenda ofisini. Hongera sana
 
Wakuu salaam,

Nimeona kuna mada ya mambo ya kusevu nikaona nishee story yangu inaweza kuwa msaada kwa mtu fulani sehemu fulani..

1. Take home ilikuwa ni 1,300,000 baada ya makato yote kazini pamoja na benki wakati wa kutoa

2. Tulishusha maisha tukawa tunaishi nyumba ya kupanga ya chumba kimoja elfu 35000 kwa mwezi, jirani kabisa na kazini, ninatembea kwa miguu saa
Ukiamka futa hii post

ila ndoto yako tamu
 
Kwanza hongera sana mkuu kwa nidham ya ku save na juhudi.

Pili, hata kama ni kwa juu juu, unaweza kuwaambia raia hizo kazi za nje ni za aina gani? Ni clean money? Yaani mihangaiko halali na bado kazi yako ya kuajiriwa unaifanya kwa ufasaha?

Mwisho umebahatika kupata chumba cha bei rahisi karibia na kituo cha kazi. Kwa huo mshahara wa take home 1.3M, ilitakiwa ofisi iwe maeneo yaliyochangamka kidogo kiasi kwamba gharama za makazi ziwe juu. Lakini wewe umepata chumba cha 35,000/- tena hakina umeme na ni mwendo wa kutembea kwenda ofisini. Hongera sana
Kazi yako please
Kazi ya kuajiriwa: Casino Manager
Kazi za nje zote ni halali kabisa: ninaandikia makala kampuni ya utalii, nina mashine ya dubu, sometimes watu wanataka niwasaidie kufanya maboresho ya kasino zao siku za wikiendi, nimo humo, hizo zote haziathiri kazi yangu ya mkataba.

Nilipanga Kigogo Sambusa, Dar, na Ofisi zipo Posta. Nikitembea taratibu sana nilikuwa ninatumia masaa mawili kufika kazini. Kwa mwendo wangu ni saa moja nimeshafika.

Kwa sasa siishi maisha hayo sababu lengo langu lilikuwa kujenga haraka ndani ya miaka mitano au sita na kupata usafiri. Nilifanikiwa.
 
Ukisevu mshahara wako wote kwa miezi sita bila kutumia kiasi chochote ni 1300000x6 =7,800,000 . Sasa hebu tueleze boss, hiyo 10m uliipataje kwa miezi 6 au wewe ni chuma ulete?
KASEMA Ana mishe mishe zingine nje ya ofisi,ANAPATA udalali it means yaeezekana jamaa Ni meanasheria,land valuer etc
 
Ukiamka futa hii post
Hahaha, mkuu ningeendelea na yale maisha muda huu ningekuwa ninaongea mambo mengine, ni kwa vile tu malengo yangu ya miaka mitano yalitimia, ninashukuru Mungu hii haikuwa ndoto. Ingawa ni ndoto kwa wengine lakini ninawasihi kuwa inawezekana hata kwa kipato cha laki nne.
KASEMA Ana mishe mishe zingine nje ya ofisi,ANAPATA udalali it means yaeezekana jamaa Ni meanasheria,land valuer etc
Ndiyo mkuu, mimi ni mtaalam wa mambo ya kasino, hivyo ninafanya udalali huo wa mambo yote ya kasino na kazi zinalipa kweli, pia kuna udalali mtu amepewa kazi aandike makala fulani anakwama ninakuwa ninazifanya, kazi zinatokea kuzidi za mishahara ila ni kwa misimu. SHukrani kwa kumfungua akili mdau huyo
 
Ukisevu mshahara wako wote kwa miezi sita bila kutumia kiasi chochote ni 1300000x6 =7,800,000 . Sasa hebu tueleze boss, hiyo 10m uliipataje kwa miezi 6 au wewe ni chuma ulete?
Hata mimi pia nilitaka kumuuliza swali kama hilo hilo. Anyways, hata kama anafanya deals zingine nje ya kazi lakini bado kuna maswali mengi yanahitaji majibu, vinginevyo hii inaweza kuwa chai tu kama chai zingine.
 
Uliza mkuu nikusaidie kujibu.
 
Umeeleweka vizuri sana Boss.

Kwa sasa malengo yako ni yapi Kapteni ili uwape motisha wengine?
Asante sana mkuu, kwa sasa nimekaa kwanza ninapunga upepo niisome ramani, sijapanga kikubwa sana zaidi ya kufanya finishing tu hapa nyumbani, nyumba bado sana haijaisha na tumehamia ikiwa na vumbi ndani, tunakomaa kuona namna gani finishing inaisha baada ya hapo ni mwendo wa biashara za nafaka na kupata mashine za kasino.
 
Kwa mara ya kwanza account yangu inasoma 10million sikuamini , ila kwa sasa kusave hiyo hela siwezi coz nahamini bora iwe kwenye mzunguko kuliko kukaa bank
Kusevu ni bora kuliko kuingia kwenye biashara ambazo hauna uzoefu nazo mkubwa
 
Back
Top Bottom