Miss Natafuta
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 26,574
- 48,725
Siku moja bwana kuna mkaka mmoja hivi akanitoa out mwaka jana tarehe kama hizihizi aliniambia yupo mjini so twende mahali tukapate dinner na mimi navopenda misosi ningekataa? Basi siku hiyo sikula siku nzima ili usiku huo niweze kufaidi mapochopocho ya hoteli saa kumi na mbili na nusu jamaa akaja home kunifata tukazama zetu kwenye dinner tukafika hoteli tukakaribishwa eneo la kukaa tukakaa muhudumu akaja hapo ndipo fedheha ilipoanzia.
Tulipokaa tu jamaa akawa ameshika simu yake anaongea mara anachati muhudumu akatupa menu. Mimi nikaagiza fasta tu maana hakuna msosi nisioujua, yeye akawa anasema subiri anajishaua huku anachat wakati huo muhudumu kasimama tu hapo maskini baada ya kama dakika tano hivi akasema nilichoagiza mimi wafanye double portion tutakula wote nikaagiza na juice na yeye akaagiza bia yake ila akaendelea tu kuwa busy na simu yake.
Jamaa haongei hadi nimuongeleshe hata nikimuongelesha anasema tu yaa yaa! Yupo busy tu na simu yake. Nikaona isiwe tabu ngoja na mimi nitoe simu yangu kwenye pochi mimi huwa na tabia moja nikiwa na mtu sishikagi simu kabisa tena naitoa na sauti kabisa kwaiyo bwana nikatoa kinokia changu cha tochi, nikadelete sms wee, nikadelete contacts nisizozijua weee, nikacheza gemu ya snake wapi dah, bahati nzuri msosi ukaja tuliagiza nyama ya kondoo.
Tukanawa tukaanza kula jamaa akachukua nyama moja, akawa anakula mimi nikala kama nyama nne hivi nikaona kama jamaa hali tena yupo tu busy na simu nikamuuliza vipi akasema aah mi nipo ok we kula tu unajua kwanza nilikuwa nishakula yaani navopenda kula mimi hamu yote ilijidelete palepale sikula tena.
Nikarudi tena kucheza game yangu ya snake kwenye simu muhudumu alipopita nikamuomba asafishe meza alete na bill jamaa ndo akashtuka eeh mbona umeacha chakula chote nikamuambia am ok nimeshiba, akasema au wakufungie take away nikamwambia hapana labda kama utachukua wewe nae akakataa. Bill ikaja akalipa nikanyanyuka nikamwambia usinirudishe home kuna rafiki yangu nampitia mahali so nitaenda tu mwenyewe.
Akanibembeleza ila nikamshawishi akanielewa nikasepa zangu nikarudi zangu home nikapitia chips mayai mtaani nikafika home nikala nikalala na maisha yakaendelea jamaa namuona tu bado yupo single amepata na ajali kavunjika mguu anataka nikamsalimie eti kila siku ananitumia salamu maana huwa simjibu simu zake kwa heri wala kwa shari kwanza nimestaafu zangu mimi.