Nilitegemea Ruzuku ya vyama Kufutwa kwenye Bajeti 2017/18

Mkuu MACCM wanachama wao hawatoi ada za kila mwaka. Hivyo ruzuku tu haitoshi inabidi wachote pia toka hazina, lakini sitashangaa hili likitokea ili wavimalize vyama vya upinzani na wenyewe wakiendelea kuchota hazina. Jitihada zao nyingine za kuviua vyama vya upinzani hazijafanikiwa.
Miaka 20 chama kinapata ruzuku na hakijafanya chochote cha maana kwanini waendelee kupewa ruzuku. Hata kujenga ofisi tu imewashinda wakati wakuu wanakula bata kwenye apatmenti za mamilioni kwa mwezi
 
Kikwazo cha kufuta ruzuku kama kilivyo kikwazo cha kuleta maendeleo ni wabunge wa CCM waliokwenda bungeni kwa ajili ya ruzuku ili waweze kufidia fedha wanazotoa rushwa kwa wapiga kura.
 
mkuu mbona hajatajwa jina??

wenyeviti wako wengi sana, huyo wako unayemtetea ni nani?

mtajeeeeeeee
Sawa hajatajwa ila wenyeviti wote wanajiweza
1.mbatia ana masters ya engineering
2. Mbowe mfanyabiashara mkubwa
3. Mghwira ana masters ya sheria na professional consultant
4 zitto naye ni consultant mwenye utajiri mkubwa
5. Lipumba naye professional consultant wa uchumi mwenye maeneo ya kupata pesa mengi tu hasa kufundisha

Sasa ni nani kati yao hapo ni kapuku kiasi kwamba hawezi survive nje ya siasa?? Embu acheni kudhalilisha watu.... kma hao hapo juu wanauwezo wa kuingiza si chini ya dollar 10,000 kwa mwezi kivp wahangaike na karuzuku kanakoishia tu kulipa mishahara na kodi ya pango??? Na ukumbuke walijiunga na vyama hivo hata wakati havina mbunge wala diwani hivyo hawapato ruzuku ila walidumu ssa kivp leo muone wanataka ruzuku tu?? Si wangekuwa wamebaki ccm???
 
Mifuko ya wachache??? Ndio alivyosema hivyo CAG??? na kma CAG alikagua vyama vya siasa na akakuta pesa zinafujwa alitoa mapendekezo gani?? Embu tuanzie hapo kwanza maana naona unaleta sababu za kufikirika na solution za kufikirika pia
Nipe maoni yako hivi vyama vya siasa siasa vinafaidikaje kwa hiyo ruzuku.
Mfano kuna chama hata makao makuu ya ofisi imeshindwa kujenga, huko mikoani ofisi nyingi zimefungwa kwa kushindwa kulipa kodi. Tuache ushabiki wa kisiasa let's face reality
 
Nipe maoni yako hivi vyama vya siasa siasa vinafaidikaje kwa hiyo ruzuku.
Mfano kuna chama hata makao makuu ya ofisi imeshindwa kujenga, huko mikoani ofisi nyingi zimefungwa kwa kushindwa kulipa kodi. Tuache ushabiki wa kisiasa let's face reality
Ruzuku kazi yake ni kufund shughuli mbalimbali za kichama kuanzia mikutano ya ndani...... ziara za viongozi..... kampeni za chaguzi.....allowance za wafanyakazi wa chama.....sasa hayo yote chadema hakifanyi???? Au unafkiri ruzuku inakuwa more than demands???

Kwa issue ya Ofisi wamenunua mbona.... lile jengo sio la kupanga wamenunua sasa kuna tofauti gani ya kujenga!!! Labda useme sio la hadhi ya ila kma jengo for the sake of jengo lile limenunuliwa hivyo si kweli hatuna ofisi

Ila kwa upande mwingine kma hoja yako ni sahihi kwa basi shida inakuwa kwenye vipaumbele mfano kufanya operation ya chama mfano operation pamoja daima ilicost bilion 2!!! Pia kampeni kma za udiwani ilitumika bilion 1 kwa sababu ya kutumika kwa usafiri wa helikopta na kuwatumia viongozi wengi kwenda kila pembe ya nchi!! Hivyo hapa challenge ipo kubwa sana!!!

Naamini wakiweka vipaumbele vzuri kwa mbele hata wwe utaona faida ya ruzuku mfano kuchangia ofisi za mikoani, kuchangia shughuli za jamii kma mikopo ya elimu ya juu kwa wliokosa, madawati,madawa n.k yote hayo yatajustify matumizi mazuri ya ruzuku na pesa za chama kutoka source mbalimbali
 
Vyama vya siasa navyo vianze utaratibu wa kujitegemea na kuanzisha miradi yao, kwan kwa ruzuku toka serikalini imekuwa chanzo cha migogoro ya baadhi ya vyama vya siasa. Inatumika vibaya kwa kuwanufaisha wachache na sio wanachama.
 
CCM ina vitega uchumi vingi pia wafadhiri tatizo chama cha washika ukuta kutakuwa ndiyo kimefikia mwisho.
Madini ya watanzania ndio vitega uchumi wa CCM???Hao wafadhili wapo wapi kumlipa shugongo na wale wafanya kazi wa redio uhuru??
 
Mkuu tatizo wanachama hawaonii benefits za hizo ruzuku. Mfano maofisi mengi ya baadhi ya vyama vya siasa vimeshindwa kulipia kodi. Vyama haviwi wazi kwa wanachama wao kwa mapato/matumizi transparency.
Vyama huwa vinakaguliwa matumizi yake na CAG,kwa maana hiyo unasema CAG sio competent kujua hayo na haoni ila wewe ndio unaona???
Je,wewe ni member wa mkutano wowote wa vyama vya siasa?Umewahi kuuliza hilo kwenye vikao husika?Au unataka wakuwekee magazetini matumizi yao?
 
Napongeza sana kwa bajeti nzuri ya serikali ya 2017/18.
Nilitegemea serikali ingefutaa ruzuku inayotolewa kwenye vyama vya siasa ili vyama hivi vitegemee michango ya wanachama wake. Ukichunguza sehemu kubwa ya pesa hizi za ruzuku huwa zinaingia kwenye mifuko ya viongozi wachache wa vyama hivi. Ruzuku pia huwa ndio chanzo cha migogoro ya baadhi ya vyama vya siasa.

You can't bite the finger with which your mother fed you......in Achebe's voice
 
Ruzuku ikifutwa hakuna CUF ya Lipumba wala CUF ya Seif
 
Back
Top Bottom