Nilivyoona Nyati na ukubwa wake anasumbuliwa na simba nilimzarau sana; Kumbe hata wanyama nao wanatushaanga sana vile Mbu na kirusi anavyotutesa

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Nyati au Kwa lugha nyingine Mbogo (Buffalo)

Ambao hamuelewi ni kwamba! Nyati ni mnyama mithili ya ng'ombe dume! Ni mkorofi sana ukiingia kwenye himaya yake! Ndiyo màna kuna msemo unasema " UMEGEUKA MBOGO"

Msemo huo ulitokana na utata Wa mnyama huyo!
Hivyo mtanange Wa Nyati hauzimwi na Simba mmoja!
Siku moja nilishuhudia mtanange Wa Nyati (Mbogo-Buffalo) na mnyama Simba;

Simba walimtaiti Nyati ipasavyo, pamoja na kwamba na yeye aliwafurusha Kwa pembe zake, lakini kadri muda ulivyozidi nguvu zake zilianza kumpungua kiasi cha kuonesha kuhitaji msaada; Nyati huyo alipelekeshana na Simba kibabe hadi wakatokea kwenye bwawa!

Yule nyati ponapona yake akaamua kuzama bwawani ili kuyanusuru maisha yake;
Simba wakiwa hoi ulimi nje, wakalala chini kando kumgojea!

NYATI akiwa ndani ya Maji, Punde aliibuka MAMBA Mkubwa akimsabahi Kwa meno kutaka kumla;

Sokomoko likaanza upya! Wakavutana na Mamba hadi akafanikiwa kuponyoka na kukimbilia nje (Nchi kavu ambako simba sana msubiria). Lakini kabla hajatoka alisimama kando ya bwawa hilo akiwaza abaki Ndani ya Maji au atoke!

Lakini mwisho aliamua kutoka kuwafuata SIMBA (Yamkini aliamini hao simba wamechoka na wanahesabika kuliko Vita ya MAJINI ambako haoni wala hajui kuna mamba wangapi)

Alipelekana nao wale Simba muda mrefu hadi pale kundi la nyati wengine walipofika kuamulia (Haijulikani walitokea wapi).

Na hiyo ndo ikawa ponapona yake yule NYATI!

PAMBANO HILO LINATOA TAFAKALI GANI
Wanyama Wa polini walinyimwa akili za kibinadamu, lakini pamoja na ujinga wao wanashinda misukosuko mikubwa sana!

HIVYO BASI! KUMBE VITA YA MMOJA MMOJA NI NGUMU SANA!; SIMBA WALIGUNDUA UDHAIFU WAO WAKAAMUA KUWINDA KWA KIKUNDI!

Laiti na nyati nao wangelitambua mapema kupambana wakiwa kikundi hakuna Simba angesogea!

TUNAJIFUNZA NINI HAPO

"
Ebu Fikilia maisha ya uwepo wa KORONA, shambani kuwepo NZIGE, wenzetu KONGO wana hadi EBOLA n.k Fikilia kutoboa bila maridhiano itawezekana?

VITA DHIDI YA KORONA NI TISHIO KWETU WANADAMU;
Nguvu ya kirusi cha korona ipo kwenye wingi wake! Mbinu kubwa ya kirusi ni kujizalisha Kwa Wingi ili atuangamize!

AKILI YA RAIS pekee haiwezi kutufanya tuushinde ugonjwa huu, AKILI YA UMMY pekee haiwezi, AKILI YA CCM pekee haiwezi;
Ugonjwa huu unapaswa kutupatanisha kama taifa moja! Mjadala Wa kitaifa ufanyike, Maoni ya Wapinzani yasipuuzwe!

ASIWEPO MTU HATA MMOJA ANAEJISIFU KWA CHAMA CHAKE! (Rais awe mfano kufanikisha hili ikibidi awe mkali zaidi kwa watu watakaoleta uvyama hata kama kawateua yeye)

LENGO Liwe ni moja tu kupambana na korona!
Yamkini Kebehi, Majungu ya wapinzani na Uvumi Wa watu kariba ya KIGOGO Ulizaliwa Kwa Kuwatenga!

Yamkini Vitisho vya kutumbuana Vimeondoa Ubunifu na uwajibikaji wataalam wetu !

Ni wasaa sasa wa kuweka tofauti zetu na kukaa nao Meza moja Tulijenge Taifa!

Na nyinyi wapinzani mkipewa nafasi Itumieni Msijitweze; Lengo liwe Moja kuiokoa nchi yetu!
Mjadala wa kitaifa ufanyike;
Kila idara ipewe siku tatu kuja na (presentation ya solution)

KORONA ITAKWISHA TUKIONGEA LUGHA MOJA

.....HERI YA PASAKA.....
 
Umetumia busara sana bahati mbaya utaambulia kebehi kutoka kwa upande wa CCM. Subiri utàamini. Wanajiona wako sahihi kila wakati...
 
Kwanza tukubaliane kuwa upendo, amani kuheshimiana ni muhimu kuliko madaraka,

pili tukubali kuwa kiongozi akishindwa awe tayari kumwachia mwingine Mwenye uwezo wa kuongoza bila kujali chama jinsia kabila au rangi.

Tatizo ni upande ule kwenye uchu wa madaraka kukubali kwa hiari kukaa na wapinzani wao.

Tumeshuhudia juzi wakati janga LA corona limeshika kasi watawala walikuwa bize kumpora umeya meya wa iringa
Bila sababu

Lakini hili janga huenda limekuja wakati muafaka ili kuleta usawa na kuondoa viburi vya watawala
Pia huenda hili janga likaleta mapinduzi ya kiuchumi kisiasa na kjamii tusiyoyatarajia nchini na duniani kwa ujumla
 
There must be a balance of nature. And the virus will balance it properly!

Kwani mlitaka nani afe labda! People must die to keep the earth balanced!

Watu milioni sitini wote mnataka kwenda wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini mnagombana?
Sijawahi kugombana na MTU nisiyemfahamu! Tuendelee na mada ya Nyati.
IMG-20200412-WA0105.jpg
 
Hii thread nimeipenda kwakuwa Kwanza umegusa maeneo yangu makuu ninayoyapenda:

-wanyama ndo hobby yangu.

-alafu umehusianisha incidences mbili tofauti ukazileta kwenye somo moja, huu ni ualimu uliotukuka, ambao ndiyo proffesion yangu.

Umesomeka sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom