Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nyie ndio mmekuja kuharb Uzi anzisha Uzi wako wa matako makubwa ndege mnaofanana mtapaa pamoja watu tunajifunza maisha ya South ili tujue tutaingie huko ww unakuja kutangaz ujinga
Unataka kuingia South kaka.
Simple tu.
Olewa na mwanaume mwenzako utapata visa ya kuingilia kule mtaa umetulea
Unajua South wamehalalisha ndoa za jinsia moja mkuu...olewa, utapata kuingia kule, tumia utupu wako wa nyuma kwa faida mkuu, maana mbele kuna bamia na nyanya chungu tu ambazo hutaweza kuzitumia.
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU

Basi nilikaa pale Kanisani mpaka Asubuhi, wakati najiandaa kuondoka nikakutana tena na Yule Dada. Nakumbuka aliniuliza naishi wapi, nikamwambia Pretoria. Akasema mbona unaishi mbali sana, Gari za Kanisa lao halina rut za huko. Akaniambia kama sitojali, Kanisa kuna nyumba limewapangishia waumini wake wale ambao wanajitolea Kanisani. Akasema ataongea na Jamaa mmoja anaishi room peke yake, kama huyo jamaa atakubali basi atanipigia simu kuniambia.

Ukweli Yule Dada alionesha kunichangamkia sana. Basi nikaondoka zangu pale mpaka Pretoria kwa washkaji zangu wa Kibongo. Ukweli kama nilivyosema mwanzo, Mbongo yeyote ukianza kufanya harakati zako tofauti na wenzio wanaanza kukusema sema. Hili natoa kama angalizo kwa mtu ambae hajawai kufika South, lakini inabidi uwe na moyo mgumu kuweza kufuata ndoto zako.

Basi nikafika mpaka kwa Jamaa Y, akaniuliza kuhusu habari za Kanisani nikamjibu kwa ufupi tu kuwa ni safi tu. Sikutaka kumwambia kila kitu kilichoendelea kule kwa sababu ningewapa mada ya kunijadili zaidi. Kichwani niliwaza endapo Yule demu atanicheki kuniambia kuwa amepata chumba kule Midrand basi hawa jamaa nitawadanganya kuwa kule Midrand nilikutana na HomeBoy wangu Kabisa wa Mtaa mmoja hapa Temeke. Homeboy amesema nikaishi nae. Nilipanga kuwadanganya hivyo ili wasijue chochote kuhusu mpango wangu.

Basi siku zikaenda, kama kawaida asubuhi tunaenda kusimama kule Barabarani na Jamaa Y. Tayari nilishafikia hatua ya kupewa Kazi mbili tatu za kuwapelekea jamaa Fulani madawa, nilikuwa nafanya hivyo, lakini moyoni sikuwa comfortable, Nilikuwa najiuliza, ina maana mimi South nimekuja kuuza Madawa? Najisemea Hapana. Hapa lazima niendelee kutafuta Mchongo wa Halali. Jamaa Y alikuwa akikutuma kumkatalia unashindwa, kumbuka unaishi kwenye chumba ambacho yeye ndo analipia Kodi. Muda mwingi unakula chakula chake. Kwa hiyo akikutuma huwezi kumkatalia. Basi nikawa napiga michongo hiyo hapo ya hapa na pale, Siku nikipata nafasi ndo nilikuwa naenda kule Midrand Kanisani. Wale Vijana ambao Jamaa Y amewaleta South yan utawaonea huruma, wanapiga Kazi kama punda. Wao wanainjoi tu kuishi Ghorofani, Kuvaa vizuri na kula KFC.

Mpaka siku ambayo Yule demu wa Kanisani alinicheki kwa simu na kuniambia Jamaa amekubali nikaishi nae. Nilifurahi sana. Jamaa zangu ziliwadanganya kama nilivyopanga. Jamaa Y alikubali niondoke lakini sura yake ilionesha kutokupendezwa na mimi kuaondoka pale. Alikuwa ananiambia maneno Fulani hivi ya kunitaka niwe makini. Alisema majamaa wengine sio wazuri sana kuishi nao. Nikamwambia mimi naenda lakini nitakuwa narudi hapa mara kwa mara. Jamaa alikubali kishingo upande. Hata sikuchelewa zangu nikawaaga jamaa, nikabeba begi langu nikasepa.

Kwa kifupi nilikuja kujua kwamba Yule demu wa Kanisa anaitwa KANYA, Alikuwa ni mmoja wa waimba kwaya muhimu pale Kanisani. Waimbaji wote walikuwa wanaishi kwenye nyumba nzima ambayo walipangishiwa na Kanisa. Alivyonicheki aliniambia tukutane sehemu mmoja inaitwa KALFONTEEN, Sio mbali sana na Midrand. Aisee nakumbuka ile siku hadi kufika huko KALFONTEEN nilipotea sana. Yan kilichotokea ni kwamba mfano wewe hapa Dar unaishi Tegeta halafu mtu akwambie njoo tukutane Makumbusho, Halafu wewe upande daladala mpaka Kariakoo, ukifika Kariakoo ndo utafute Daladala za Makumbusho uende zako Makumbusho. Wenzetu miji yao mikubwa, barabara nyingi mpaka mtu unachanganyikiwa.

Hatimae nilifika mpaka aliponiambia Kanya tukutane, hapo nina begi langu Mgongoni. Hao mdogo mdogo kwa mwendo wa miguu akanipeleka kwa huyo jamaa ni raia wa Ghana anaitwa Thomas. Maisha yangu mapya yalianzia hapo Kalfonteen. Yan kwenye Chumba tulipokuwa tunaishi na Thomas na kule Wanapoishi Wadada waimbaji sio mbali sana. Tuliishi kwenye Chumba Kimoja kikubwa, Jiko na Choo. Hakukuwa na Sebure. Thomas alikuwa na visa vingi sana, kwa sababu kabla ya mimi kufika pale yeye na rafiki zake wengine wa Kanisani ndo walikuwa wana date na wale wadada waimba kwaya, nilivyofika mimi kibao kikageuka. Basi pale maisha yangu na Thomas yakawa magumu mno mpaka nikawachukia Waghana wote. Mpaka Nikatamani kurudi Pretoria kwa Jamaa Y.

Sehemu inayofuata nitaelezea maisha yangu na Thomas yalivyokuwa, Mapenzi yangu na Kanya yalivyoanza na Harakati zangu za kuanza kutafuta mchongo wa Halali.
Umecholopoka kwa wajanja waliokuweka mtegoni!
Naona unatembea kwenye njia za kijanja.
 
L

Haaah haaah!!!mwana acha hizo,wewe mwenyewe kwenye story yako ya KHUMBU kuna mambo kibao yalikuwa yanaleta utata kwa watu wanaoijua South vizuri ila tulitulizana tu mpaka mwisho,sasa muache jita amalize story yake naye!!!
Stori ya Khumbu hakuna hata kipande kimoja chenye utata, sana sana kuna mambo mengi sana sikuyaongelea maana ningeyaongelea yote nadhani mpaka sasa stori ingekuwa inaendelea. By the way nimemuomba Keagan Paul nitoe tu kicoment changu na wala sikuwa na nia mbaya mkuu.
 
Tatizo lilikuja kutokea siku moja kwenye Birthday Party ya Mchungaji wetu ilifanyika usiku nyumbani kwake. Tulifika waumini kama wote.Kulikuwa na Nyama choma kama zote. Sasa yule demu mrembo mwenye ndinga lake nae alikuwepo. Nikasema leo lazima nitumie nafasi vizuri. Party ilifanyika nje halafu kulikuwa na kigiza giza fulani hivi, Nikasema Leo natumia hii nafasi vzr, Nikawa napiga piga nae story pale, mara tunapiga piga picha pale, sikufanya makosa hadi tukabadilishana namba. Kosa nililolifanya ni kwamba baada ya kutoka pale zile Picha nakumbuka nilipost Facebook. Halafu Kanya sijawai hata siku moja kumpost. Ugomvi kati yangu na Kanya ulikuwa mzito. Ishu ya namna hii kwa Wanawake ni kubwa sana.

poor reasoning
poor reasoning yake iko wapi
 
Konda Msafi

Naomba niwe upand wa Mtoto wa mstaafu kwa hoja mbili

1. Mkuu kusema kuwa mademu wa hadhi fulani unawajua hiyo statement iko too general na kwa namna moja ama nyingine haina uhalisia..ni kama vile sisi wabongo tunapowazungumzia wakenya utasikia tunasema 'wakenya wenzetu wako active sana kwenye kazi kuliko sisi tuna uvivu mwingi', at same time wakenya nao watakuwa wanatuzungumzia kuwa sisi watz tuko so active sana kwenye kazi kuliko wao...hizo ni general statements ila kiukweli kuna wavivu ndani ya nchi zote mbili.

2. Kiufupi tu mi naona story teller yupo sahihi..inabidi tuelewe story kama ilivyoletwa na tukitaka kupitia neno hadi neno tutakua tunakosea.. So mkuu konda msafi hizo statement zako ni too general na haziapply kwa wote. Pengine wabongo uliowaona ndio walikuwa wanakula bata ila walioonwa na Keagan Paul wenyewe wanafanya kazi kama punda. Hakuna kati yenu aliyewaona wabongo wote, au aliyewaona wahamiaji haramu wote wanaoishi south au aliyeishi na warembo wote..so statement uliyotoa bwana Konda ni sahihi kwa watu uliowaona ila haiapply kwa wote.

Ni kama vile weweau mtoto wa mstaafu mnavyotuambia mademu wa south ni wazuri kinoma ila kiuhalisia hiyo ni general statement na sio uhalisia kwa wote. mmeitoa hiyo statement kwa kufanya reference kwa watu wachache mliowaona ila kiuhalisia mademu wengine na wengi tu ni wakawaida kama hao tunaowaona kila siku kwenye isdingo, kipindi cha kombe la dunia na kwenye taarifa ya habari.

kiufupi tuielewe story kama ilivyoletwa tusije na generalized arguments ambazo hazijawa proven.
Sawa mkuu, nimekupata. Sitii neno tena.
 
Stori ya Khumbu hakuna hata kipande kimoja chenye utata, sana sana kuna mambo mengi sana sikuyaongelea maana ningeyaongelea yote nadhani mpaka sasa stori ingekuwa inaendelea. By the way nimemuomba Keagan Paul nitoe tu kicoment changu na wala sikuwa na nia mbaya mkuu.

Haina noma mkuu,acha story niendelee mengine we potezea tu!!
 
Nimekaa huko ila kuna vitu kama sembe naona hakuwa na dili nazo,wauza sembe wanapesa sana na ndo dili kubwa unaweza kutoboa.mwakani nitarudi maana maisha ya kule rahaa sana
Kwa sasa maisha yamebadilika ndugu.. siku hizi sembe hata wazawa wanauza. Ukisikia watu wanapiga wageni kwa kisingizio kuwa wageni wanaharibu watoto/ndugu zao ujue hiyo sio kweli. Lengo lao kuu ni kuona wageni wanaondoka au wanaziacha hizo biashara afu wanabaki wanauziana wenyew
 
Back
Top Bottom