Nilivyomjua Dr JK Baada ya Hotuba kwa wazee wa Dar

Kumjadili mtu kwa kuwa alipata GPA ndogo nadhani ni aina ya ubaguzi na sio sahihi. Nadhani ni bora kuangalia anachokifanya ni sawa ama si sawa ndipo ujadili hilo. Naamini mtu mwenye GPA ndogo anaweza kufanya kazi nzuri kuliko mtu mwenye GPA kubwa. Kuna watu walikuwa na uwezo mdogo darasani lakini katika maisha nimewaona wakiishi maisha ya mafanikio makubwa (sio kifedha tu) kuliko waliiokuwa wanafaulu zaidi. Kuna mfano kwenye Biblia ya watu waliokuwa wavua samaki kulijua neno la MUNGU kuliko waliofuzu dini kwa kiwango sawa na PhD.
 
Kuna watu wadhaniao hii JF iko Tanzania tu na inasomwa na walio Bongo tu. Sisi tulio mbali kwa kweli tungependa kujadili masuala na siyo personality. Nigetaka kujua:
1-alisema nini juu ya tatitizo la umeme, mikataba, ukodishaji wa maeneo makubwa ya ardhi kwa wageni?
2-Juu ya katiba, Zanzibar, uonevu unaofanyiwa wapinzani, Tanzania kufilisika etc?
3- Angalau kudokeza serikali itayakabili vipi matatizo mawili matatu makubwa ya sasa?
Kama hakuzumgumza chochote juu ya hayo, ingekuwa vizuri mazungumzo yake kama yalikuwa ya faragha, bila kupeperushwa taifa zima, kwani naamini atakuwa amewatia watu wengi simanzi.
 
Ndugu zangu, Leo baada ya kupoteza muda wangu mwingi kumsikiliza Mh Dr JK nimepata kumfahamu zaidi na namna anavyoendesha nchi yetu.

1. Raisi wetu ana ''below average thinking capacity'' kama sitakosea masomo yake ya degree ya kwanza alipata GPA ya 2.0 hadi 2.5.

2. Dr JK anaongoza hii nchi kwa kutumia madesa na hii ni hatari sana maana hafikirii kufanya tofauti na kilichofanywa nyuma hata kama kuna haja ya kufanya hivyo.

Mwenye mengine unakaribishwa kushusha....

Nawakilisha

Hii ni hotuba ya wazee na siyo watanzania kama vijana.
 
Back
Top Bottom