Nilitegemea watalamu wetu kumuepusha Rais na aibu inayoweza kumkuta au hasara ya fidia

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,491
2,355
Awamu hii imekuwa na maamuzi mengi ya harakaharaka hali ambayo inaweza kumuabisha Rais wetu au kuliingizia Taifa hasara kubwa sana. Naamini nia ya Rais ni njema ila napata mashaka sana na wataalamu wetu wanaompelekea taarifa, kuna wakati nahisi wanapeleka taarifa ambazo hawajazifanyia utafiti wa kina, au wanapeleka kwa lengo la kujipendekeza
 

Attachments

  • 13218933_245564115799617_1145413387_n.mp4
    3.8 MB · Views: 38
Labda wanataka turudi kwenye RTC (regional trading company) maana kipindi kile cha ujamaa wananchi walikuwa wanapimiwa kiasi cha kilo za kununua kwa kuwa haikuwa soko huria, mimi nafikiri na ninaamini wao wangejikita kukusanya kodi huku wanaendelea kuboresha viwanda vyetu vya sukari
 
Kuna ushauri wa aina mbili. Kwanza ushauri huru ambao mshauriwa anaweza kuupokea na kuutekeleza hata kama ushauri huo unakwenda kinyume na imani, mategemeo, mila desturi, na msimamo aliojiwekea. Ushauri wa aina hii ni kama dawa ya daktari; mgonjwa uipokea na kuimeza akiamini uwezo wa dawa hiyo kumponya lakini pia akiamini kwamba lengo la daktari ni kumtaka apone hata kama dawa hiyo ni chungu. Ushauri wa aina ya pili ni wa kuridhisha au kukidhi imani, mila desturi, mategemeo na msimamo wa mshauriwa. Kwenye aina hii ya ushauri mshauri kwanza anafanya utafiti wa imani, mategemeo na msimamo wa mshauriwa. Kadhalika mshauriwa utafuta washauri wanaoweza kuleta ushauri ule ambao tu unakidhi imani, mategemeo, na msimamo wake. Wanaofuata ushauri wa aina ya pili mara nyingi ni madikteta!
 
Kwani kabla hajaibuka huko alikoibuka na kutoa amri aliwaomba ushauri? Hakuna kuhamisha Lawama.Aliyetoa Amri ndiye chanzo cha yote haya
 
Back
Top Bottom