Nilitigemea hadi sasa CHADEMA wangekuwa wameshafungua kesi nyingi za kupinga matokea ya ubunge na madiwani

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,699
3,088
Mimi binafsi huwa siwaelewi CHADEMA wanapo lalamika kuhusu upigaji kura na matokeo ya uchaguzi mkuu 2020.

Wao huwa na malalamiko mengi na kudai wana ushahidi lakini cha kushangaza wao ushahidi walionao ni wa kura za Lissu tu ila kuhusu wabunge wao na madiwani wao hawana ushahidi kama waliibiwa kura.

Msitufanye sisi ni mambumbu kama nyinyi kama kweli Lissu angekuwa ameibiwa kura za uraisi basi CHADEMA ingekuwa na wabunge na madiwani wengi kuliko CCM.

Sasa kama wabunge na madiwani wenu wamekubali kuwa wameshindwa kihalali sasa hizo kura za uraisi Lissu atazipata wapi.

Na kama wabunge wenu na madiwani wameibiwa kura na nyinyi wanachama wa CHADEMA mnajua na mnao ushahidi basi wapeni huo ushahidi ili waende mahakamani kupinga matokeo.
 
Siku moja isiyona jina utatamani kufuta huu uzi. Ila kwa ufupi tu tambua hakuna haja yoyote kufungua kesi kwa mazingira ya sasa. Ngoja tuchukulie CCM imeshinda kwa haki kabisa na CHADEMA wameshindwa kihalali sawa boss? Acha maisha yaendelee, maisha sio uchaguzi tu kuna mengi pia ya kufanya
 
Wewe acha kuongea mambo usiyoyajua

Sema kuwa wewe umesikia na unakisema ulicho kisikia

Unafikiri Kawe wameshinda ,unafikiri Kigoma kwa Zitto wameshinda

Kura za Kagera na Mtwara zilifanana kila kitu kwa wwe unavyoona tu hakuna ujanja ujanja

Kura za Kawe jumla za Rais zilikuwa laki 3 alafu jumla za wabunge zilikuwa laki 2 unafikiri watu laki moja hawakumpigia Mbunge?

Chemsha bongo
 
Hujielewi wewe. Kama Tume huru haikuwa huru. Hizo mahakama huru zipo anga gani? Msisitizo sasa hivi ni ICC. Hakukuwepo uchaguzi bali uchafuzi. Mahakama za ndani utapinga uchaguzi ambao haukuwepo. Uliokuwepo ni uchafuzi.
 
Siku moja isiyona jina utatamani kufuta huu uzi. Ila kwa ufupi tu tambua hakuna haja yoyote kufungua kesi kwa mazingira ya sasa. Ngoja tuchukulie CCM imeshinda kwa haki kabisa na Chadema wameshindwa kihalali sawa boss? Acha maisha yaendelee, maisha sio uchaguzi tu kuna mengi pia ya kufanya
🙏🙏
 
Kama hujui ni hujui.

Ili ufungue kesi yenye mashiko lazima uwe na karatasi za matokeo kila kituo yaliyosainiwa, unafikiri mawakala walipewa wote?

Kama wakala alizuiwa au alifukuzwa wakati wa mchakato wa kupiga na kuhesabu kura ambao ndio mashahidi muhimu, Kama huna hivyo vielelezo unashindwa kesi siku ya kwanza.

Wataendaje mahakani pasipo hizo nyaraka.

Kiufupi walijiandaa kwa yote hayo. Uchaguzi imeisha tugange yajayo.
 
Wewe ni mpuuzi tu. Mahakama zipi ?!. Vyombo gani vya dola na vya maamuzi ?!.

After all jukumu la kuweka ground play ya siasa si ya CHADEMA tu . Kama wewe huwezi kuona taratibu zinazotumika kusimika watu madarakani kama zina kasoro bali unaiona kasoro ya CHADEMA !!!.

Huna msaada na nchi hi
 
Kesi ya ngedere kuiba mahindi unawapelekea nyani na kima wawe waamuzi.😆

Ajabu la 9 la dunia!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Hata wewe unaruhusiwa kwenda kufungua kesi kwa niaba ya chadema. Kumbuka hata kesi za kutaka muda wa uraisi kuongezwa zimefunguliwa na mtu wa kawaida yaani asiye na maslahi ya moja kwa moja na uraisi. Hivyo hata wewe ruksa kwenda kufungua kesi
 
Wanaojua ni waliohesabu, wewe umesikia kama wengine, kauli zilizotamkwa kabla, na matendo, ndo watu wanaonganisha dot, ila uchaguzi umeisha tufanyeni kazi
 
Almost comments zote ni za kulalamika tu na kusurrender.

Yaani watu wamekata tamaa na mbele hakuonekani. We are doomed!
 
Haiwezekani mtu akaenda kufungua kesi ya kupinga uchaguzi ambao haukuwepo. Uchaguzi ni haukuwepo sasa ukisema unaenda kupinga matokeo maanayake unakubaliana na kilichotokea kuwa kilikuwa uchaguzi wakati kiuhalisia hakikuwa uchaguzi. Na kama watu tuliowaamini wameona ni sawa kwa yaliyofanyika basi kama taifa tuna safari ndefu sana kufikia mafanikio ya Kweli.
 
Haiwezekani mtu akaenda kufungua kesi ya kupinga uchaguzi ambao haukuwepo. Uchaguzi ni haukuwepo sasa ukisema unaenda kupinga matokeo maanayake unakubaliana na kilichotokea kuwa kilikuwa uchaguzi wakati kiuhalisia hakikuwa uchaguzi. Na kama watu tuliowaamini wameona ni sawa kwa yaliyofanyika basi kama taifa tuna safari ndefu sana kufikia mafanikio ya Kweli.
Uchaguzi haukuwepo wakati Lisu alizunguka Tanzania nzima na kutaja tarehe ya uchaguzi akiwaomba wananchi wampigie kura ?

Mmeishiwa hoja tu hamuna ushahidi wowote unaoweza kukubebeni mahakamani ndio maana mnaleta visingizio tu
 
Uchaguzi haukuwepo wakati Lisu alizunguka Tanzania nzima na kutaja tarehe ya uchaguzi akiwaomba wananchi wampigie kura ?

Mmeishiwa hoja tu hamuna ushahidi wowote unaoweza kukubebeni mahakamani ndio maana mnaleta visingizio tu
ndiyo.maaana.mmeambiwa.mmeshinda kwa.haki ongozeni sasa tuone maendeleo,CCM si.inakubalika.sana na WAPINZANI wanachelewesha maendeleo,sasa kuna haja gani ya kuwaambia watu wakafungue KESI,je wakishinda si wataenda bungeni kupinga.maendeleo.

Sent from my SM-A9000 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom