Nilitegemea kuziona CPA ( T ) na ACCA zikitufafanulia utata wa 1.5T kabla ya Polepole kuja kuokoa Jahazi

Kama majibu ya polex2 na taarifa ya serikali ndio hayo na ni sahihi!? Basi CAG na team yake ni vilaza wa ajabu hawakuweza kuelewa mapema !? Vinginevyo mnawafanya Watanzania ni wajinga sana!!!! Kibaya zaidi taarifa rasmi imetolewa Bungeni
! IPO siku Bunge litakuwa na uzalendo watawahukumu kwa kudanganya!
Swali kubwa nani anathibitisha entry hizo za kubalance 1.5T mnataja tu kubalance figure,mnatufanya malofa sana
 
Hii IPSAS accrual imewaingiza wengi kwenye Chaka. CAG mwenyewe na watu wake pia wamejichanganya sana hasa kwenye suala la consolidation. Kama suala ni interpretation ilikuwa wafanye adjustment mambo yaishe lakini CAG naye kaingia chaka!
Pole sana chaka umejiingiza wewe kwa kukosa weledi wa kuelewa hili eneo la ukaguzi kwa upande wa kanuni na taratibu zake ...

Hivi Bro! unamjua vizuri Prof. Assad au umeamua tu kujifurahisha nafsi kwa kujiona eti umetambua na kung'amua vizuri mpaka umegundua kua SI.EI.Jii nae kaingia chaka kwa kile ulichokiita "IPSAS accrual"

Watu mna jichanganya sana, hapa issue sio basis gani inatumika kutunza hesabu whether it is Cash or Accrual basis, kila muamala lazima uwe na support document pia na Muhtasari wa kuruhusu muamala huo kwa maofisa husika basing on budget perimiters ...

Now Cash or Accrual Basis inahusika vipi na muamala kufanywa bila supporting documents?

Whether umetumia Cash or Accrual Basis lazima muamala wowote utakaofanyika uwe na supporting document ili kuonyesha kua pesa husika imetumikaje, imetumika lini, kununua Nini, kwa ajili ya Nini ...

Sasa iwe ni hati fungani iliyoiva, au ambayo bado mbichi lazima tuone ushahidi wa voucher iliyotumika kulipia voucher ya ugavi wa matumizi husika ...

Issue nikua SIEIJii kashindwa kujua 1.5 trln ilipo kwa sababu haikuonyesha zimetumika vipi hana uthibitisho kua pesa hiyo imetumikaje ...

Sasa Hili swala la basis watu ndio mnafanya uchochoro wa kujitetea, this has nothing to do with voucher verification jamani acheni kufuata akili za Pole Pole mnapotezwa nanyie mnapotea you guys wake up ...

Let us not pretend kua tunaelewa taaluma wakati hakuna kitu, hivi kweli SIEIJii umeshindwa kumuelewa kuhusu 1.5 trln halafu eti umemuelewa Pole Pole you guys are not serious. Pole Pole mwenyewe hajielewi atawezaje kuwaelewesha ...

Hivi huyu Pole Pole ndio ataweza kukuelewesha zilipo 1.5 trln kuliko Prof. Assad na ukaelewa ... !!!
 
Binafsi nilitegemea ilipotoka tu taarifa ya Zitto ambaye kitaaluma ni mchumi kuhusu utata wa 1.5T katika ripoti ya CAG basi wataalamu wa fedha na uhasibu wangemiminika kutoa ufafanuzi. Haikuwa hivyo na badala yake akaibuka mwanaharakati Kafulila ambaye badala ya kufafanua yeye akazidisha utata.

Wakati taharuki ikiongezeka katika mitandao kwa bahati njema akatokea mwenezi wa CCM ndugu Polepole na kutengua utata uliokuwepo. Na kwa bahati njema zaidi ufafanuzi kama ule wa Polepole kesho yake ukatolewa bungeni ikiwa ni taarifa ya serikali.

Ndiposa nauliza taifa bado lina wahasibu wale wa kwa Musasira au wamebadili field na kujiunga na taaluma nyingine.

Wale wahasibu wa zamani wa Naboce na NAD wangelikwishajitokeza mapema na kusema " .....hakuna utata wowote Zitto anatafsiri kwa Cash basis wakati serikali inatumia mfumo wa Accrual basis"....... Niishie hapo!
Umeamua kuokoka?

Ubarikiwe sana
 
Huo mfumo mpya wa 'accrual' inaelekea uliwachanganya hata hao wahasibu wa CAG katika ukaguzi wao na hivyo kuyaacha mahesabu hajabalance kwenye ripoti yao ya ukaguzi na kutoa mwanya kwa akina Zitto kupata kiki ya kisiasa kama kawaida yao.
 
kinachochanganya, hata zikijulikana zilifanyiwa nini CAG atazikagua tena kama zilitumika itakikanavyo ama? hapo lazima mechi ihairishwe
 
Huo mfumo mpya wa 'accrual' inaelekea uliwachanganya hata hao wahasibu wa CAG katika ukaguzi wao na hivyo kuyaacha mahesabu hajabalance kwenye ripoti yao ya ukaguzi na kutoa mwanya kwa akina Zitto kupata kiki ya kisiasa kama kawaida yao.

What are you trying to say?!

The cash received from Zanzibar of 200 bl Tzshs was that an accrual income? !

Now in their government defence, that cash(NOT ACCRUAL income) 200bl be precise was taken out or reversed from the initial total revenue for the period reported in the CAG report, as per government statement .

Let me tell you something it is really unfeasible and not widely used accounting preparation method using a cash basis! Therefore 99%, I repeat 99% of government and its affiliate entities around the world including Tanzania use “accrual concept” in preparation of its account, therefore recording the transactions in a correct period when its due, therefore in CAG report dealing with the accounts 12 months up to June 2017.

“Cash basis” is mainly used in preparation of going concern Accounts, the company about to be going burst, bankruptcy or sometime used on NGO or charitable organisation, therefore in organisation or government for this matter which its affair is facing uncertainty dooms days if you like!

The question!, is this government considered as a “going concern” entity. ? Never heard of any government around the world in that position to consider preparing their accounts on “cash basis”

After all based on Pole Pole and waziri statement, the government is also suggesting CAG don’t understand the difference between receivables and cash receipts, therefore render him incompetent!

This is what they are trying to say to wananchi at the same time pausing a question, As regard to this 200bls, how can you report the unreported if the report is already showing that income already included in the report as being reported by the government and willingly submitted to CAG,

In other words they try to confuse you not to understand the confusion,!

You are being duped!
 
Komredi Polepole kafafanua kwa urahisi mpaka wakulima na wafugaji huku vijijini wamemuelewa.

Mi sijamuelewa kabs yani sijaona hata kitabu cha book-keeping frank hood jmn bado ajanisaidia kwa hesabu alizo piga pole pole na report zimenifanya nicheke na kuuliza kwa lugha nyingine kilo moja na nusu(1.5kg) za mchele kitumbo ziko wp mtujuze jmn
 
Binafsi nilitegemea ilipotoka tu taarifa ya Zitto ambaye kitaaluma ni mchumi kuhusu utata wa 1.5T katika ripoti ya CAG basi wataalamu wa fedha na uhasibu wangemiminika kutoa ufafanuzi. Haikuwa hivyo na badala yake akaibuka mwanaharakati Kafulila ambaye badala ya kufafanua yeye akazidisha utata.

Wakati taharuki ikiongezeka katika mitandao kwa bahati njema akatokea mwenezi wa CCM ndugu Polepole na kutengua utata uliokuwepo. Na kwa bahati njema zaidi ufafanuzi kama ule wa Polepole kesho yake ukatolewa bungeni ikiwa ni taarifa ya serikali.

Ndiposa nauliza taifa bado lina wahasibu wale wa kwa Musasira au wamebadili field na kujiunga na taaluma nyingine.

Wale wahasibu wa zamani wa Naboce na NAD wangelikwishajitokeza mapema na kusema " .....hakuna utata wowote Zitto anatafsiri kwa Cash basis wakati serikali inatumia mfumo wa Accrual basis"....... Niishie hapo!

Hii ndiyo shida ya nchi yetu,hatuna profffesional volunteers kutueleza ukweli...
Basi tuna yumbishwa huku na kule
 
Hii IPSAS accrual imewaingiza wengi kwenye Chaka. CAG mwenyewe na watu wake pia wamejichanganya sana hasa kwenye suala la consolidation. Kama suala ni interpretation ilikuwa wafanye adjustment mambo yaishe lakini CAG naye kaingia chaka!
Consolidation ya nini?
 
Huo mfumo mpya wa 'accrual' inaelekea uliwachanganya hata hao wahasibu wa CAG katika ukaguzi wao na hivyo kuyaacha mahesabu hajabalance kwenye ripoti yao ya ukaguzi na kutoa mwanya kwa akina Zitto kupata kiki ya kisiasa kama kawaida yao.
Accrual ni mfumo mpya?hahah polepole kweli amekamata vichwa kama hivi aisee.
 
Binafsi nilitegemea ilipotoka tu taarifa ya Zitto ambaye kitaaluma ni mchumi kuhusu utata wa 1.5T katika ripoti ya CAG basi wataalamu wa fedha na uhasibu wangemiminika kutoa ufafanuzi. Haikuwa hivyo na badala yake akaibuka mwanaharakati Kafulila ambaye badala ya kufafanua yeye akazidisha utata.

Wakati taharuki ikiongezeka katika mitandao kwa bahati njema akatokea mwenezi wa CCM ndugu Polepole na kutengua utata uliokuwepo. Na kwa bahati njema zaidi ufafanuzi kama ule wa Polepole kesho yake ukatolewa bungeni ikiwa ni taarifa ya serikali.

Ndiposa nauliza taifa bado lina wahasibu wale wa kwa Musasira au wamebadili field na kujiunga na taaluma nyingine.

Wale wahasibu wa zamani wa Naboce na NAD wangelikwishajitokeza mapema na kusema " .....hakuna utata wowote Zitto anatafsiri kwa Cash basis wakati serikali inatumia mfumo wa Accrual basis"....... Niishie hapo!

Aisee kweli mkuu,una mawazo kama yangu,kuna group moja huko whatsapp limejaa ma CPA holder wao nao wamekaa kujadili alichosema polepole!
 
Aisee kweli mkuu,una mawazo kama yangu,kuna group moja huko whatsapp limejaa ma CPA holder wao nao wamekaa kujadili alichosema polepole!
Mimi nimembana mmoja mbona kanielezea vuzurii tuuu sema mambo kama haya watu wengi tunayaweka kisiasa zaidi japo ipo lakini tuwe tunauliza kwanza wataalamu wa mambo ya fedha,kikubwa ni hela haikuidhinishwa matumizi yake na hayaonekani,sasa wahusika kazi yao ni kuelezea hiyo hela iko wapi au kama imetumika imetumika kwenye mambo gan watu hawataki kusikia propaganda nyingi tunataka uhalisia wa kitu usemwe basi matumizi kama hayakuonekana kwenye ukaguzi je hiyo hela imeenda wapi na kwenye matumizi bunge halijaidhinisha..
 
nani ajitokeze wakati mgogo mwenyewe hajiwezi kwa pombe ..
hata lile gongo analopigia watu linamshinda siku hizi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom