Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

UMUGHAKA itabidi ujitafakari San mnk katika ule Uzi wa mzee makono ile ilifikia viewer 126000 +++ yaani waliosoma tu ,sas huu wa sasa HV umefika laki 132 kwa sas HV na Bado unaendelea sijui itafikia ngapi siju ilo ,ila ninachotaka kukumbia Ni kwamba jitafakari kuangalia namna ya kuzalisha vitabu upige pesa au movie kbsa tengenezaa mnk unajuwaa mnoo kusimulia na kuandika vzr sna
Watanzania wengi sio wasomaji wa vitabu, unaweza usirudishe hata hela ya kuchapisha
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 19.


Baada ya muda wa nusu saa yule Bosi alirudi akiwa na jamaa mmoja wa wale jamaa wawili tuliowakuta pale sebuleni kabla hawajaambiwa watupishe kwa ajili ya mazungumzo!.

Alimwambia yule jamaa "Kaa pale"

Bosi "Hawa ni watu wa kazi,ni wakurya wakwenu huko!"

Basi yule jamaa akaanza kutuongelesha lugha ya kikurya huku akituuliza maswali na sisi tukimjibu kwa ufasaha,sasa baada ya kujiridhisha ya kwamba tulikuwa wakurya,akamwambia Bosi kwamba ni kweli sisi ni Wakurya.

Bosi "Sawa naomba utupishe!"

Yule jamaa akanyanyuka akaondoka akatuacha pale sebuleni!.

Bosi "Kazi nitakayowapa itawatoa kwenye umasikini na hizi shida ndogo ndogo mtazisahau!"

Aliendelea "Pesa yetu ipo mikononi mwa watu hivyo inapaswa irudi kwetu!"

Bosi "Mimi nitawalinda wala msijali!"

Aliendelea "Kanuni huwa ni pasu kwa pasu kwa kitakachopatikana!"

Bosi "Endapo kikinuka jisalimishe au tetea uhai wako,Yeyote atakaye kuwa kikwazo huyo ni halali yako!"

Muda wote wa mazungumzo nilikuwa naona Mtatiro akitikisa kichwa kana kwamba yale maneno yalikuwa yakimuingia sana na yeye kuyakubali!.Mimi kiukweli niliingia uoga sana lakini nilikuwa tayari kumfuata Mtatiro atakachokiamua yeye!.

Bosi "Kufa na siri hapa si hiari ni lazima,fanya ufanyavyo usije ukathubutu kumtaja mtu endapo ukiwa mikononi mwa wendawazimu(Mapongo)"


Aliendelea "Kitakachopatikana narudia tena itakuwa pasu kwa pasu!"

Bosi "Sasa tutaondoka wote kuelekea Arusha,lakini kabla ya kwenda huko mtaondoka na jamaa kwanza mkatengenezwe ndipo tuondoke!"

Aliendelea "Nyinyi ni wanaume bhana,haya ni maisha tu,pesa ndiyo kila kitu na hivyo lazima zirudi mikononi mwetu!"

Bosi "Eric mwambie Doto Akupatie milioni mbili uniletee"

Eric ambaye muda wote alikuwa kimya akimsikiliza bosi wake,alinyanyuka akaelekea huko ndani ambako aliagizwa!.

Baada ya dakika 1 alirejea na bunda mbili ambayo kila moja ilikuwa na milioni moja!.

Bosi "Kamata hii"

Mimi nikapewa bunda moja na Mtatiro nae akakabidhiwa bunda lake!.

Bosi "Hizo ni pesa mtakazo tumia kutatua shida ndogo ndogo!"

Aliendelea "Nadhani utaratibu mwingine Eric atawaeleza,nendeni mjipange ili ikiwezekana kesho au kesho kutwa muondoke mkatengenezwe kabla ya kwenda Arusha"


Kiukweli ile pesa ilikuwa ni kama vile sumaku,maana baada ya kuipokea ile hela niliona kama nilichelewa kwenye utajiri!.Tulinyanyuka tukamuaga yule jamaa na taa ikazimwa sisi tukatoka nje!.Tulipofika nje tulitembea kuitafuta barabara ambapo ilitulazimu kutafuta Taksi ili tuondoke!.

Eric "Nyie ni wanangu ni lazima niwaambie ukweli,mara zote huu ni mchongo ambao nikiufanya,kule kwenye zile pesa bandia pia natafuta tu maisha lakini kiukweli maisha yako huku!"

Aliendelea "Siwezi kuwashikisha dili mbovu!"

Eric "Huyo mliyekuwa mnaongea nae ni Askari lakini mpelelezi!"

Aliendelea "Si mko tayari ndugu zangu tupambane huku?"

Mtatiro "Mi nilitaka kumwambia anikabidhi chuma niingie mzigoni hata muda huu,nishachoka kudharauliwa!"


Eric "Usiwe na haraka Mtatiro,nyie jiandaeni kesho kuna mahali mtapelekwa na jamaa ili mkitoka huko muwe kamili gado"

Sasa kwakuwa Mtatiro alilidhia ile kazi kwa moyo mweupe,kiukweli na mimi nilijikuta nakubali kwasababu nilikuwa namkubali sana jamaa yangu!.

Muhimu:-

(Yule tuliyeambiwa ni mpelelezi kiukweli hakuwa Askari wala mpelelezi,nilikuja kugundua baadae jamaa alikuwa ni mafia wa hatari na alikuwa akisakwa na jeshi la polisi sana,sasa nilichokuwa nikijipa moyo ni kwamba,kwakuwa alikuwa askari sikuhofia chochote maana nilijua endapo kikitokea cha kutokea tungesaidika,kumbe ile ilikuwa ni zuga tu wanaume tuingie mkenge,sitomtaja jina kwasababu maalumu na hata hivyo jamaa kwasasa ni marehemu).

Eric "Umughaka mbona kama huna amani mwanangu"

Mimi "Mimi niko fiti kaka"

Eric "Au unahofu?,mbele ya chuma hakunaga hofu kaka ile subiri uishike ndiyo utaniambia!"

Mimi "Kwahiyo chuma tunapewa lini?

Eric "Msiwe na haraka,chuma zipo tutazikuta Arusha!"

Aliendelea "Hamuwezi kupewa chuma mpaka mkatolewe uoga ndugu zangu!"

Mtatiro "Mimi si muoga kaka labda Umughaka"

Baada ya ile kauli ya Mtatiro tukajikuta wote tunacheka sana!,basi sisi tulifanikiwa kuondoka tukawa tumeagana na Eric na kukubaliana asubuhi tungeonana ili kuondoka tulikoambiwa tungeenda ili kutengenezwa kutolewa uoga!.

Tulipofika nyumbani kiukweli kila mtu alianza kuhesabu hela zake na kukuta ilikuwa milioni moja moja!.Mazungumzo yalichukua nafasi pale ndani na kiukweli Mtatiro alikuwa akiniambia sisi ni watoto wa kiume hatuna budi kupambana kwenye madili makubwa ya hela ili tufanikiwe katika maisha!.Ndugu yangu Mtatiro alikuwaga ni jasiri sana na asiyekuwa na chembe ya aibu na uoga!,alikuwaga akiamua kitu basi hakuna kurudi nyuma,ile roho ya ujasiri na isiyokuwa na uoga ndiyo Mtatiro aliniambukiza na mimi pia hata leo!.Mtatiro alikuwa ameamua liwalo na liwe,yeye alichokuwa akitaka ni pesa tu,hakutaka kusikia mambo mengine kabisa!.

Asubuhi kulipokucha Mtatiro alinishauri twende kwanza tukanunue nguo na viatu ili tuwe kila wakati tunapendeza!,sasa hakufahamu hayo ndiyo yalikuwaga mambo yangu,kiukweli nilifanya mambo yote hayo ili nipate pesa ya kula vizuri na kuvaa vizuri tu!.Baada ya lile zoezi la kununua viwalo,tukaianza safari ya kuelekea kitangiri ambapo yalikuwa makazi ya muda yule jamaa.

Tulipofika nje ya geti Mtatiro alimpigia simu Eric akawa amekuja kutufungulia geti na kuzama ndani!.Tulipofika hapo ndani hatukumkuta yule bosi wa Eric ila tulimkuta jamaa mmoja ambaye hakutaka tupoteze muda bali tuanze safari!.

Jamaa "Si mko Tayari!?"

Sisi " Ndiyo"

Jamaa "Ok tuondoke"

Tuliondoka kuelekea nje ambapo alianza kuwasiliana na mtu kwenye simu akimaambia asogee maeneo tuliyokuwepo ili tuondoke!.Baada ya muda mfupi gari aina ya Noah Ace ikawa imefika pale na aliyekuwa akiendesha alikuwa Demu!.Tulipanda kwenye ile gari sisi tukakaa katikati na yule jamaa akawa amekaa mbele!.Sasa tulimpa hai yule demu lakini hakutoa ushirikiano ikabidi tukaushe!.

Ndani ya ile gari hakuna mtu aliyezungumza na mwenzie zaidi ya mikausho mikali.

Eric ni nani tena, maana mwanzo naona aliyewapeleka ni Gabi kwenye huo mchongo?
 
UMUGHAKA itabidi ujitafakari San mnk katika ule Uzi wa mzee makono ile ilifikia viewer 126000 +++ yaani waliosoma tu ,sas huu wa sasa HV umefika laki 132 kwa sas HV na Bado unaendelea sijui itafikia ngapi siju ilo ,ila ninachotaka kukumbia Ni kwamba jitafakari kuangalia namna ya kuzalisha vitabu upige pesa au movie kbsa tengenezaa mnk unajuwaa mnoo kusimulia na kuandika vzr sna

Naomba unipe link ya huo wa mzee makono jamaa amenivutia kumsoma!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom