Nilivyokoswa kuuawa, kaka yangu akamuua Bibi mchawi aliyemuua kaka yetu na kutoroka

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
ilikuwa miaka ya late 1980s mpaka middle 1990s mwishoni ndo tunakua kua hivi tunaishi sehemu mmoja inaitwa sinde mkoani mbeya. ilukuwa ni chini juu kulikuwa ni isanga. sisi huku chini sinde. ilikuwa miaka ambayo ungeweza kudhani askari walikuwa likizo maana maisha yalikuwa ya kibabe sana.undava undava. kila sehemu ni ubabe. miaka hiyo kuna wababe mbeya kama akina daudi,shetani n.k watoto wa mama ilikuwa ngumu kuishi maeneo yetu. labda wakaishi uzunguni huko,forest n.k

pilika pilika nyingi zilianzia kwenye mechi za mpira wa miguu. ukisikia leo mnacheza na team ya kutoka nonde au majengo mjue hiyo mechi haitaisha mkaondoka kwa amani. tulikuwa tunajiandaa hasa. kama ni manati,mapanga,visu,magongo n.k kuna jamaa yangu mmoja namkumbuka sana alikuwa anaitwa ezekia huyu alikuwa mbabe jamaa mmoja huwa namfananisha na mayuku wa kwnye gazeti la sani. alikuwa mfupi mweusi ana mikono mikubwa halafu mirefu utadhani sokwe.alikuwa amejaa sana na makovu mengi sana.

ezekia sauti yake ilikuwa muda wote inakoroma maana alikuwa anavuta sana bhangi.saaaana. alikuwa akipenda kuvaa buti zake kama za jeshi kuuubwa mbele zimeinuka hivi halaf na suruali ya kubana. ile buti ilikuwa ndefu pia kuja juu na humo ndani anaficha kisu. kwenye jeans yake tight pia anaweka visu hata viwili halafu anavaa shati refu kufunika juu.

alikuwa anasoma sangu kidato cha pili.akiamua shule anaenda akiamua haendi.ukiingia geto kwake kuna mapicha picha kibao ya watu mbali mbali akina tupac,b.i.g n.k alilipenda maisha ya kigangway.

siku hiyo tulikuwa tumeenda uwanja wa sokoine kuangalia mechi kati ya simba na mecco kama sikosei. nilitoroka home nikajichanganya na kundi letu wana sinde tunaelekea uwanjani ilikuwa ni options mbili.kuruka ukuta au kupita kwenye ile mifereji ya maji machafu.tuliangalia mechi mpira ulivyoisha tukawa tunapita zetu kumbe tumepita jukwaa walilokaa wamekaa watu toka Majengo.mmoja alirusha jiwe likampiga mwenztu mmoja kichwan akachanika damu iliruka kama maji ya bomba lilipopasuka. masela wakapandisha mzuka.ezekia alikuwa kama ana mashetani hivi.akiona damu anapandisha mori.akaanza kutetemeka akacheki juu akawaoana jamaa kama 15 hvi akaanza kupanda huku anapiga kelele za kishujaa.

alimkamata jamaa moja shngoni akamrusha chini yule jamaa alitua hapa miguuni pangu akanyamaza kimya. nikashtuka na jamaa wenzetu nao wakapanda juu kuwafuata washkaji toka majengo.tulipigana ndani ya dk kadhaa polisi wakatia team n magari yao manne. wakaja kututawanisha. tulivyokuwa na akili mbovu tukawageukia polisi na kuanza kupeana nao kichapo. nilikuwa karibu sana na ezekia..inasemekana jamaa alikuwa amechanjia kwa macho yangu nlimwona akimvunja mkono polisi huku akiwa anapigwa virungu na polisi mwingine kama hasikii yeye amekamata mkono akaunyofoa kabisa.

nlichanganyikiwa hapo nilikimbia kuelekea kwenye ile mifereji ya kupitisha maji machafu nikafanikiwa kutoka.... baada ya muda nlimwona mtu anaaanguka chini kwa kishindo.alikuwa ezekia anatua aliruka ukuta. nje hali ilikuwa mbaya kila sehemu ni uwanja wa vita polisi walikuwa wameitana wameongezeka tumetawanyika tunapambana. polisi mmoja alikuwa na mbwa anatukimbiza alipigwa jiwe kichwan akayumba akaanguka na kumwachia yule mbwa ambaye aliendelea kutukimbiza.aliruka kumng'ata mmoja wetu na hapo ezekia alipoona jamaa ameumwa mguu alirudi akamkamata mbwa miguu ya nyuma na kuichana halafu akamshika yule mbwa anatoka utumbo akawa anamfuata polisi mmoja akamchape naye. yule polisi alikimbia ile mbaya.

hali ilikuwa mbaya sana na giza limeingia....polisi wameziba ile njia ya kwenda isanga na huku chini kwenda sangu hakuendeki. nilikimbia na kuingia kwenye mto....unaokatisha sinde na isanga. maji yalikuwa ni baradi nikaingia ndani wakat huo polis wanatufuata sasa wakiwa wengi wengi. kucheki namwona ezekia anapigana na polisi kama wanne hivi.yule jamaa hakuwa wa kawaida. nikaingia kwenye ule mto....polisi kuja kucheki wakasubiri kama ntaibuka maana kina kilikuwa kirefu halafu kuna majani mengi sana...kumbe mwenzao naogelea chini kwa chini mpaka kuja kutokea nyuma ya sehemu moja sikumbuki lile eneo ilikuwa ni gereji au kampuni ya nini lakini ilikuwa imezungushiwa na ndani magari makubwa yalikuwa yakiingia na kutoka.

kufika mbele nikatoka nikiwa na hema sana.kuchecki hivi nikamwona nyoka mkubwa sana....chatu. nilirudi kwenye maji kwa kasi kubwa ile kutua ndani kelele za maji zikawashtua wale maaskari nikasikia tu wakisema yule kulee... haraka wakaanza kuja na mbwa.kumbe yule chatu alishtuka naye akaruka kwenye maji halafu sijui ikawaje akajirusha tena nje maaskari wanafika na mbwa wanakutana na chatu. basi wakadhan nimejibadili chatu..... ilikuwa mshike mshike wakati huo mimi nimetoka tena kwenye maji nimepanda kwenye mti wa mafyurisi ulikuwa pembeni mwa ule mto.

nilisikia tu mbwa akipiga kelele then kukawa kimya...wale maaskari walitowekea huko mbali....sasa issue ikabaki mimi nipo juu ya mti nashukaje na usiku umeingia sana.... baada ya muda kiasi kwenye manyasi nikawa nasikia sauti ya yule chatu akijiburuza mpaka pale karibu na mto.alikuwa mkubwa sana.sikufaham kama alimmeza mbwa au alimkosa... giza lilikuwa limeingia ila kuna mbalamwezi flan hivi.baridi kali inapiga.... usiku huo sikushuka nikalala kwenye mti mpaka asubuh.

ile asubuh nikaangalia kwa umakini sana nikashuka haraka kukimbilia home.kule home walikuwa wamenitafuta ile mbaya.wakajua nitakuwa nmekamatwa na kuwekwa ndani.hivyo wakawa wanamtafuta babu ili akanitoe maaana yeye alikuwa maarufu sana na anaheshimika.

ile ilisambaa jioni ile na usiku walikuwa wameuawa raia watano na maaskari wa 3 nliwaza kuhusu ezekia.ilikuja kuambiwa alisalimika na hakuonekana toka usiku huo ila hakuwa sehemu ya zile maiti au waliokuwa wamewekwa ndani.kwa kipindi kile ilikuwa mara ya mwisho kumwona ezekia.

ilipita miezi kadhaa ikatokea siku moja bro karudi toka shule akawa analalamika kichwa kichwa. baada ya muda tu nimekaa nje nasikia kelele. kwenda ndani bro kavuta. ilikuwa balaah bibi katika kulia lia akaropoka kuwa hiyo ilikuwa kazi ya bibi kashinde. yeye ndo alimuua mtoto.... bro mdogo hakutaka kuuliza zaidi. si tulimwona ameingia ndani ilikuwa mida ya saa 1 kasoro.kumbe alitoka na panga aliruka ukuta akaondoka zake. alimfuata bibi kashinde. alimkuta amekaa ndani huyu bibi kwenye mkeka akitengeneza haijulikani ni nini.bro alimkata kata na panga ile kinyama hasa. akarudi home anavuja damu sisi kumwona tulishtuka sana haraka akaingia chumbani na kutoka na mkoba akatoka ndani speed sana. hatukumwona tena bro.

mara tukasikia kelele nyingi raia wamekuja home wanapiga kelele kuwa bro atolewe ndani.wakaingia na kukuta nako ndani kuna msiba na bro hayupo.inasemekana ni kweli yule bibi alikuwa mchawi.so wakawa katika shughuli zao bibi yetu yeye anagoma kutoa sadaka ila alishakula wa wenzie.so wakaona isiwe issue ndo wakamchukua bro. haraka baba mdogo na shangazi wakamchukua bibi na kumpandisha kwenye landrover ya mzee ba mdogo akatia gear na kuondoka naye. inasemekana alimpeleka nzovye, na siku iliyofuatia alisafirishwa kupelekwa huko mbali sana kyela mpakani wa tanzania na malawi.

baada ya msiba mzee aliamua kutuhamisha wote tuje kuishi huku.mimi ambaye nlikuwa nmeenda kuka mbeya na bibi ikawa ndo mwisho wa kukaa kule.yule bro wetu nlikuja kumwona mwaka 2005 alishakuwa raia wa zambia ana maisha yake huku huwa anakuja kututembelea tu na mbeya anapita juu kwa juu tu.

ni maisha ambayo sisi wengine tunapozungumzia uhuni au ununda tulifanya miaka hiyo...kuchomana vitu kabali mawe ilikuwa ni jambo la kawaida sana. sijajua maisha ya sasa ya huko nonde,sinde,isanga,machinjioni,sokomatola,majengo,uhindini,makunguru n.k

UPDATES.
KUNA MTU KANIFUATA ANANAMBIA YEYE NDO EZEKIEL TUNATAKA KWANZA KUTHIBITISHANA MAANA KILA MTU ANAMWOGOPA MWENZIE BAADA YA HAPO NADHAN NTAPATA KISA CHAKE.
 
Mkuu nimeisoma yote, miaka ile kila sikukuu lazima ngumi zilike, na ni za ukweli.

Halafu sikumbuki kesi zilikuwa zinaishaje ishaje.
 
Joseverest zamani ulikuwa mstaarabu sana..umepatwa na nini mpaka unapost hivi? nakumbuka jamaa mmoja ashawahi kusema kwenye post yake kuwa wewe ni mstaarabu ila sasa inaonekana umeanza kuiga uhuni wa kijinga. kama gazeti si unatuachia wenzio tunaopenda kusoma? acha kuiga mambo ya kipuuzi jose...
duuuh aisee sawa naona kama umepanic mkuu...samahani
 
why nipanic na thread nimeikuta tu. nmeshangaa uandishi huo ni wakihuni. sisi wengine tunapenda kusoma hasa visa na mikasa kama hii. so hata hii mi naona ni fupi. nimependa tu alivyosimulia kisa na visa hivyo. ni msimuliaji mzurina story ni ya kumbukumbu kweli... ila nikashtuka na comment yako.

Ndio maana Mbeya hamuendelei.
Uchawi, kupigana kijinga, kwa madhumuni yasiyoeleweka.
Watu, vijana wazunguka nchi nzima kuendeleza biashara na masoko nyie mwaendeleza ujinga!
 
why nipanic na thread nimeikuta tu. nmeshangaa uandishi huo ni wakihuni. sisi wengine tunapenda kusoma hasa visa na mikasa kama hii. so hata hii mi naona ni fupi. nimependa tu alivyosimulia kisa na visa hivyo. ni msimuliaji mzurina story ni ya kumbukumbu kweli... ila nikashtuka na comment yako.
Okay...Dont Bother
 
Back
Top Bottom