Ninasikitika kwa kutokuweza kutumia haki yangu ya kuchagua viongozi wangu leo. Nilijiandikisha kupiga kura, nilihakiki jina langu kwenye tovuti ya NEC, bahati mbaya nimepata safari ya ghafla ya kikazi. Nipo nje ya nchi. Najua kuna watanzania wengi leo ambao hawataweza kupiga kura kwa sababu mbali mbali. Sote, nami kwa niaba yao, nawatakia uchaguzi mwema.