Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Mkuu umeongea ukweli sana , uoga unajenga hofu sana, na hofu isiyo na msingi inakwamisha ndoto nyingi...

the fear of uncertainty

Hahahah ila hapo kwenye kula pitiku na ugali umenikumbusha songea sehemu moja inaitwa Ruhuwiko ....

Baada ya kushinda njaa siku nzima na kulala na njaa, usiku ulikuwa mrefu lakini nilivumilia hadi kukapambazuka....

asubuhi wakati tunajiandaa kwenda shule kuna msichana alikuwa mwanafunzi mwenzetu alikuwa anapasha kiporo cha ugali na hiyo mboga ya pitiku ili apate kifungua kinywa ..

Na me nikaomba nile maana niliamka na njaa sana,

Kufika darasani kipindi cha kwanza kikaisha , kuingia cha pili , tumbo liliniuma sana, nilihisi kutapika na kuharisha kwa wakati mmoja .

kwenda kujisaidia hakuna kitu kinatoka nikarudi class ...kuendelea kusikiliza kipindi.

Nikaenda kuomba ruhusa nikakatiliwa .

Wakati narudi class kukaaa kidogo kama dk 10
Hali yakutapika ilizidi hadi kunyanyuka mbio kwenda kutapika nje ya darassa lakin sikufika nilitapikia njiani karibu na ubao huku mwalimu wa chemistry akiwa anaendelea na pindi.

Dah mwailmu alishtuka na kutaka kuikimbia nje... maaana alikuwa anaandika ubaoni so wakati anageuka ndio nakutana na mimi natoka mbio kwenye desk kueleka nje, alihisi kama naenda kumvamia hivi. Wanafunzi walicheka sana wengine walicheka zaidi walipoona mzee nimetapika igali na pitiku yani ule mchanganyiko nilioula asubuhi nimeutoa kama ulivyo.

Kuna siku baada ya njaa ya siku nzima nakukosa uhakika wa kula tena usiku hata asubuhi ili tubidi tuanze kutembea kwenye mashamba ya watu na kula mahindi mabichi kama manyani au sokwe ..tukabamia kwenye shamba lilovunwa mihogo... dah

nilikaa kwa muda kama wa miezi mitatu kwangu ilikuwa kama mwaka mzima sitasahu tabu tulizopitia kule na wenzangu...

Ama kweli kusafiri na kuishi ugenini kunafungua akili
Hahahaha umenifurahisha sana. Unajifunza mambo mengi sana
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Basi nikaanza maisha yangu mapya ndani ya south pale Kalfonteen. Ratiba ya kwenda Kanisani ilikuwa ni karibia kila siku. Uzuri wao muda wa kwenda Kanisani ni Jioni kuanzia saa kumi na mbili na kutoka saa nne usiku. Mpaka Jumapili muda ni huo huo. Gari ilikuwa inatufata mpaka getini, tunaingia hao kanisani. Kwenye gari mnakuwa wengi. Nilikuwa nikifika Kanisani najichanganya sana na Vijana wenzangu, wazee, watoto mpaka Mchungaji nilianza kumzoea. Kwenye maisha ukiamua kujilipua, jilipue mazima, usijilipue nusu nusu, lazima uwe na uwezo mkubwa wa kujitoa ufahamu. Mimi sikuwa mwoga kama Wabongo wengi. Hata hapa Bongo nilikuwa sio mtu wa kwenda sana Kanisani, lakini kule ilikuwa kila siku nipo. Tena vile usafiri wa kwenda na kurudi bure, nyumba Bure, Basi kila siku nilihudhuria Ibada.

Kiongozi wetu kwenye upande wa Camera alikuwa anaitwa Max. Nilimfanya Max kuwa rafiki. Ndani ya muda mfupi nilihakikisha watu wengi wananizoea. Kanisa lilikuwa na siku za Michezo, ilikuwa ikifika siku hiyo naingia uwanjani kucheza mpira wa miguu. Nilikuwa najitahidi kucheza kweli kweli. Uwanja mzima nakimbiakimbia tu. Macho yangu yote yalikuwa kwa washua. Nikaanza kujipendekeza kwa watoto wao. Kupitia Kanya niliwazoea watu wengi pale Kanisani mpaka watu wakaanza kuhisi na date na Kanya hata kabla sijaanza hizo harakati.

Kanya alikuwa anapenda sana kupiga story na mimi. Ukweli hapa ndo kidogo nilianza kuinjoi maisha ya South Africa. Nilikuwa nakaa na watu ambao hata nikitembea nao barabarani nina amani.

Nilichokuwa nafanya muda wa mchana ambao nakuwa free, Kwa kutumia ile Akiba yangu nilikuwa natoka mwenyewe nakwenda mpaka Johanesburg kutembea tembea, Nilikuwa nashuka pale MTN Taxi Rank huyo naingia Mitaani. Nilikuwa nasambaza Barua zangu za Maombi ya Kazi. Niliomba kila aina ya Kazi ilmradi tu iwe ya halali. Nakumbuka niliendaga mpaka sehemu inaitwa Auckland Park, Sehemu ambayo kuna Media mbalimbali kubwa kama SABC, BBC na Media 24. Kwa kuwa nilikuwa najua kidogo mambo ya Camera, kote huko niliacha Barua zangu. Pale BBC nilikutana na Jamaa wa BBC Swahili, Nilikutana na Mzee Anaitwa Omary Muktadha. Hapa nitarudi kufafanua zaidi huko mbele. Kwa hiyo nikawa nafasi hivyo kila nikiwa free nakwenda maeneo mbalimbali, nilikuwa siogopi, nakwenda kwenye maviwanda huko.

Nirudi kwa Thomas, Thomas alikuwa ni mpiga Kinanda pale Kanisani, alikuwa hajui kama Kanya aliniambia kila kitu kuhusu Chumba tulichokuwa tunakaa kama kinalipiwa Kodi na Kanisa. Nashangaa siku moja nimeamka zangu Thomas ananiomba hela ya Kodi. Nikamwambia mbona nimeambiwa hapa Kodi inalipwa na Kanisa, alivyojua najua kila kitu, akaanza kuwa ananuna nuna bila sababu. Kwa kifupi Thomas alitaka kunipiga hela Kupitia hicho chumba, Chakula tu ndo mtu ulikuwa unajitegemea.

Nilikuwa natumia Akiba yangu nanunua chakula cha kutosha naweka ndani nakuwa najipikia tu. Thomas alikuwa hanunui chakula. Yeye alikuwa akirudi akikuta chakula anakula tu. Tena wakati mwengine alikuwa anakuja kula na rafiki zake. Wakiwa na hela hao walikuwa wanaenda kula KFC, Hakikosa hela anarudi nyumbani kula. Mimi nanunua chakula kwa bajeti zangu. Nilikuwa navumilia ivo ivo tu siku ziende nitimize malengo yangu.

Mara nyingi Kanya alikuwa anakuja pale ghetto, ananisaidia kupika, kufua na kufanya mambo mengine. Kanya alikuwa mzuri na halafu alikuwa na Bonge la Tako.Yan bonge la Shape. Ila mimi ni kama vile nilikuwa namkwepa kwepa kwa sababu mle Kanisani kuna demu nilishamuona, huyo demu huwa anakuja na gari yake, halafu anaonekana kama matawi fulani hivi. Nilikuwa namkwepa Kanya ili asije kuniaribia kumpata huyo mtoto, Kanya alikuwa anaishi kama mimi tu kwenye nyumba inayolipiwa Kodi na Kanisa. Niliona nikianzisha nae mahusiano atakuwa mzigo kwangu, wakati mimi nilipanga kuwa mzigo kwa mtu mwengine.
umarioo MDA mwngne unalipa....
 
Nimeishi nao...nimefanya nao kazi ...kuna wanaija walikamatwa mkoa X Wakaswekwa lupango... Waliokuwa kumi na 6 ...mshkaji wangu (mnaija mwenzao) yeye yupo njema kifedha ...katika hai kumi na 6 sita pekee ndo aliokuwa anawafahamu Ila alipambana mpaka wote wakarudishwa makwao...
Kila siku anawapelekea msosi.. asubuhi mchana jioni..
Anaenda mahakamani...
Lastly Igbos wote walijiunga kuhakikisha majamaa wanarudishw kwao.
Wana umoja Sana..
nakubali mkuu umoja walio nao wale sisi bado kutokana na uchache wa waliopo either hapa au kule nje kwa kujilipua

kuna mahali nilienda tu trip wapo watanzania wenzetu hawapendi kujulikana kama wao ni watanzania kabisa yani unashangaa sana

mahali hapo marafiki nilionao 50 kwa hesabu ya haraka 30 west africa 10/12 kenyans na 9/10 waganda
 
Na washarika Tuungane nae Kwa pamoja tuseme ee myaazi Mungu Utusaidie...

Much:Bwana awabariki na kuwalinda.
Awaaangazie Nuru ya uso wake apate kuwafadhili.

Mch: Bwana akae nanyi.
Ush:Akae na roho yako.
Mch:Tummhimidi bwana.
USH:Tumshukuru Mungu....

Mch:Tukienda kulipia matoleo yetu kule telegram Usharika Tuimbe wimbo namba 205 Beti 5..

Baada ya hapo dada Noelia atatuongoza pambio wakati tunamsubir Keagan Paul Aje atupe Uzi wa leo.
Usiniimbishe bure tu nikakausha mate, nipe uelekeo Kwanza uko wapi? Ulishawahi kujilipua? Kama bado je hujawaza maana nahisi we Ni kidume, sie ke wengi tunabebwa na maumbile yetu
 
Back
Top Bottom