Nilivyo peleka Sera ya bana matumizi katika familia yangu

shonkoso

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
671
1,426
Baada ya pesa ya Mkulu kuadimka sana mifukoni mwangu ikilinganishwa na enzi za Mzee wa msoga,nimeona kuendelea kulalamika haitosaidia sana badala yake nione namna ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuangalia namna ya kupanua vyanzo vingine ambavyo serikali haitonidai kodi,maake kwenye kodi ndo wanakamua hadi kamtaji,nimefanya mambo yafuatayo ili kubana matumizi kulingana na kipato changu,wewe mwenzangu pia utanambia umefanya nini ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha

1.Nimepunguza kufanya manunuzi yasiyo ya lazima,nanunua vitu ninavyovihitaji na siyo ninavyovitaka2

2nimeacha kupikia gas,natumia Mkaa zaidi

3.Nimepunguza idadi ya matafiki wapenda starehe

4. Samaki,nyama ya ng'ombe ,ya kuku mayai,nakula na familia yangu tukipata wageni.

NB: KIPATO CHANGU KIMESHUKA TOKA AROUND LAKI SITA MPAKA TISA KWA MWEZI MPAKA LAKI MBILI AU TATU KWA MWEZI
 
Ongezea na haya machache..!

Epuka chai asubuhi, Kupunguza matumizi ya Sukari.

Godoro litumike siku za mechi tu, ili lidumu mda mrefu.

Ongeza juhudi ya kula viporo baridi, kuepuka matumizi ya mkaa..
 
Achana na matumizi ya umeme tumia mshumaa na koroboi. Pasi ya mkaa. Mkitaka maji ya baridi nunua mtungi. Asubub uji bila sukari. Saa nyingine ambia familia yako mchana mtawanyike mkale kwa jiran jion kila mmoja akupe marejesho.
 
Matumizi ya gas na mkaa hayana tofauti kubwa kwenye gharama fikiri upya.
 
Ongezea na haya machache..!

Epuka chai asubuhi, Kupunguza matumizi ya Sukari.

Godoro litumike siku za mechi tu, ili lidumu mda mrefu.

Ongeza juhudi ya kula viporo baridi, kuepuka matumizi ya mkaa..
Kwene viporo umenena mkuu.... Apunguze matumizi ya mkaa kwa kweli
 
Hakuna kitu ulichokifanya hapo solution ni kuongeza mauzo kwenye shughuli unayoifanya...kuwekeza kqenye kujitangaza ili ufahamike, kuwa na huduma bora kwa wateja...etc...
 
Cha msingi tengua ndoa yako mara moja, ukae mwenyewe utakuwa umekata 50%., kama kuna watoto waelekeze kwa ndugu
 
Back
Top Bottom