Nilitegemea hotuba za wastaafu zijikite kujisahihisha kwa nini waliua na kugawa kwa wahindi TTCL, ATCL, NBC, TRL, watueleze kiini cha ESCROW, KAGODA

Badala ya kujikita kwenye hoja fikirishi na nzito wao wanazama kwenye unyenyekevu na kujishusha!.

Wanazama kwenye mipasho ya kwenye kanga badala ya kuongea vitu vya kizalendo, Nyerere alikuwa mnyenyekevu lakini alijaliwa uwezo wa kuwa na msimamo thabiti usiyoyumbishwa.

Nyerere alikuwa anapenda kusikiliza ujenzi wa hoja zenye mantiki, lakini hakukubaliana na majungu ya makundi ndani ya chama.


Nyerere kama akiinuka leo kutoka kaburini atakaowashangaa ni wengi tu ambao wamo ndani ya ukumbi na kujadili mchango wake kwa taifa hili.
Toa mfano wa hoja fikirishi hapa ambayo wewe umewahi kutoa..vinginevyo itakuwa ni walewale wakosoaji wasiotoa mwelekeo wa kufanya baada ya kukosoa.
 
Wastaafu wanaposimama wasitueleze mambo mepesi mepesi ya kitoto kama historia ya nyerere hata kwenye vitabu waeleze makaripio ya Nyerere kuhusu Rushwa waeleze kiini cha mikataba ya kimangugo kwenye mashirika na rasilimali za nchi yetu watueleze ACCACIA ni nani na nan alinufaika na ACCACIA
kama hao jamaa walifanya uhalifu wote huu, na awamu hii imejipambanua katika kutokuheshimu katiba ikiwemo kuondoa kinga kwa walengwa.... je inasubiri nini kuwasweka ndani hawa wahalifu?

halafu awamu hii ikumbuke tunadai 1.5tr zetu fasta!!
 
Toa mfano wa hoja fikirishi hapa ambayo wewe umewahi kutoa..vinginevyo itakuwa ni walewale wakosoaji wasiotoa mwelekeo wa kufanya baada ya kukosoa.
Matatizo yapi yaliua viwanda vyote alivyojenga Mwalimu Nyerere miaka yake 23 ya uongozi, ambayo yanawez kuchangia kufa kwa viwand vinavyojengwa katika awamu hii?.

Ni namna gani urasimu wa mawizarani na katika taasisi za kiserikali unavyokwamisha nia mbalimbali za uwekezaji za wawekezaji wa ndani ya wa nje?.

Ujamaa unamaanisha ukubwa wa serikali kwa maana ya serikali kutaka kuhudumia elimu za wanafunzi na afya kinamama, je pato la taifa linayo misingi endelevu ya inayoiwezesha serikali kuuishi ujamaa wa Mwalimu Nyerere?.

Yapo mengi tu yenye kuhitaji tafakuri za kina, kwani nyakati za Mwalimu na za sasa zina mengi yasiyokwenda sambamba.
 
Waliobinafsisha mashirika ya umma hawakufanya hivyo kwa lengo kuhujumu taifa hata kama walipata maslahi binafsi kupitia ubinafsishaji huo.

Mashirika ya umma yalikuwa "mahututi" chini ya uendeshaji wa kizembe/kifisadi wa watendaji wa serikali. Bali maamuzi ya kubinafsisha ndo njia pekee iliyodhaniwa ingeokoa tija ya mashirika hayo.

Jambo la msingi lakujifunza ni kwamba uchumi wa nchi chini ya utawala wa hao "wastaafu" uliendelea kukuwa kila mwaka labda kutokana na ubinafsishaji wa mashirika hayo. Tofauti na utawala wa sasa ambao unatekeleza itikadi za utaifishaji wa shughuli za kiuchumi bado tunashuhudia kusinyaa kwa uchumi wa nchi chini ya asilimia 6.
 
Wala hajamsema Magufuli, Magufuli yuko zake busy kutatua kero za wanyonge

KUTATUA KERO KWA

Wasio wanaccm wakawaambie Waume zao, Madiwani wao na Wabunge wao.

Kwa Mwanaccm RPC na DC walipe 25,000,000/= ndani ya siku tano (5).

HAPO KUTAKUWA NA UZALENDO, UMOJA, UPENDO NA AMANI?

TARAJIA MTIFUANO TU.
 
Wastaafu wanaposimama wasitueleze mambo mepesi mepesi ya kitoto kama historia ya nyerere hata kwenye vitabu waeleze makaripio ya Nyerere kuhusu Rushwa waeleze kiini cha mikataba ya kimangugo kwenye mashirika na rasilimali za nchi yetu watueleze ACCACIA ni nani na nan alinufaika na ACCACIA
Tusijisahaulishe hata Mwalimu (hata alibatizwa jina - baba:haambiliki):pamoja na mema yake pia mapambio na sifa tunazompa alijenga matabaka ya "hawa sio wenzetu..." pale alipokosolewa na kutokana na makosa hayo aliiacha nchi taabani bin hoi hata bidhaa za matumizi ya kawaida zikaitwa BIDHAA ADIMU!!! Watu wakafulia majani ya papai na kujipaka sabuni.... ikawa hata hayo maduka ya RTC ukinunua sukari wanakupa na bakuli za bati!!! Watu walivaa magunia na wengine kwenda uchi wa mtu!!! Mpaka SAS aliporuhusu mitumba ambayo mzee alikuwa haitaki wakati viwanda vyetu (alivyonyang'anya kwa jina la kuwataifisha makabaila) alivyovilinda kufeli kabisa. Leo yooote hayo watu tumesahau kuwa ni damu ileile ya ukoo uleule tutarajie mabadiliko??? Tuna nadharia nyingi na kujisahaulisha kwingi...
Labda itokee miujiza...
Mwalimu baada ya kuwa nje madaraka na kuiona hali halisi aliandika " TUJISAHIHISHE...
 
Wastaafu wanaposimama wasitueleze mambo mepesi mepesi ya kitoto kama historia ya nyerere hata kwenye vitabu waeleze makaripio ya Nyerere kuhusu Rushwa waeleze kiini cha mikataba ya kimangugo kwenye mashirika na rasilimali za nchi yetu watueleze ACCACIA ni nani na nan alinufaika na ACCACIA
Wanaona watajivua nguo mkuu,ndio maana wako kimya.Katika kitabu cha Mkapa ambacho anajitambia kweli kweli,sidhani kama amezungumzia biashara aliyofanya Ikulu.Nikiri kwamba binafsi sijawahi kukiona hicho kitabu.
 
Back
Top Bottom