Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
3,983
10,804
Mkasa : NILIVUNJA NDOA ZANGU 3 KULIPIZA KISASI
Mwandishi: IRENE MBOWE (Irene Mbowe Kungwi Lao)
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES


KISA CHA UKWELI ANACHOSIMULIA CHARLOTE, ANASEMA HIVI, MAJIBU YA MAMA WA HAWARA WA MUME WANGU YALIVYOSABABISHA NIKAVUNJA NDOA TATU.
Charlote, mwanamke aliyeishi kwenye ndoa yake kwa miaka 5. lakini baada ya kukutana na changamoto za ndoa ambazo alishindwa kuzivumilia na kujikuta kuwa na kisasi rohoni, Sasa aliamua kulipiza kisasi hicho na kupelekea kuvunja ndoa tatu. Hembu msikilize Charlote anachokisimulia. Hii inaweza kukusaidia sana katika maisha yako kutokuwa na kisasi moyoni.


SEHEMU YA 1: KUPENDWA RAHA

PART 1

Nimelelewa kwenye mazingira ya maisha ya utulivu na amani. Wazazi wangu walipendana na kuheshimiana sana. Na kutufanya sisi watoto wote kuwa na heshima na kupendana . lakini pia kujali jamii iliyotuzunguka na kuishi kwa adabu sana.

Nilipata bahati ya kupata elimu nzuri na ya viwango. Wazazi wetu walitusomesha, tena shule zenye hadhi na gharama kubwa mno.
Nikiwa kidato cha pili , Mtoto wa mzee ambaye ni family friend na sisi aliingia kidato cha tano katika shule niliyosoma. Hivyo kijana huyu Jones tuliheshimiana sana. Alinipenda na nilimpenda wote tulipendana na kuhurumiana na kuheshimiana.

Wengi shuleni walijua sisi ni family friends, na hivyo kila mmoja ni kama alikuwa akimchunga mwenzake. Jones aliogopa kufanya upuuzi akiamini ni lazima ningemsemea nyumbani, lakini na mimi pia niliogopa kufanya upuuzi nikiamini kabisa jones angenisema Nyumbani.
Hivyo Jones na mimi tukajulikana kama wana ndugu haswa haswa, na heshima ikawepo. Sikuwa na utani wala mizaha na watoto wa kiume.. hii ni kwa Vile Jones alikuwa akinifuatilia sana. Lakini na mimi nilimfuatilia sana kuhusu kuwa na mazoea na mabinti na hivyo aliogopa pia nay eye.

Wengi walisema Jones na Charlote ni ndugu. Wengi wa vijana walimtania Jones na kumwambia mwenye dada hakosi shemeji. Na Jones alichukia sana.

Tuliendelea kupendana sana.

Baada ya kumaliza masomo ya Secondary Jones alienda kujiunga na chuo wakati mimi nikiendelea na masomo ya Secondary. Lakini tuliendelea kuwasiliana sana. Na hatukutupana hata kidogo.

Alinipenda na kunikumbuka kila mara.

Nilipomaliza kidato cha sita, yeye tayari alikuwa ameshaanza kazi ya kuajiriwa.

Na sasa nilikuwa najiandaa na mimi kuanza chuo.

Nakumbuka siku moja alinipigia simu na kunitaka tukutane tuzungumze. Wana familia walijua urafiki wangu na Jones. Hakuna aliyekuwa na mashaka juu ya urafiki wetu. Kila mmoja alitupenda na kutufurahia kwa urafiki wetu.

Nilimpa ahadi Jones ya kukutana na mimi. Kwanza nilishangaa sana kwa namna ambavyo alikuwa kabadilika. Alikuwa kanawiri sana, kawa na hali ya utu uzima zaidi na pia alionekana ni kijana ambaye alikuwa na pesa.

Tulikutana na kukaa mahali kwa ajili ya kuzungumza.

Kitu cha kwanza aliniuliza …
Charlote,,, je una rafiki ama mpenzi?
 
SEHEMU YA 1: KUPENDWA RAHA
PART 2



Nilitabasamu sana kwani moja kwa moja nilianza kuona akili yake ikiwa inanihitaji kuwa mpenzi wake. Ni kweli sikuwa bado nina mahusiano. Na hii ni kwa vile nilikuwa sitaki kuwakere wazazi wangu na nilitamani mahusiano nitakayokuwa nayo yaishie kwenye ndoa ni we mke wa mpenzi nitakaye kuwa naye. Badala ya kubadilisha mara huyu ama huyu kama nilivyokuwa nikiona wengi. Hivyo niliamini nitakapofikisha umri mkubwa ndipo nianze mahusiano. Wakati huo nilikuwa na miaka 20 wakati Jones akiwa na miaka 26.
Aliniuliza kwa kusisitiza tena, je una mpenzi?

Nilimjibu hapana sina mpenzi na si hitaji. Ni kama hakamini.

Ila akaamua kufunguka na kuniambia kwamba,, hata yeye hana mpenzi na hana mahusiano, ila amekwua na marafiki kama marafiki lakini amegundua kwamba marafiki hao hawana viwango avitakavyo. Na aliogopa kunieleza kwani alifikiri tuna mahusiano ambayo yasingeweza kuruhusu sisi kuoana.Ila baada ya kuongea na wazazi wake walimruhusu na kumueleza kama Charlote atakubali kuwa mchumba wako haina neno. Hivyo akaamu akusitisha urafiki wowote na hivyo kuja kuniuliza kama niko tayari.

Nilishindwa kutoa jibu la haraka kwani sikuwa tayari ninamhitaji. Alionekana ni kijana nadhifu, msomi na mwenye upendo. Lakini bado sikuwa na hitaji mpenzi, hivyo nilimueleza sina mpenzi na sihitaji mpenzi. Na nilimueleza kwa nini sihitaji mpenzi, na sababu mojawapo ikiwa ni kwamba natamani mpenzi nitakayekuwa na mahusiano naye awe mume na sio kuwa na wapenzi wengi wa kila mara.

Jones alinitazama na kuonyesha anamaanisha anachotaka kukisema.

Aliniambia,, Sharlote wewe ni msichana mrembo sana, na ukweli ni kwamba nakupenda sana, na kwa vile sasa hatuna uhusiano wa kindugu kama nilivyofikiri natamani kama ungekuwa mpenzi wangu kisha uwe mke wangu.

Nilimtazama na nilifahamu kabisa kwamba Jones anamaanisha mimi kuwa mpenzi wake. Sikuwa na historia mbaya ya Jones hata kidogo. Lakini bado sikuwa na sababu ya kumkubali. Bado jibu langu lilikuwa ni mapema sana, nahitaji kusoma na kuwa na kazi ndipo maswala ya mapenzi niyaanze.

Aliniambia anaweza kunisubiri na kunihakikishia kwamba nikimkubali nitasoma, nimalize nipate kazi ndipo anioe. Kama hilo ndilo ningelihitaji.

Nilitabasamu na kumwambia ni mapema mno sina jibu la kumpatia ila asubiri.

Aliniambia Charlote tafadhali najua mapema utaenda chuo. Hivyo endapo utakuwa na maamuzi ya kuwa na mahusiano usinisahau, ninakuahidi sitakuwa na mahusiano mpaka utakaponieleza msimamo wako .

Tulimaliza maongezi yetu na kila mmoja akaondoka.

Siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwangu, kwani sasa nilianza kuwa na shauku ya kuwa na mpenzi. Niliyatafakari maneno ya Jones usiku kucha. Nikiamini kabisa alikuwa anamaanisha anachokisema.

Nilipokuwa naendelea kutafakari aliniandikia msg na kuniambia,,, CHARLOTE TAFADHALI KABLA HUJAAMUA KUMPA MTU NAFASI NAOMBA UNIFIKIRIE MIMI, NAKUPENDA SANA, NAKUFAHAMU NA NINGETAMANI UWE MKE WANGU . WEWE NI MZURI SANA NA MREMBO MNO, BADO SIJAONA MWANAMKE MZURI NA MREMBO KAMA WEWE.

Nilipomaliza kusoma msg ile niliisave ili iwe kumbukumbu yangu, ni msg ya kwanza ya kimapenzi kuipokea yenye nguvu na heshima. Si kama nilizozoea kusipokea za kishenzi na kipuuzi puuuzi.

Hivyo niliisave.
 
SEHEMU YA 2: PENZI JIPYA LINACHIPUKA
PART 1


Muda wa kwenda chuo ulifika. Wazazi wangu walinipenda sana, hivyo walinitafutia chuo kizuri na nilichokipenda Nchi jirani. Nilianza masomo yangu ya Usekretari. Lengo langu ni niwe na kiwango kikubwa cha taaluma hii. Wengi waliniambia Charlote wewe ni mrembo sana, unapendeza sana ukifanya kazi kwenye maofisi makubwa. Urembo wako na kazi ya usecretari vitakufaa sana. Kila mtu aliniambia hivyo, na hata nilipokuwa shule ya sekondari kila mmoja aliambia hilo, hivyo nikajikuta natamani sana Taaluma hii. Hivyo nikiwa nchini Nairobi niliisoma vyema na kuhakikisha nafaulu vyema.

Niliipenda sana Taaluma hii, na nilifanya vizuri sana.

Tuliendelea kuwasiliana na Jones, nilimueleza ninachokifanya. Na bado nikiwa mwaka wa kwanza chuoni bado sikuwa nimemueleza kuhusu suala la mimi kumkubali yeye kuwa mpenzi wangu.

Lakini nikiwa Nairobi nilikuwa na kijana rafiki tu ambaye ni Mtanzania, isipokuwa naye alikuwa ni rafiki na si mpenzi. Na sikumpenda kama mpenzi ila rafiki ili niwe na mtu wa karibu mtanzania mwenzangu. Hivyo niliamua kuwa na urafiki naye wa karibu nikiamini kuwa na mwanaume rafiki nitakuwa salama.

Nilipendeka sana chuoni, wanaume wengi walinipenda na kunitamani, lakiini bado msimamo wangu ulikuwa pale pale sihitaji mpenzi wa kuniacha, ila mpenzi ambaye atakuwa mume.

Muda ulipita nikiwa chuoni , na nilisifika kwa tabia njema na kujiheshimu, wengi walinifurahia na hawakuweza kuwa kama mimi kwani walikwua na tama sana.

Nakumbuka siku moja nikiwa hostel. Nimejilaza. Rafiki yangu Penina, msichana wa Kinyarwanda ambaye tulipenda sana, na wengi walisema tumechaguana warembo,, alikuja kuniamsha na kuniambia .. Charlote,,, uko na mgeni, kijana handsome sijui katoka wapi ila ana sound kama mtzedi… he is outside anakusubiri kwa nyumba ya wageni ukaonane naye…

Mh… haraka nilijua huenda ni kaka zangu na si mtu mwingine, wazo halikuwa kwa Jones kabisa.

Dah.. sikuamini kwa kadiri nilivyokuwa nikisogeza hatua zangu.. nilimuona kabisa ni Jones,, nilianzakupata furaha sana moyoni. Nilimsogelea na kumkumbatia kwa furaha kama mtu na kaka na dada yake. Nilifurahi sana kumuona.

Tulizungumza na akaniambia kama naweza kupata ruhusa ya kutoka chuoni na kwenda mjini basi nifanye hivyo na siku inayofuata atanirudisha kwani ilikuwa ni week end. Nilizungumza na rafiki yangu Mnywaradwa Biera na alikubali kwamba tutoke. Hivyo tukaomba ruhusa na kkwetu ilikuwa rahisi sana kuruhusiwa kutokana na tabia zetu. Tuliondoka na Jones na Biera mpaka mjini.

Jones alituvutisha raha za kila namna, tulikunywa, tulikula na kufanya shorping. Kisha jioni wakati wa dinner kabla hatujaenda kulala kwenye hotel nzuri ya kifahari aliyobook kwa ajili yetu nay eye, aliniomba sana nimpatie jibu.

Alinieleza nia yake na lengo lake kwamba bado anahitaji niwe mpenzi wake.

Sikuona sababu ya kukataa sasa. Moja kwa moja kwa moyo wa hiyari kabisa, nilimwambia Jones nampenda na niko tayari kuwa na mahusiano naye ya mapenzi , awe mpenzi wangu na kisha mume wangu. Na nilimueleza kwamba natamani sana tuheshimiane, tupendane na kuwa mke na mume kama Mungu akitupa maisha.

Jones alifurahi na kwa mara ya kwanza kuona machozi ya Jones. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwake mimi kumkubali.

Tulilala usiku huo. Mimi na biera kwenye room yetu. Usiku kucha tulipiga mastory na kumueleza juu ya Jones. Biera alinishauri vyema na kuniambia nimepata kijana mwenye anaonekana ni smart, muaminifu na anayemaanisha mahusiano. Aliniambia sio kijanahohe hahe ni kijana ambaye yuko smart na very handsome and educated.

Tulifurahi na kulala.

Asbh tuliamka na kuelekea kwenye chai. Kisha tukazunguka tena mjini na ndipo sasa Jones akaturudisha chuoni. Huku akinisisitiza kwamba mimi nay eye sasa tuko kwa stage ingine kabisa na sio ya urafiki tu, ni urafiki wa uchumba kwani tunafahamiana miaka mingi, hivyo ni vyema sasa tukaheshimu mahusiano hayo.

Nilimuhakikishia kwamba mimi niko salama sana na asijali, nay eye pia awe salama.

Aliondoka na kuniacha. Nilianza kumuwaza sana, nilianza kumuona alivyo mzuri,na kijana wa thamani sana kwangu.

Nilimfurahia sana Jones. Lakini Biera naye aliniambia sio kijana ambaye ni chokoraa ama mang’aa. Akaniambia kwa namna vile anaonekana kama angekuwa mang’aa angetafuta tu msichana wa kuspendi naye na asingehangaika kuja naibori kwa ajili yangu. Nilimuelewa Biera.
 
SEHEMU YA 2: PENZI JIPYA LINACHIPUKA
PART 2


Sasa Jones alianza kunifuatilia kwa simu. Alipiga simu kila mara, alijua natoka darasani saa ngapi na aliongea na mimi zaidi ya lisaa kila siku mara agunduapo niko na nafasi. Wakati mwingine nilichelewa hata kuoga ama kula. Hii ni kwa sababu alishikilia simu muda mrefu. Na kama ingekuwa naongea na simu basi ni lazma nimueleza naongea na nani.

Jones aliingia wazimu juu yangu. Na mimi sikushawishika kutompenda, ila nilimpenda zaidi na zaidi.

Muda ulipita. Sasa ni mwaka wa pili niko chuoni.

Jones ameshajulikana kila mahali, si chuoni wala nyumbani kwamba ni mpenzi wangu na mchumba wangu.

Wasichana wengni walinionea wivu, hali kazalika vijana wa kiume nao. Walinitamani sana na walitamani mahusiano yetu yangekuwa kamayao. Kwani mara nyingi walikorofishana.

Biera naye alikuwa akikorofishana na mpenzi wake kila mara.

Jones alifika Nairobi kila mara alipohitaji, hasa siku za jumamosi na jumapili, hivyo ijumaa jioni nilitoka chuoni na kurudi jumatatu asbh.
Tulipendana sana. Na tulpofunga chuo Jones alikuja na kunichukua na gari yake.

Marafiki wa Tanzania walinitamani na waliomba lift ila Jones aliniambia hakuja kuchukua chuo ila kunifuata mimi hivyo hawezi mpatia mtu yeyote lift, isipokuwa mimi ambaye ni mpenzi wake.

Mapenzi yalipamba moto. Tulipendana sana.

Niliporudi kutoka chuo, nilifikia kwa Jones ambaye alikuwa na nyumba yake aliyopangisha, nilikaa kwake siku tatu kisha ndipo nilienda nyumbani, na muda wowote alinifuata nyumbani na kutoka na mimi. Wazazi wangu walimpenda kijana ambaye alijiheshimu sana.

Wakati narudi chuoni kwa ajili ya kumaliza elimu Yangu, Jones aliniomba kunivisha pete. Nilimuomba anivishe pete mara baada ya mimi kumaliza chuo. Aliniambiahapana naomba kabisa nikuvishe pete ya uchumba, nilimuomba sana asubiri. Na akakubali.

Nilienda chuoni nikiwa msichana mwenye furaha na kujiona ni mwenye bahati sana.

Maisha yaliendelea kwa furaha mno. Na nilibahatika kufanya mitihani yangu vyema.

Kabla sijamaliza chuo, Jones aliniambia kaka yake anaoa, na angependa nihudhurie harusi hiyo. Nilimueleza situation ya masomo, aliniomba sana kwamba nichukue ndege nifike jijini kwa harusi na baada ya siku mbili nitarudi.

Nilimtii wkani nilimpenda. Alinilipia tiketi ya ndege na kwa mara ya kwanza nilipanda ndege. Nilienda kwa ajili ya harusi ya kaka yake. Alinipeleka shorping kwa ajili ya nguo za harusi. Kisha Jumamosi siku ya harusi tukawa tuko pamoja kwa ajili ya harusi ya kaka yake
Kila mtu alimhurumia na kumwambia huyo Charlote kakukamata haswa, na alifurahi kusikia hivyo. Alikuwa muaminifu sana kwangu, na hakuwa na mahusiano na msichana yeyote Yule. Mara nyingi aliambiwa ukimuamini sana Charlote iko siku atakutenda, na mimi sikutaka kukamilisha ndoto hizo na misemo hiyo mibaya. Hiyvo nilijitahidi kumpenda na kumuonyesha yuko mahali salama na kwenye penzi salama . na sikushawishika na kutamani mwanaume yeyote.

Harusi ilikuwa kubwa sana na ilifana sana.

Maharusi waliingia ukumbini kwa nderemo na vijijo.

Kisha wageni waalikwa nasi tukaingia ukumbini.

Baada ya utambulisho, Maharusi walifungua champagne kisha tukagongeza kuwatakia mafanikio mema.

Baada ya Hapo Jones naye alipewa nafasi ya kuongea, sikuwa na wasi wasi kwani nilijua anataka kusema jambo kama mwanafamilia.
Kisha Jones alisema kwa sauti ya juu kwa kutumia kipaza sauti… CHARLOTE MY LOVE WHERE ARE YOU?

Ukumbi mzima ulitulia kutaka kujua nini kinaendelea. Nilitoka nilipokuwa, hofu na kutetemeka kwa aaibu kutokana na umati wa watu, na sikuwa na ujasiri wa kusimama mbele za watu wengi. Ila kwa vile nilimpenda sana Jones sikutaka kumuangusha, nilijikaza sana huku natetemeka.

Kisha nikafika, na akanibusu. Baada ya sekunde kazaa alitoa kitu mfukoni mwake,, na kusema..

Huyu hapa ni mpenzi wangu, rafiki yangu na mchumba wangu, mke wangu mtarajiwa, naomba kusema kwamba baada ya harusi hii ya kaka inayofuata ni yangu…

Charlote will you marry me?

Dah…. Ilikuwa mtihani,, nilijikuta naogopa,machozi yanatoka,,, na Jones naye hali kazalika… Alipiga magoti na nikamwambia yes,,, will marry you….

Watu walishangilia sana, na kufungua champagne. Kisha nikaenda kukaa na wazazi wangu walikuwa harusini kwani ni family friend wakaambiwa Jumamosi ijayo wajiandae na ugeni wa kupelekewa mahari.

Ilipendeza sana japo nilishtukizwa kabisa.

Harusi iliishia vyema na nikarudi chuoni.
 
SEHEMU YA TATU: KARATA YA BARADHULI
PART 1


Nilimaliza masomo yangu salama. Na tayari nilikuwa na ujauzito wa miezi 2. Kwanza Jones alifurahia sana kusikia nina ujauzito. Haraka mipango ya harusi ilifanywa na tulioana, na sasa ikawa ni mke na mume rasmi. Harusi yetu ilifana sana, ilipenda mno. Na wengi walitupenda, na baada tu ya mimi kujifungua tulisimamia harusi kama mbili hivi, hii ni kwa vile waliotuomba tuwasimamie walivutiwa na maisha yetu ya ndoa na kupendana kwetu.
Jones alinipenda sana.
Nilipata kazi nzuri nay a mshahara mzuri kutokana na elimu yangu ilivyokuwa ya juu. Nilifanya kazi kwenye ofc kubwa mjini na ambao wanalipa vizuri.
Haraka sana Mume wangu alininunulia gari nzuri ya kutembelea na kuniambia hataki nipate shida.
Nilimpenda Jones nay eye alinipenda sana.
Sikuwahi kumuwazia mambo mabaya hata kidogo. Na pia hatukupenda kugombana wala kulumbana kwani wazazi wetu walipendana sana na hatukutaka kujiaibisha. Mara tulipokoseana pole pole tuliambiana na kurekebishana kabla mambo hayajawa magumu na mabaya zaidi.
Hivyo matatizo ya ndoa yetu hakuna aliyeyajua zaidi yetu wawili.
Nakumbuka ni mara moja tu Jones aligomba kwa tabia yangu ya kunywa pombe, na nilimuahidi kuacha, kwani nilikuwa natumia pombe hasa balantine, na alipokuwa akisafiri ndipo nilikunywa sana. Japo sikuwa natoka ila nilinyewa nyumbani tu. Na alinikataza tabia hiyo. Na siku moja aliniaga anasafiri na kwa vile nilimwambia nimeacha alitaka kuhakiki je nimeacha ama la? Na hivyo alisafiri safari feki na kurusi na kunikuta niko bwii. Alikasirika sana na kuniitia mama yangu anionye. Huu ndio ugomvi ambao naweza kusema kwa mara ya kwanza niliuona mkubwa na kumuona Jones alivyobadilika. Na kuanzia siku hiyo nilimuahidi sitakunywa tena pombe. Japo sikuweza kwa mara moja ila nilimuahidi sitakunywa tena pombe.
Ndoa yetu na maisha yetu yalkuwa gumzo mtaani , kwenye familia , kwa ndugu na marafiki, hata wafanyakazi wa jones na wafanyakazi ninaofanya nao kazi walikwua wakitushangaa sana.
WENGI WALISEMA IVUMAYO HAIDUMU….. NA WALITUBEZA MNO.
WENGINE WALITUFURAHIA, WENGINE WALITUTAMANI.
Ndani ya ndoa ya miaka mine nikabahatika kupata mtoto mwinngine. Mungu akatujalia watoto 2. Tuliwapenda sana. Walikuwa wavulana wote, walifanana na sisi sana.
Maisha ya ndoa yalikuwa matamu haswa.
Sikuwahi kumuwazia Jones kuwa na mwanamke hata kidogo.
Nakumbuka siku moja nikiwa natoka kazini, niliamua kumfuata ofcn kwake ili tupitie mahali nimuonyeshe friji ili tununue. Ilikuwa ni saa kumi na moja.
Wakati natoka napanda ngazi za ofcn kwake nilikutana na mfanyakazi mwenzake, aliponiona alirudi kwa speed ya ajabu, nilishikwa na butwaa nini kinamrudisha? Lakini nikasema ni ofc za watu.
Sikujali sana, nikaendelea kupanda ngazi. Kisha ghafla nikapishana kwenye ngazi na msichana ambaye ninamfahamu. Lakini hakunisalimia, ila alinipita kwa kasi ya ajabu, niligeuka nyuma kumtazama na aliendelea kuziruka ngazi kwa speed ya ajabu mpaka akamalizikia sikumuona tena, Nilipogeuzauso wangu nilikutana macho kwa macho na Jones, alinikumbatia na kunibussu, kisha akanishika mkono na kunipelake ofcn kwake. Akanipatia juice. , na nikamueleza kilichonipeleka kwake na tukaondoka kuelekea madukani na kununua friji hiyo kisha kwenda nyumbani.
Siku hiyo mume wangu alionekana kuwa busy sana na simu sana, na si kawaida yake. Na tuliwekeana sheria hakuna kuweka simu pw, na kila mmoja ana ruhusa na simu ya mwenzake. Na hii ilitufanya tukaaminiana sana na kutokuwa na wasi wasi kwenye ndoa yetu.
Kwa vile ilikuwa ni sheria sikuona shida nilijua tu acha awe busy kuna saa nitaishika simu yake na kuikagua.
Na kweli usiku kabla ya kulala nilimuomba simu yake na nilifanikiwa kuikagua.
Nilikuta ametuma msg na kasahau kuifuta na kasema ,, Samahani Husna naomba tuongee kesho nimeshafika nyumbani sihitaji kukuudhi, tutaongea kesho mpenzi.
Dah,, nilipaniki kimoyo moyo,, lakini sikumuonyesha kama nimejua, ila Husna ni binti ambaye alinipita kwenye ngazi na speed za ajabu, Namfahamu mama yake, namfahamu baba yake, na ninawajua ndugu zake. Dah. Kiliniuma. Kisha nikafuta ile msg wala sikumuonyesha mume wangu kwamba nimejua kitu.
 
SEHEMU YA TATU: KARATA YA BARADHULI
PART 2



Usiku sana muda wa saa saba nilimuamsha, nikamwambia Jones, naomba usinifiche, niambie ukweli wote kuhusu jambo nitakalo kuuliza.
Je husna ni nani? Kwanza alisema alienda kuomba kazi, mara mpenzi wa mfanyakazi mwenzake nk. Nilikasirika nikamwambia kwa nini unanidanganya? Akaniambia mke wangu sio kweli sina mahusiano naye.
Nikamwambia poa haina neno.
Tulilala, asbh nikakasirika sana, nikampigia Husna simu kumuuliza ana nini na mume wangu, alipokea simu na kusema hana mahusiano yoyote ila ni kama shemeji yake. Nilinyamaza na nikamuuliza anatoka na nani akaniambia anatoka na Damson. Nikamkumbuka Damson. Nikampigia simu, nikamuuliza shem samahani, Husna unamfahamu? Akasema ndio namfahamu, nikamuuliza ni nani? Akasema kwa nini shem unaniuliza hivyo? Nikamwambia mbona kasema ni demu wako? Kwani wewe umemuacha prisca? Maana alijua namfahamu prisca, akasema aa shem vunga. Kisha akakata simu, na mara simu yake ikawa busy sana, nikajua anaongea aiza na Husna ama Mume wangu. Haraka nikampigigia mume wangu, simu ikawa busy sana. Nikanyamaza.
Jioni mume aliporudi home akawa kaweka simu pw. Tena kwenye kila kitu, nikamuuliza kulikoni? Akasema naona tu tutakosana kisa simu, naona niweke pw. Na mimi nikamwambia so na mimi niweke sio? Na mimi nikaweka. Kisha nikaanza kugombana naye, kwanza nikampigia Prisca nikamuuliza kuhusu Husna, akaniambia Charlote naomba tu nikuambie kweli, Husna anatoka na mumeo, ila wanatabia ya kusame ni demu wa Damsosn ili usijue. Lakini Husna anatoka na mumeo, ila wewe tulia nitakukamatisha naye. Wewe nyamaza.
Prisca akanihakikishia kuwakamata. Na kweli akachonga njia mpaka akanipigia simu siku moja na kuniambia niende ofcn.Nilifika ofcn na kweli hamadi, Husna na mume wangu hawa hapa . Sikuamini, kwanza aligoma kufungua ofcn lakini nilisukuma mlango wa alminium ambao niliwaona kwa ndani .
Jones hakuamini, aliogo pa sana, niliomba tu wafungue, mwisho akafungua. Kiliniuma sana, nikamwambia Husna ni nini hiki? Hakunijibu, nikataka kumshika nimpige akaniponyoka.
Nikamwambia mume wangu ni nini unanifanyia? Akaanza kuomba msamaha, mwisho nikaona sina sababu ya kuendelea kulumbana naye, nikaondoka na kwenda nyumbani, kufika nyumbani nikalia sana, kikaniuma sana.
Akaja na kuniomba msamaha, nikamuuliza kulikoni nini anakosa? Hakuwa na jibu. Nikamuuliza mimi nikifanya hivi utajisikiaje? Hakujibu pia.
Alikuwa mpole sana. Akaniambia nisamehe mke wangu sitarudia tena naomba yaishe.
Nikamwambia poa haina neno, ila asante sana.
Kuanzia hapo nikaanza kujiuliza inakuwaje mume anabadilka hivyo. Mume niliyemjali kiasi hicho na kumuamini.
Niliogopa kuwapa watu faida, nikasema sitaondoka wala kufanya lolote, ila nitaenda kumshtaki Husna kwa mama yake.
 
SEHEMU YA NNE: MWANAMKE AKITAKA KULIPIZA KISASI, SHETANI HUWA ANAKAA PEMBENI AJIFUNZE KITU
PART 1


Nilijua mama yake Husna alipofanyia kazi. Nilimfuata asbh sana, kabla hajaingia ofcn kwake.
Nilimsalimia na kumwambia mama samahani nataka kuzungumza na wewe.
Namna alivyonitazama ni kama aliyenibeza na mwenye kujua jambo, niligundua hilo mapema sana.
Nilimwambia shikamoo mama, alinitazama chini juu, hakuniitikia. Ni mwanamke mweusi mnene na mfupi. Hivyo hata aliponitazama ilikuwa ni rahisi mimi kujua ananitazama yani kunishusha kwani ilibidi anyanyue sana shingo kunikuta nilipo.
Sikkujali, alisema enhe unasemaje?
Nilimwambia mama samahani,, nimegundua mwanao ana mahusiano na mume wangu.
Akaguna, na kusema ninao watoto wengi ni nani?
Moja kwa moja nilisema ni Husna…. Alicheka kwa kejeli,, akaniambia,,,
Uliwashika ama ni umbea umekusanya mtaani?
Nikamwambia niliwashika.
Akaniambia uliwashika wapi? Nikamwambia niliwashika ofcn kwa mume wangu.
Akaniambia kwa hivyo huyo mumeo haruhusiwi kufanya kazi na wanawake? Kwani uliwakuta wako uchi ama?
Mh.. hii ilinishangaza,, nilijiuliza huyu ni mama ama ni Jini? Mbona hana huruma kama hajaolewa?
Nilimwambia mama nina uhakika ndo maana nimekuja ili umuonye mwanao.
Akaniambia naona huna jipya mama,,, sikia,, naomba sisikilizi umbea, Nenda kamtosheleze mumeo sawa.
Alivuta hatua na kuniacha nikiwa nimeshangaa nisijue la kufanya, kiliniuma sana.
Nilienda kazini kwangu huku nina mawazo debe zima.
Nililia sana, ila kwa vile sikutaka ofcn wajue kisa changu nilijikaza sana na kunyamaza tu.
Sikuongea lolote.
Baada ya muda kidogo Husna akaniandikia msg na kuniambia,,, Umeongea na mama yangu ili nini? Itakusaidia nini? Mchunge mumeo usinifuatilie.
Niliisoma ile msg bado nikajikaza, nikasema sina sababu ya kushindana kwa maneno, nahitaji matendo zaidi.
Nikanyamaza kimya sikuijibu.
Nikamaliza kazi nikaenda home kama hakuna kilichowahi kutokea.
Nikaanza kujidunga balantine moja. Kila siku lazima soda moja ya ginger lemon na glass ya balantine.
Kila jioni, ili kupoteza mawazo. Na jones alishindwa Kunizuia kwani sasa alikuwa na kosa na hakutaka kukubali kosa. Kuomba msamaha anashindwa, kuniambia nisinywe pombe anashidwa,
Akaniambia mke wangu naomba tufungue simu zetu.
Nikamwambia sio tu kufungua yani yangu hata chini sitakaa niiache. Nitaenda nayo mpaka chooni. Nikaweka pw kila kona, japo sikuwa wala na baya la kufanya.
Nikawa nawaza nifanye nini ili roho yangu isikie raha?
Miezi mitatu nilikuwa nikinywa tu pombe huku nawaza nifanye nini.
Je nimpige ama kumfanyizia Husna? Je nimfanyeje? Nikaona haya yote hayamfai.
Nikajikausha kama sio mimi, nikaanza kumpotezea, na kuanza kuishi maisha yangu mimi kama mimi.
Mume wangu akaanza kuwa na wasi wasi akasema anaomba nisifunge simu yangu, nikamwmabia poa.
Nikafungua pw zote na nikamwambia simu hii hapa.
Maisha yakaenda.
Baada ya miezi mitatu kuuisha nikafuatilia nikagundua mume wangu na Husna wameachana. Hawana mahusiano kabisa, na Husna kapata mpenzi wake.
Nilianza kumfuatilia Husna kujua mpenzi wake ni wa wapi, na nilijua na kujua ofcn anayofanyia kazi.
Na baada ya muda nikasikia husna kavishwa pete ya uchumba. Kwangu ilikuwa ni shangwe siku hiyo. Nilifurahia sana, nilijisikia rah asana, Nilikunywa sana usiku huo. Husna alikuwa na miaka 25 hivi. Na mpenzi wake kama miaka 28. Na mimi nilikuwa na miaka 28 na mume wangu miaka 34.
Baada ya kuhakiki kweli husna ana mchumba nilitulia kidogo huku napanga mbinu zangu za kulipiza kisasi.
 
SEHEMU YA NNE: MWANAMKE AKITAKA KULIPIZA KISASI, SHETANI HUWA ANAKAA PEMBENI AJIFUNZE KITU
PART 2



Siku moja nilikuwa nimekaa ofcn,, nikakumbuka Babayake Husna mzee Zuberi Muarabu anapofanyia kazi, niliinua simu yangu na kutaka kuongea na Huyo mzee nimsikie ni wazee wa aina gani?
Nilimpigia simu na kuongea naye, alikuwa ni boss wa kampuni Fulani mahali Fulani. Nikamwambia samahani Baba mimi naitwa Charlote, naomba nije na cv’s zangu ili kama unaweza unisaidie kazi.
Aliniambia sasa hivi hawana nafasi za kazi. Nilitumia akili ya kike ya kumshawishi aniruhusu tu nizipeleke ili likitokea la kutokea basi anisaidie. Alikataa sana, lakini badae alikubali.
Na ndipo nilisema sasa njama zangu za kulipiza kisasi zimekamilika.
Siku ya jumatano asbh saa nne nilitoka nyumbani nikiwa nimevalia vizuri sana kwa heshima, tena kwa kujitanda. Nilienda moja kwa moja ofcn kwa mzee Zuberi, nilifika nikaomba kuingia ofcn kwake.
Secretary aliniambia naweza kuingia. Nilingia, ni mtu mzima, nilimsalimia, nilijitambulisha, Na akanisifia sana na kusema dah, umevalia vyema sana, sikuwaza kama wewe ni Charlote, pengine ungesema unaitwa Hidaya… nilicheka na kumueleleza nina shida na kazi. Alishangaa inakuwaje kwa elimu ile sina kazi? Nilimwambia ninafanya kazi ila sipati mshahara mzuri. Nilimdanganya. Aliniambia kwa saa hana nafasi za kazi, ila akaniomba nimpe wakati kisha atanitafutia kazi yeye mwenyewe kwa elimu yangu.
Nilifurahi sana na kuondoka.
Wakti naondoka alinitazama na kuniiita, Charlote,,, niligeuka na kusema abee baba.. Aliniuliza umeolewa? Nilimwambia ndio baba.
Akaniambia, dah,, mumeo ana mke mrembo sana, Nilicheka kwa kujishebedua kisha nikamfinyia jicho na nikatoka. Lengo langu lilishakuwa la kishetani, sikuwa na mswalie Mtume tena, nilishajivika uibilisi, sikwua na huruma hata kidogo.
Nilipokuwa natoka nilipofika reception, Yule dada aliniambia Umeambiwa urudi.
Ni mara ya kwanza tu nimeonana na mzee Zuberi, aliniambia Charlote, naomba kesho ninaenda kwenye mkutano mkoani, tafadhali kama hutajali naomba uongozane na mimi ukafanye kazi zangu. Ukanisaidie kazi. Nilimueleza kwamba atanilipaje maana nina shida na pesa nadaiwa kodi ya nyumba, nilidanganya.
Aliniambia unadaiwa shilingi ngapi? Nilimwambia nadaiwa laki saba na nusu, kodi ya miezi mitatu.
Mzee zuberi alinitazama kisha akaniambia subiri hapa. Alipiga simu accounts na kuitisha pesa hiyo. Mh, sikuamini, nilipatiwa Laki Saba na nusu na kuniambia basi kalipe hizi ili uwe na uhakika usije haribu kazi.
Niliondoka hapo nikiwa na kicheko cha hali ya juu, na kuanza kuona mission zangu zikitiki.
Nilifika nyumbani nikiwa na rah asana, nikachukua balantine yangu na kujidnga kama kawaida.
Mume waangu alirudi na kunikuta niko njwii. Alianza kuongea na mimi, nilimwambia wala usijali mpenzi, ulilianzisha wacha nilimalize, mimi sitafanya umalaya ila nitafanya umalaya na balantine, sitaacha kunywa pombe, ukitaka niache.
Mume wangu alikuwa akiwaza sana na kujuta kunikosea, ila azma yangu ilikuwa kulipiza kisasi.
Asbh nilimuaga nasafiri . Aliniuliza naenda wapi sikumjibu.
Niliondoka nimejiandaa vyema, na kupitia hoteli niliyoambiwa nitafuatwa pale na gari la mr Zuberi. Kweli muda ule nilikuwa nimeshafika pale, na mr zuberi na dereva wake waliwasili.
Tulianza safari nje kidogo ya mji, haikuwa mbali sana ni kama km 60. Na kufikia kwenye hotel ya kifahari, nilifika hapo na Mr Zuberi aliniambia Charlote wewe ni msichana wa kwanza mimi kukutamani tangu nimeoa, na sijui kwa nini umenivutia, ila nakupenda sana tafadhali naomba uwe mpenzi wangu.
Kwangu hii haikuwa na shida kwani ndicho haswa nilitaka.
Sikujali hata kidogo, nilijivunga na kulalamika shida ya maisha, na aliniambia atanisaidia kwa chochote nitakacho. Na akanihakikishia uhakika wa maisha.
Tulilala hotelini hapo siku tatu, kisha siku ya nne tukarudi.
Mume wangu niliporudi aliniuliza nilikuwa wapi, nilimwambia aniache, alishikwa na hasira na kunipiga, nikamwambia umeharibu sana kunipiga, nikaanza kufungasha niondoke.
Alipogusa pochi yangu alikuta pesa taslimu milioni moja na laki mbili, akaniambia pesa hizo nimetoa wapi? Nilimwambia ni zangu na asinibabaishe, alizichukua pesa zile,na kisha kunifungia chumbani kisha kumuita mdhamini wa ndoa yetu na mkewe.
Walikuja na tukakaa kikao. Tuliongea sana na nikasema nilikuwa nimeenda kupumzika kwa hasira, hivyo aniache kwani alikwua na mahusiano na husna. Mume aliomba msamaha sana na kusema anaomba yaishe, na akaomba nifungue simu yangu.
Nilifungua na akanirudishia pesa na kuniambia yaishe , nikamwambia poa. Ila bado nilikuwa na kisasi.
Tuliishi maisha ya mimi kumficha sana mume wangu tabia zangu na hakuwezi kunikamata kabisa.
Mwezi mmoja kabla ya harusi ya Husna, nilihama kwa mzee Zuberi, na sas nilitaka kuwasiliana na Majidi, mpenzi na mchumba wa Husna, hii ilikuwa ngumu kidogo. Kwani Majidi alikuwa ni mfanya biashara na alikuwa na duka kubwa la kuuza tv, simu na vifaa vya umeme, hivyo ningeenda pale ningeonekana. Na pengine Husna angepewa taarifa.
Nilijiuliza nitawezaje kumpata Majidi? Ohoooni rahisi sana. Ni rahisi sana, Niliangalia bango la tangazo la biashara yake, na namba za simu niliziona.
Nilichukua namba za simu na nikasema nitampigia, ila nitamwabia nini? Hiyo ilikuwa juu yangu.
Wakati huu mzee Zuberi alishanieleza kamba binti yake anaolewa siku za usoni. Na nilikuwa namsifia sana na kumwambia una bahati kuozesha binti kwani sio kila mtu anaozesha bintiye.
Na yeye alifurahia sana na kunipenda sana, sikuwa mapepe na alinisifia namna ambavyo namheshimu yeye na mkewe kwani huwa sipigi simu wala kumsumbua kabisa akiwa nyumbani.
Mzee wa watu maskini asijue nini lengo langu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom