Nilitemwa uspika kwa hila za vigogo-sitta

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
Sitta: Nilitemwa uspika kwa hila za vigogo Send to a friend Sunday, 19 December 2010 21:27 0diggsdigg

kiliositta.jpg
Mr Samwel Sitta

Tausi Mbowe
WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta jana alitoa kauli nyingine inayoweza kukitikisa chama chake cha CCM baada ya kueleza kuwa aliondolewa kwenye kinyang'anyiro cha kiti cha spika wa Bunge la Muungano kutokana na hila za viongozi ambao walishindwa kuhimili kasi ya utendaji wake kwenye chombo hicho cha kutunga sheria.

Jana, Sitta ambaye alikuwa akihojiwa na Mwananchi, alisema utendaji wake wa kasi na viwango uliwatisha viongozi wengi wa serikali na ndio maana wakaamua kutumia kigezo cha jinsia kumwondoa.

"Unajua nataka hili ilieleweke; juzi nilienda jimboni kwangu Urambo Mashariki nikawaeleza wapiga kura wangu kwa nini sasa mimi sio spika tena, maana wanaweza kudanganywa kama kazi imenishinda au nimefukuzwa," alisema Sitta.
"Watanzania lazima wajue mimi sijafukuzwa kazi wala sijashindwa kufanya kazi hiyo, ila kuna viongozi ambao ni wakuu wangu ndani ya chama chetu ambao wameshindwa kuendana na kasi na viwango vyangu ndio maana wakaamua kuweka sharti ambalo kamwe nisingeweza kulitimiza.

"Kigezo hicho cha jinsia walikileta katika hatua za mwisho za mchakato wa kumtafuta spika wakijua kwamba sitaweza kukitimiza na ningejua hilo mapema, nisingepeleka jina langu kuomba kuteuliwa tena."
Sitta alisema ni wazi kamba asingeweza kutimiza sharti kwamba spika aliyetakiwa safari hii ni mwanamke ndio maana hakuweza kuteuliwa tena kuwania nafsi hiyo.

"Mimi ni Sitta na nitabaki kuwa Sitita yule yule kama nilivyozaliwa na kwa vyovyote vile; nisingeweza kufanya chochote ili kuhakikisha sharti hilo nalitimiza," alisema Sitta.
Hata hivyo Sitta alisema kuwa endapo jina lake lingepitishwa, alikuwa na ukakika wa kurudi katika kiti hicho kwa kuwa asilimia kubwa ya wabunge walikuwa wameukubali utendaji wake.

"Nawaahidi Watanzania huu sio mwisho wa utendaji wangu wa kazi sasa kasi na viwango navihamishia katika Wizara hii muhimu na kwamba wananchi wasiogope tena Tanzania kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki,"alisema.
Alisema akiwa Waziri wa Afrika Mashariki atahakikisha Watanzania wanafaidika na shirikisho hilo na kwamba suala la ardhi halitakuwepo kwa kuwa tahadhari zote zimechukuliwa.

Sitta alifanya ziara kwenye jimbo lake la Urambo Mashariki ambako pamoja na mambo mengine, alihudhuria mkutano wa uchaguzi wa mwenyekiti wa halmshauri ya Urambo.
 
Hiyo iko wazi mzee SIX,
Mpango mzima ilikuwa kumuweka Chenge ili atetee mafisadi ila akachemka kuongelea ishu ya rada mapema kuwa yuko safi.
Balozi wa Uingereza baada ya kutoa Tamko la kupinga kauli ya Chenge ndipo ghafla upepo wa kuweka Mwanamke uligeuka.
Kama wangekuwa wanataka mwanamke kwa nini hawakusrema mapema naamini kuna wanawake wengi wangeomba uspika kama Mh. MANYANYA
 
Hapo kwenye red. Unasema Manyanya yupi. Si ndiye yule aliyetoa hoja bungeni kwaba CHADEMA hawamtabui rais hivyo hawawezi kuruhusiwa kugombea unaibu spika. Si nidye huyu Tundu Lissu alipoingilia swali hili Anne Makinda akashindwa hoja na kuisha kusema Tundu anaingilia mawazo ya Manyanya.

Kuweni na kumbukumbu na si kuishia kukumbuka ushiriki wa kamati teule ya RICHMOND.
 
Thanks Subiri jibu,

Kumbe naye ni Kimeo.
Yaani CCM vimejaa vimeo Tupu.
 
Ni kweli kabisa, jamaa walishindwa speed and standards za mzee Six.
 
6 hauwezi kukata tawi ulilokalia.kama kweli una uchungu na nchi jiunge CHADEMA ili uvishwe miwani.utaona mbali ya hapo!
 
Ujkomage na uendelea kuwa vuguvugu UTATEMWA HATA NA MUNGU MWENYEWE
 
Hakika Samwel Sita hana Tofauti na Zitto Kabwe! Mambo ya ndani yeye anawahi vyombo vya habari, hana lolote huyu anataka sympathy ya wananchi. Kwani alizaliwa awe spika? Anazeeka vibaya
 
Mwenzake hosea kwenye cable za wikileaks anasema hawezi kulinda maslahi ya nchi kwani uhai wake utakuwa hatarini hivyo anatumia PCCB kulinda "big fish" wachache kama alivyosema ili aishi kwa raha duniani.

Sasa si aijuzulu ili wananchi tujue anasimamia wapi. Mambo ya kuuma huku unapuliza tunaanza kuyashtukia.
 
Six nahisi anatafuta popularity kwa style hii ya kuropoka wakati yeye si msemaji.
Mbona alipewa ushauri kwamba hata wakitaka kumteua uwaziri akatae na hakufanya hivyo?
Six hana lolote ni njaa tu, hawezi kujiweka pembeni na kujifanya msafi wakati mchafu.
Kama yeye jasiri basi ajiuzulu uwaziri, nakujiondoa chamani. Shame on you Six.
 
Hana lolote, huwezi kukaa na wasafi ikiwa wewe ni mchafu. CCM ni wasafi kwelikweli sasa kama anataka kuwa mchafu atoke ccm, ili aingie kwa wakombozi wa kweli sio unafiki na 2015 asijisumbue kuchukua fomu ya urais
 
si angefanya plastic surgery tu
"Kigezo hicho cha jinsia walikileta katika hatua za mwisho za mchakato wa kumtafuta spika wakijua kwamba sitaweza kukitimiza na ningejua hilo mapema, nisingepeleka jina langu kuomba kuteuliwa tena."
Sitta alisema ni wazi kamba asingeweza kutimiza sharti kwamba spika aliyetakiwa safari hii ni mwanamke ndio maana hakuweza kuteuliwa tena kuwania nafsi hiyo.

"Mimi ni Sitta na nitabaki kuwa Sitita yule yule kama nilivyozaliwa na kwa vyovyote vile; nisingeweza kufanya chochote ili kuhakikisha sharti hilo nalitimiza," alisema Sitta.
Hata hivyo Sitta alisema kuwa endapo jina lake lingepitishwa, alikuwa na ukakika wa kurudi katika kiti hicho kwa kuwa asilimia kubwa ya wabunge walikuwa wameukubali utendaji wake.
 
Mzee Sita hakukataa kuteuliwa uwaziri wa Jumuia,labda anataka kupeleka mapambano akiwa ndani ya Cabinet.
 
Hapo kwenye red. Unasema Manyanya yupi. Si ndiye yule aliyetoa hoja bungeni kwaba CHADEMA hawamtabui rais hivyo hawawezi kuruhusiwa kugombea unaibu spika. Si nidye huyu Tundu Lissu alipoingilia swali hili Anne Makinda akashindwa hoja na kuisha kusema Tundu anaingilia mawazo ya Manyanya.

Kuweni na kumbukumbu na si kuishia kukumbuka ushiriki wa kamati teule ya RICHMOND.
Subirijibu we ni full brain <it means high thinking capacity> Thank u and God bless u.
 
Hakika Samwel Sita hana Tofauti na Zitto Kabwe! Mambo ya ndani yeye anawahi vyombo vya habari, hana lolote huyu anataka sympathy ya wananchi. Kwani alizaliwa awe spika? Anazeeka vibaya

we umeoza sana[your brain is resting]
 
Mwenzake hosea kwenye cable za wikileaks anasema hawezi kulinda maslahi ya nchi kwani uhai wake utakuwa hatarini hivyo anatumia PCCB kulinda "big fish" wachache kama alivyosema ili aishi kwa raha duniani.

Sasa si aijuzulu ili wananchi tujue anasimamia wapi. Mambo ya kuuma huku unapuliza tunaanza kuyashtukia.

Hosea ni nyani huyo na hana utashi mkuu uko sahihi sana
 
Back
Top Bottom