Nilivyolala na mke wa mtu baada ya kukutana safarini

Kipenseli

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
814
1,055
Siku nilivyolala na mke wa mtu kiutani utani tu. Mwezi uliopita nilikuwa nasafiri kutoka Iringa kuelekea Jijini Dar Es salaam, kwa usafiri wa basi moja maarufu (jina kapuni).

Niliiingia ndani ya basi na kwenda kuketi kwenye siti yangu, baada ya dakika kadhaa akaja Mwanadada mmoja mwenye urembo wa wastani, na umbo moja maridhawa, huku nikiwa nimemkazia macho, alifika pale nilipo huku akiangalia tiketi yake mkononi, baada ya kunisalimu akaketi pembeni yangu na kutulia tuli.

Baada ya mwendo fulani safarini tukajikuta tumetumbukia kwenye stori za hapa na pale, stori zilienda kwa muda na mara kila mmoja akaanza kusinzia kwa wakati wake, nilipokuja kushtuka baadae nikamkuta bi Dada ameuchapa usingizi na wala hajitambui, baadaye kidogo nami nilisinzia tena na kupotelea usingizini. kabla ya sote kushtuliwa na tangazo la Muhudumu wa Basi kwamba tunaingia hotelini kwa mapumziko ya dakika kumi pamoja na kupata chakula.

Baada ya msosi na kurudi kwenye basi mastori yalianza tena upya huku wote wawili tukiwa tumechangamka tofauti na pale awali, ndipo kwenye maongezi nilipogundua yeye ni mke wa Mtu mwenye Watoto wawili, na tena akanionyesha picha za wanafamilia wake alizokuwa nazo kwenye simu yake.

Ndipo la haula nilipogundua kuwa muda wote wa safari nilikuwa nimelala na Mke wa Mtu. Hakika tulifurahiana sana kwenye safari ile, huku stori zikinoga kadri tulipokuwa tunakaribia eneo la ubungo ambako ndio kituoni na mwisho wa safari yetu, tuliagana kwa bashasha huku tukitakiana kila la kheri kule tuendako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom