Nilivyosave Milioni 10 kwa miezi 6 na kujenga nyumba mbili na kununua gari zuri

mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
923
1,585
Wakuu salaam,

Nimeona kuna mada ya mambo ya kusevu nikaona nishee story yangu inaweza kuwa msaada kwa mtu fulani sehemu fulani..

1. Take home ilikuwa ni 1,300,000 baada ya makato yote kazini pamoja na benki wakati wa kutoa

2. Tulishusha maisha tukawa tunaishi nyumba ya kupanga ya chumba kimoja elfu 35000 kwa mwezi, jirani kabisa na kazini, ninatembea kwa miguu saa moja nimeshafika. Mwanzo tulikuwa ninakaa nyumba ya 900,000 kodi ya miezi sita bado na umeme juu.

3. Nikaacha kula bia na nyama kila siku, nikawa ninakunywa mbili mwisho wa wiki na nyama nusu

4. SIkupanga nyumba ya umeme, nilikopa sola ya Zola ule mtambo mdogo wa kulipia 10000 kwa mwezi

5. Bima, pampers na vyakula special vya mtoto (maana sometimes wanachagua sana vyakula wakiwa wadogo) nikaweka bajeti ya 150,000 hapo pamoja na bima yake

6. Ikitokea shida sikuwa ninakopa kwa benki, ninakopa kwa marafiki

7. Nikawa nina kazi za mishemishe na dili za hapa na pale ukijumlisha udeiwaka na udalali mida ya jioni na wikiendi na nje ya Ofisi

Nilipofanya hayo yote niliweza kusevu milioni 10 ndani ya miezi sita ya mwanzo na kuendelea, IKAWA NDIYO DESTURI YANGU kwa miaka kadhaa mbele, hapa ninavyoandika hivi sasa nina gari ya kifahari SUV na nina nyumba ya zaidi ya milioni 30 ninayoishi na familia yangu (bado haijaisha finishing) na mama yangu nimemjengea nyumba ya milioni saba huko Kijijini kwetu.

Nimejifunza: FANYA IBADA, punguza bajeti za kifamilia, kama umepanga kakae jirani na Ofisi, ongeza njia za kupata kipato, sevu, wekeza. Utafikia lengo.
 
Kama ndiyo maisha unayofurahia basi Hongera, na kila mmoja aishi maisha anayoyafurahia bila kuwapa wengine tabu au karaha, na ambao hawafurahii maisha yao basi waongeze bidii ipo siku Mungu atabariki juhudi zao nao wafurahi
Ndilo jambo la msingi, asante kwa kushea
Inabidi utupe shule mkuu, maana kusave 1.6m out 1.3m kwa mwezi sio mchezo ati!
Namba 7 pale mkuu
 
Ukisevu mshahara wako wote kwa miezi sita bila kutumia kiasi chochote ni 1300000x6 =7,800,000 . Sasa hebu tueleze boss, hiyo 10m uliipataje kwa miezi 6 au wewe ni chuma ulete?
Nimeelezea kwenye point namba 7 hapo, hela ya mshahara haijawahi kutumika, ni dili za nje ya kazi ndizo zilijazia pamoja na kugharamia kuishi kwneye chumba cha kupanga
 
Asante sana.

Hebu nisaidie na mimi namna ya kusevu nifike ulipo.

Mimi ni Hotelier, napokea 280000 kwa mwezi, hiyo ni take home baada a makato...nimepanga chumba cha umeme, kodi 40,000 kwa mwezi...Mke na Mtoto anayesoma st Kayumba darasa la nne.
Labda hapo ufikirie namna ya kumfungulia biashara ndogo shemeji (kama ni mama wa nyumbani)

Kwa take home hiyo ningekuwa mimi ningeweza kusevu 100000 kwa mwezi, punguza matumizi ya nyumbani kwa kununua vitu vya muhimu sana, bia na wanawake kwako iwe mwiko, kama unapata muda zaidi tafuta kazi za mtaani ndogo ndogo nje ya kazini kwako.

Kinachoniokoa mimi ni kazi za nje ya Ofisi ninazofanya zinaendesha familia huku mshahara ukikaa kwneye akiba.
 
Back
Top Bottom