mtanzania asiye jielewa
Senior Member
- Nov 13, 2016
- 179
- 98
Alikuwa mdada mzuri sana mwenye weusi wa kupendaza, mume wake alikuwa rafiki yangu sana , mbaya zaidi alikuwa ananipa siri za mke wake na kasoro za mke wake, (nisamehe rafiki yangu) sasa basi huyo mke wa rafiki yangu alibahatika kuzaa mtoto mmoja tu, alipobeba mimba alienda kuitoa, ndipo ikaelekea kutokuzaa tena, ikabidi huyo rafiki yangu amtafute demu mwingine na akampa mimba, sasa huyu demu wa nje tulijuana sana , basi huyu demu alinishauri nifanye kila njia ili yule mke halali atoke yeye aingie ndipo nikakubali na namba ya simu ya mke halali akanipatia yule demu maana alikuwa nayo, kumbuka mke halali wa rafiki yangu hanijui na hakuwahi kuniona, Ndipo nikaanza kumtongoza kwa njia sms na nikajifanya kuwa nitamtibia tatizo lake,............ moja kwa moja akaamini kuwa mimi ni dactari .............tukaaanza kuchat kwa sana nikamjengea chuki kwa mume wake (wanawake hawako makini) akaanza kunipenda bila hata kuniona wala kuisikia sauti yangu. .... akaanza kuwa na kiburi kwa mumewe...... na mume wake akawa ananiambia mabadiliko ya mke wake (hakujua mimi ndo sumu kwake) mwisho wa siku nilimuongopea kuwa nitamuoa tena nilimwambia mimi ni tajili sana (mke wa mtu akavimba kichwa) ...... mambo yakazidi kuharibika ndani ya nyumba ikabidi waachane. Wakati huo hajawahi kuniona ila nilikuwa nampa maelekezo. Ni kweli waliachana ikabidi rafiki yangu ayahamishie mapenzi kwa huyu demu..... kwa kuwa nilikuwa na kiu na yule mke wa jamaa nikapanga kujitambulisha kwake wakati huo alikuwa alisharudi kwao. .... simu hiyo nilienda na simu kama saba na zote zilikuwa zinapigwa kila mara napokea vya uongo naongea mamba ya mapesa mapesa tu, dah mke kaingia kingi nikamaliza mchezo kesho yake. Jamani kesho yake akapita kwenye mitaa yangu bila kutegemea na bila yeye kutegemea akanikuta nauza machungwa kilichotokea . Nitakijibu kwenye komenti