Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Mlezi wa wana

Member
Apr 13, 2021
43
150
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Basi nikaanza maisha yangu mapya ndani ya south pale Kalfonteen. Ratiba ya kwenda Kanisani ilikuwa ni karibia kila siku. Uzuri wao muda wa kwenda Kanisani ni Jioni kuanzia saa kumi na mbili na kutoka saa nne usiku. Mpaka Jumapili muda ni huo huo. Gari ilikuwa inatufata mpaka getini, tunaingia hao kanisani. Kwenye gari mnakuwa wengi. Nilikuwa nikifika Kanisani najichanganya sana na Vijana wenzangu, wazee, watoto mpaka Mchungaji nilianza kumzoea. Kwenye maisha ukiamua kujilipua, jilipue mazima, usijilipue nusu nusu, lazima uwe na uwezo mkubwa wa kujitoa ufahamu. Mimi sikuwa mwoga kama Wabongo wengi. Hata hapa Bongo nilikuwa sio mtu wa kwenda sana Kanisani, lakini kule ilikuwa kila siku nipo. Tena vile usafiri wa kwenda na kurudi bure, nyumba Bure, Basi kila siku nilihudhuria Ibada.

Kiongozi wetu kwenye upande wa Camera alikuwa anaitwa Max. Nilimfanya Max kuwa rafiki. Ndani ya muda mfupi nilihakikisha watu wengi wananizoea. Kanisa lilikuwa na siku za Michezo, ilikuwa ikifika siku hiyo naingia uwanjani kucheza mpira wa miguu. Nilikuwa najitahidi kucheza kweli kweli. Uwanja mzima nakimbiakimbia tu. Macho yangu yote yalikuwa kwa washua. Nikaanza kujipendekeza kwa watoto wao. Kupitia Kanya niliwazoea watu wengi pale Kanisani mpaka watu wakaanza kuhisi na date na Kanya hata kabla sijaanza hizo harakati.

Kanya alikuwa anapenda sana kupiga story na mimi. Ukweli hapa ndo kidogo nilianza kuinjoi maisha ya South Africa. Nilikuwa nakaa na watu ambao hata nikitembea nao barabarani nina amani.

Nilichokuwa nafanya muda wa mchana ambao nakuwa free, Kwa kutumia ile Akiba yangu nilikuwa natoka mwenyewe nakwenda mpaka Johanesburg kutembea tembea, Nilikuwa nashuka pale MTN Taxi Rank huyo naingia Mitaani. Nilikuwa nasambaza Barua zangu za Maombi ya Kazi. Niliomba kila aina ya Kazi ilmradi tu iwe ya halali. Nakumbuka niliendaga mpaka sehemu inaitwa Auckland Park, Sehemu ambayo kuna Media mbalimbali kubwa kama SABC, BBC na Media 24. Kwa kuwa nilikuwa najua kidogo mambo ya Camera, kote huko niliacha Barua zangu. Pale BBC nilikutana na Jamaa wa BBC Swahili, Nilikutana na Mzee Anaitwa Omary Muktadha. Hapa nitarudi kufafanua zaidi huko mbele. Kwa hiyo nikawa nafanya hivyo kila nikiwa free nakwenda maeneo mbalimbali, nilikuwa siogopi, nakwenda kwenye maviwanda huko.

Nirudi kwa Thomas, Thomas alikuwa ni mpiga Kinanda pale Kanisani, alikuwa hajui kama Kanya aliniambia kila kitu kuhusu Chumba tulichokuwa tunakaa kama kinalipiwa Kodi na Kanisa. Nashangaa siku moja nimeamka zangu Thomas ananiomba hela ya Kodi. Nikamwambia mbona nimeambiwa hapa Kodi inalipwa na Kanisa, alivyojua najua kila kitu, akaanza kuwa ananuna nuna bila sababu. Hakuna tabu kama kuishi na mtu ambae asubuhi anaamka amenuna bila sababu. Mtapiga story pale atakapojisikia yeye kuongea. Alikuwa Mjinga kweli yule jamaa. Kwa kifupi Thomas alitaka kunipiga hela Kupitia hicho chumba, Chakula tu ndo mtu ulikuwa unajitegemea.

Nilikuwa natumia Akiba yangu nanunua chakula cha kutosha naweka ndani nakuwa najipikia tu. South Africa chakula bei rahisi. Kule gharama kubwa ipo kwenye Kodi za Nyumba na Nauli kwenye vyombo vya Usafiri. Kule Umbali wa Makumbusho mpaka Posta, Kwa Taxi zao, Kule ukisema Taxi ndio Daladala, unaweza kulipia hata Elfu 2 mpaka 3 za Kitanzania. Hiyo ni nauli ya kwenda tu.

Sasa Thomas alikuwa hanunui chakula. Yeye alikuwa akirudi akikuta chakula anakula tu. Tena wakati mwengine alikuwa anakuja kula na rafiki zake. Wakiwa na hela hao walikuwa wanaenda kula KFC, Hakikosa hela anarudi kula nyumbani. Mimi nanunua chakula kwa bajeti zangu. Nilikuwa navumilia ivo ivo tu siku ziende nitimize malengo yangu.

Mara nyingi Kanya alikuwa anakuja pale ghetto, ananisaidia kupika, kufua na kufanya mambo mengine. Kanya alikuwa mzuri na halafu alikuwa na Bonge la Tako.Yan bonge la Shape. Ila mimi ni kama vile nilikuwa namkwepa kwepa kwa sababu mle Kanisani kuna demu nilishamuona, huyo demu huwa anakuja na gari yake, halafu anaonekana kama matawi fulani hivi. Nilikuwa namkwepa Kanya ili asije kuniaribia kumpata huyo mtoto, Kanya alikuwa anaishi kama mimi tu kwenye nyumba inayolipiwa Kodi na Kanisa. Niliona nikianzisha nae mahusiano atakuwa mzigo kwangu, wakati mimi nilipanga kuwa mzigo kwa mtu mwengine.
Lakini Kanya aliniganda kinyama.

Hata Mimi majina ya kina Thomas nilip wahi kukutana nao ni watu kama huyo jamaa wana tabia za kujisikia na kususa susa
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
4,556
2,000
Unataka kunambia kuna wanaijeria wengi hapa bongo? Makazi yao hasa ni wapi? Na wanajishughulisha na nini wengi wao?
Wengi sana mkuu sema mishe zako hazikukutanishi nao labda. Mbezi,Tegeta wamejaa kuanzia wenye makanisa,wauza magari,wauzaji wa bidhaa za China,wauza kompyuta,wataalam wa IT,matapeli na wezi wa kwenye ATM mpaka wauza ngada

Kuna chimbo siku moja nilishangaa kukutana na jamii ya waHungary zaidi ya 100 wote wafanya biashara Dsm
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
4,556
2,000
Kuna wakati kujilipua kusiwe kama fasheni kwasababu unaona watu wanajilipua, hapana jitahidi uwe na sababu hasa ya kujilipua..

Jitahidi unapotaka kujilipua uwe tayari umepambana vya kutosha humu humu imeshindikana na njia pekee ni kujaribu kwingine, kuna wimbi la vijana wako nje kwa sababu ni sifa kwake kuwa nje na hakuna juhudi alizojaribu kufanya akiwa hapa na hata huko aliko hana anachokifanya zaidi ya kuishi normal life ambayo hata hapa si ajabu ungeweka nguvu kidogo ungefanikiwa..

Kwenye kusafiri kuna namna nyingi, wapo wanaosafiri kwenda kutembea, wapo wanaosafiri kwa kutumia ramani zilizoanzia hapa na kwenda kupiga michongo mbele na kurudi hapa, wapo wanaosafiri baada ya kushindwa kabisa kutoboa hapa...
Ukijilipua kwa ajili ya fasheni utaumbuka tu

Ila mtu ambaye kashapigika hakuna pa kutoboa ndani ya bongo ni bora tu kujilipua ukafie mbele
 

Madame B

Verified Member
Apr 9, 2012
28,473
2,000
una msambwanda lakini ?
Ebu fanya kama unaanza kuandaa sahv ili ukiiachia isiwe na episode zakutuchosha kusubir
Wanaume wa humu mna nini lakini?
Si tumekubaliana kuwa akimaliza yake nami nampa yangu aiweke humu?
Mna haraka kama bao la kwanza.
Tulieni wakaka...au mnataka kula kwa macho!!
Au ngoja niwaletee Pm yenu slip way na Patra31 ......
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,087
2,000
Wabongo hamuelewek aliyekua anajenga barabara mlimpiga Vita eti diktera Leo hii mnaanza kudemka mnasema Tena barabara
Acha kuchangia upuuzi hapa,awamu unayosema imejenga vipande vya barabara sio barabara,sasa unataka tulinganishe barabara ya Dar to Moro au dodoma au mwanza na Lusaka to Livingstone?tembea ujifunze na kuona kuliko kuhadithiwa mkuu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom