Nilivyo-date na mzungu nikajikuta Finland mpaka Malmo-Sweden

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kupenda penda huku sometimes

Kuna kijana wa kizungu tulifahamiana nikiwa Arusha kwenye shughuli zangu za kimaisha

Huyu ni raia wa Finland alikuwa anatoa huduma za kikanisa Arusha na Kilimanjaro, basi akawa amenitongoza basi tukawa tunawasiliana

Tukawa tumekuwa wapenzi lakini bila sex baada ya kukubaliana afya zetu kwanza

Yule kijana hata kabla ya penzi letu kukolea akawa ametakiwa kurudi Finland, akaanza kunishawishi kwa ahadi kem kem za kunioa ataachana na mambo ya kidini,atanitafutia kazi nzuri Finland ambayo itakuwa inaniingizia kipato zingine niwe natuma kwa wazazi huku Tanzania

Nikafikiria ,nikauliza sina hati ya kusafiria wala Vissa nafikaje huko,akanambia hilo ni jukumu lake

Siku ya siku akanambia kila kitu kipo sawa,akanambia siku fulani tuanze safari

Siku ikafika tukapanda basi hadi Nairobi,alfajiri tukaingia kwenye chopa mara nasikia tupo Dubai,mara Netherlands tukafika Finland mji wa Stockmann baada ya siku tatu, kijana akanambia tuchukue basi mpaka mji wa Tempere

Kumbuka hatujawahi sex ila tunalala pamoja

Itaendelea.....

Tulifika Tempere kituo cha kimisionari,wakatupokea na mwenzangu akanitambulisha kuwa nasoma chuo kikuu Gothenburg basi mafatha na masista wakatupokea vizuri

Tukakubaliana kuwa hapo tutaishi kama marafiki na tusionyeshe aina yoyote ile ya mahusiano ya kimapenzi

Maisha yakaendelea ,siku zikasonga nikamwambia huku tuna mpango gani,akanambia anasubiri apewe hela twende zetu Sweden kuishi,nikasema poa

Baada ya wiki hivi akawa tayari amepata pesa basi tukaanza safari kwenda Sweden mji wa Gothenburg ,tulipanda basi jioni saa 9 hivi za usiku tukawa tumefika Gothenburg

Tukachukua hotel moja hapo ya kufikia,tukapumzika saa 3 asubuhi tukaamka ,tukaoga na kubadilisha mavazi,kisha akanambia twende Garden moja kutembea,akachukua Tax mpaka hiyo Garden ndo akaanza sasa kunitamkia kuwa ananipenda na hapo ndo akanambia safari ya mapenzi rasmi yanaanzia hapa na akaleta kipimo tukapima afya zetu ,na madikodiko ya mapenzi ya kizungu yakaanzia hapo na mizawadi akanipa ya kutosha,wazungu wanaamini katika zawadi aisee

Huwezi amini muda huo wote pamoja muda mwingine kulala kitanda kimoja,pamoja na kukumbatiana kwa muda mrefu tukiwa faragha ,hakuwahi kutaka kusex,nikawaza wanaume wa bongo,asubuhi mnafahamiana jioni anataka uende kwake kulala au hotel mkasex,nikajua wazungu ni wavumilivu sana

Itaendelea.......
Jioni alinipeleka mgahawa moja unaitwa Jerzia kitchen,tukapata chakula aina ya sandwich,akawaza kunipeleka casino nikamkatalia ,nikamuomba tukalale,akaita Tax ikatupeleka mpaka mitaa ya Martin John ambako tulichukua hotel ya kufikia

Alfajiri akaamka akawa ameniaga kuwa anaenda maeneo ya viwanda kutafuta kazi hata za manual work ili kujikimu na maisha ambayo yalikuwa ya ghali zaidi

Alivyoondoka akaniacha nimelala mpaka saa 3 hivi ndo nikaamka nikatengeneza chai nikanywa

Kipindi hicho naangalia Tv habari za corona ndo zikawa zinaanza kuchipua kutoka China

Kijana akaenda hiyo mitaa ya viwanda inaitwa Stranda karibu na i akapata kazi kwenye kiwanda kutengeneza baiskel na bahati nzuri akawa amepata

Baada ya wiki hivi akawa amenitafutia kazi kwenye taasisi moja ya kidini katika jiji la malmo nikapata maana yeye alikuwa mwenyeji na alikuwa anafahamika kwa sababu awali alijishughulisha na dini

Kazi niliyopata ilikuwa ni kuuza vitabu ,majarida na magazeti ya dini hapo malmo ila akanipa tahadhari nisije nikawambia wafanyakazi wa hapo kuwa sisi ni wapenzi,nitafukuzwa kazi,pia akaniambia niwe naenda kanisani muda wowote kwenye misa na ibada kwa sababu moja ya sifa niliyopokelewa kuwa mimi ni mkristu

Habari za ugonjwa wa corona ukaanza kushika kasi duniani ,viwanda vikaanza kupunguza wafanyakazi hasa wa kawaida na kijana alikuwa miongoni,ukumbuke hapo nimehamia Malmo nakaa kwenye nyumba za wafanyakazi wa mission

Kijana alivyoachishwa kazi ilimbidi arudi Finland kwenye shirika la awali aendelee na kazi yake hata hivyo alitakiwa kurudi Tanzania ,akanambia kuhusu kurudi Tanzania kuwa aniache,nikamwambia hapana ,hapa siwezi kukaaa wala kufanya kazi maana niliona viashiria vya kibaguzi hasa sisi waafrika na wenye asili ya Latin Amerika na hasa vijana wa kiume wawili kutoka Haiti walikutana na ubaguzi kwa kweli hadi huruma

Kwa hali ile nikamwambia hawezi akaniacha ulaya ,akanielewa akawa ameanza kunitafutia hati za kusafiria kama mfanyakazi wa taasisi ya kidini na kama raia wa kenya kama ilivyokuwa mwanzoni basi safari hii tulipandia ndege Denmark jiji la Copenhagen maana kutoka Malmo ni dakika chache tu

Tukashukia Nairobi gari la shirika likatuchukua hadi Arusha,yeye akawa anakaa moshi mimi Arusha,wakati huo penzi linaendelea

Habari za kufunga mipaka ikawa imeanza kule ulaya,akaomba arudi nyumbani ndipo akarudi Finland
 
Kumbe wazungu Wana swaga kama zetu ,sema zao hazina mbwembwe , huyo mzungu mshipa hausimami, Kwa msambwanda wako huo ulitakiwa uiname kutwa mara tatu kama dozi ya panadol ...Ila mkuu nipe connection nitokomee Sweden maana bongo nyoso ...
 
Mkuu wametupiga marufuku Kuingia Christiania kwaajili ya Corona. Unatakiwa kupita tu hamna kujichanganya.

Covid sasa hivi imechachamaa inakula vichwa vya madereva Teksi vibaya sana copenhagen
Dah napamis sana hapo christianiaa
kwa nyomi la humo ndani+vurugu
Lazima wapige maarufuku

Ova
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom