Nilivyopigana Enzi za Ujana wangu

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,416
85,844
Waswahili husema "Ujana ni maji ya moto"! Enzi za ujana wangu na mie niliyaoga hayo maji ya moto haswaaa!

Siku moja wakati tunacheza mpira pale kiwanjani karibu na kwa Mzee Msangi, ghafla mpuuzi mmoja akanikanyaga, nadhani alikusudia, sina uhakika hata mimi.
Ikabidi tuweke mkono, I mean tupigane lakini kwakua Mshkaji alikua mtemi sana, nikaona isiwe tabu, kila nikifikiria majirani zangu walivyodundwa na huyu mshkaji nikaona nitaaibika!
" Nguvu sina, pesa Sina, vifaa sio kama maabara nazungumzia mawe, sina! Nikajisemea moyoni, yaani hata mkwara unishinde??" Hapana aiseee

Nikakusanya kila kilichochangu nikakimbilia mlimani pale Store Mombasa nilipozaliwa, nikiwa mbali nae sasa, nikaanza kushusha mkwata huku nimevua shati na nimetanua kifua kweli kweli! Ooghh kama kweli wewe kidume, njoo sasa, mshenzi wewe, dogo tu,kawatishe hao Wapuuzi wenzio huko sio mimi! Oyaaa wanangu, asiwatishe huyo mpuuzi mmoja tu hivi!

Lakini kila SAA nilikua naangalià kama mlango wa home uko wazi! Akatokea jamaa akapaza sauti "Kama kweli wewe kidume si uje huku uwanjani sasa?" Nikaendelea kupiga mkwara, hapa ndio kwetu msinitishe, nimezaliwa hapa na hata nikifa nitafia na kuzikwa hapa! Sijui hata jamaa walisemaje tena.

Subiri narudi kuendelea ngoja ninywe dawa kwanza
 
Noma sana mzee baba,nakushauri pia usiende kula mapapai ya pale kwa mzee Mfinanga inasemekana hayako salama sana.
Mbuzi je? Unashaurije? Nimeitiwa Mbuzi kwa Mzee Msuya pale!
 
Mbuzi je? Unashaurije? Nimeitiwa Mbuzi kwa Mzee Msuya pale!
Hio kua nayo makini kidogo,mcheki mtoto wa Mama Kitururu aitwae Mbaga, yeye ni bwn mifugo maarufu pale Chome anaweza akakueleza ugonjwa wa siku hizi unaosumbua sana mbuzi unaoitwa Unspecified.
 
Hio kua nayo makini kidogo,mcheki mtoto wa Mama Kitururu aitwae Mbaga, yeye ni bwn mifugo maarufu pale Chome anaweza akakueleza ugonjwa wa siku hizi unaosumbua sana mbuzi unaoitwa Unspecified.
Hahahaha hamna shida ngoja niende kwa Mrutu kwanza
 
Active Cookie Farida mbona mmehamisha thread yangu kutoka kwenye jukwaa la Siasa? Na nyie hamjasoma na kuelewa nilichoandika! Please hii ni siasa na ndio maana nilipost kwenye siasa! Naomba irudishwe kwenye siasa. Waelewa watakuja kuelewa nilichoandika!/
 
Bora umeandika kifupi ili uzi ukifutwa usiumie sana, hebu tuendelee haraka haraka kabla mods hawajaamka.

Enhee, kwahiyo ukatunisha kifua kama yule Musukuma.?
 
Back
Top Bottom