Nilisingiziwa kesi ya kumpa mimba mwanafunzi, nafikiria kufungua mashitaka ya udhalilishaji

inyele

JF-Expert Member
Aug 8, 2017
1,244
2,000
Salaam wakuu!

Januari mwaka huu mimi mwenyewe niliundiwa kesi ya kutengenezwa, wenyewe waliita "plan". Nikakamatwa na Polisi na kupelekwa mahabusu ambako nililala siku moja kabla ya kupata dhamana.

Ilikuwa hivi..

Kabla ya kukamatwa kwangu; niliwahi kuwa na mazoea ya karibu sana na binti mmoja katika mazingira ninayoishi ambaye kwa kipindi hicho alikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari. Baada ya mazoea kuzidi sana Julai 2016 nilimtongoza huyo binti na ALINIKUBALIA KWA MDOMO ombi langu ukaribu wetu ukawa mkubwa kiasi kwamba watu baadhi walijua kuwa kuna kitu kiliendelea kati yetu yaani mapenzi.

Kwa kipindi chote hicho HATUKUWAHI KUFANYA MAPENZI. Alinizungusha sana kwa muda mrefu bila mafanikio licha ya kuwa kuna kipindi tulikorofishana hadi akanitolea maneno machafu ; binafsi sikuwahi kumjibu matusi yake badala yake nilijaribu kutafuta suluhu ya tofauti zetu nikizingatia kwamba lengo halikutimia(sikumla).

Novemba 2016 alihitimu kidato cha nne na sikumuona kwa muda hivi na simu yake haikupatikana!

Mwezi Desemba 2016 niliondoka na kwenda likizo mkoa mwingine kwani huko ndio kwetu. Nikiwa likizo nilipigiwa simu na mtu ambaye alidai anataka msaada wangu kwenye jambo fulani nikamjibu niko mbali na nkamwelekeza namna nyingine ambayo ingemfaa kutatua shida yake.

Baada ya kumaliza muda wa likizo nikaanza safar kurudi eneo langu la kazi. Nikiwa nimemaliza muda mchache tu baada ya kushuka kwenye gari mara paaap...nikapokea simu ya yule yule mtu, alijitambulisha tena na kuuliza nilipo.

Bila wasiwasi wowote nikamjibu niliko na akaomba kuniona nikamkubalia. Dakika chache tu akawa amekuja nilipo; kumbe ALIKUWA AFISA WA POLISI!

Alinikamata akiwa na wenzake na kunipeleka kituo cha Polisi! Nilisomewa shitaka la kutuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi (yule rafiki yangu kipenzi) na yeye binti akakihakikishia kituo cha polisi na maafisa wote kuwa mimi ndiye niliempa ujauzito na nkapelekwa mahabusu (lockup).

Baada ya kupata dhamana nilifanya uchunguzi wa hali ya juu na utafiiti yakinifu kwa kumtafuta yeye mjamzito wa kuigiza na marafiki zake. Wakati huo kazini nilisimamishwa wakisubiri hatima za tuhuma zangu ndipo wanipe utaratibu mwingine kama ni kuendelea na ajira au la.

Kumbe hata HAKUWA MJAMZITO. Nilipeleka taarifa nilizopata kituoni japo polisi wapate kujua ukweli lakini bila huruma yoyote walisoma data zangu na kuendelea kuning'ang'ania kama kawa!

Jina langu lilichafuka nikasemwa nikanyoshewa vidole na kila namna ya kejeli!! Niliwashangaa sana watanzania kwa jinsi walivyo wepesi kukubali kulishwa sumu na kudiriki kuongelea mambo wasiyoyajua!!

Tulisumbuana sana na mzazi wa binti nikihitaji suluhisho la jambo hilo licha ya kuwa siku za mwanzo aliniomba rushwa kuuubwa nami kutokana na hofu na kutokuamini mahakama nilikubali kulipa kidogo kadri tulivyoelewana.

NB: Nilikubali kulipa kwani kipindi hicho nilikuwa sijui lolote kuhusu ukweli wa mambo yaani hata kujua kuwa binti ni mjamzito au la sikujua!!

Baada ya kujiridhisha na uchunguzi wangu nilikataa kutoa rushwa tena nikawaambia polisi na mzazi wa binti sina hela nyingine hivyo wachague moja kati ya kufuta shitaka au waamue twende mahakamani.

Nilizungushwa weee hadi mwishowe wakanichia huru mnamo Machi 2017. Niliporudi kazini baada ya kuachiwa huru nikawapa taarifa zote na baada kukaa muda mrefu bila mustakabali wa Ajira yangu hatimaye niliachishwa kazi Aprili 6, 2017.

Sikuchukua maamuzi magumu ya kuwachukulia hatua wabaya wangu licha ya kuwa kuna watu wangu wengi wa karibu walinishauri niwafungulie mashitaka kutokana na kudhalilishwa.

Mwezi uliopita yaani Novemba 2017 mbaya wangu(binti) alinipigia simu akiniomba msamaha akadai anataka aje kuniona nikamruhusu aje na nikamwelekeza nilipo. Alikuja tukaonana tukaongea kidogo akaondoka! Anajifanya kuumia kwa kile alichonifanyia, anatia huruma ukimwangilia hana jipya! Yuko flat kama nyigu.

Wakuu nikifikiria jinsi hadhi yangu kwenye jamii ilivyochafuka nashikwa na hasira sana na natamani kurudisha heshima yangu kama zamani na watu wananiambia hakuna namna nyingine zaidi ya kufungua mashitaka dhidi ya udhalilishaji ule ambao ulinichafua sana!

Wakuu napata msukumo na nafikiria kufungua mashitaka hivyo naomba ushauri wenu juu ya hili. Je inawezekana kufungua mashitaka? Kama inawezekana ni namna gani naweza kuliendea hili?
 

Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,458
2,000
kudadadeki,hapo ni jino kwa jino,wafungulie mashtaka ili kurudisha heshima yako na kutoa funzo kwa wanajamii kama hao!

ikibid wakulipe au wakamueleze boss wako uhalisia ili urudi kazni!
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,473
2,000
kosa kubwa ulilolifanya ni kumtongoza kipindi bado anasoma.. na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi ni umevunja sheria hata kama hukula mzigo... nina imani kipindi cha uhusiano wenu kuna vitu ulimnunulia na hata sms za kimahaba uliwahi mtumia... hivyo vinakufunga hivyo.. makampuni ya simu yakiambiwa na mahakama yatoe ushahidi wa mawasiliano wanatoa

hivi wadada wa vyuo walivyojaa na wanashoboka kweli ukiwa na kaajira na kagari.. unaanzaje kutongoza mwanafunzi tena wa o level ...
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,046
2,000
Uwezekano wa kufungua kesi dhidi ya binti na wazazi na dhidi ya mwajiri wako upo.
Ila huyu binti na wazazi itategemea sana wakoje kiuchumi ili wakusafishe jina vizuri
 

inyele

JF-Expert Member
Aug 8, 2017
1,244
2,000
Mkuu unasema kazi umeachishwa kwa kosa lipi au mie cjaelewa.... every person is innocent until contrary is proved..... au unafanya kazi libya poleeee kwa maswaibu
Sababu ya kutuhumiwa na kulala lockup ...jamaa walisema hata kama tuhuma si za kweli wew hawawezi kuendelea kuwa nawe kazini
 

inyele

JF-Expert Member
Aug 8, 2017
1,244
2,000
kosa kubwa ulilolifanya ni kumtongoza kipindi bado anasoma.. na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi ni umevunja sheria hata kama hukula mzigo... nina imani kipindi cha uhusiano wenu kuna vitu ulimnunulia na hata sms za kimahaba uliwahi mtumia... hivyo vinakufunga hivyo.. makampuni ya simu yakiambiwa na mahakama yatoe ushahidi wa mawasiliano wanatoa

hivi wadada wa vyuo walivyojaa na wanashoboka kweli ukiwa na kaajira na kagari.. unaanzaje kutongoza mwanafunzi tena wa o level ...
Hiyo ni kesi nyingine mkuu...vipi kuhusu upande mwingine KUDANGANYA VYOMBO VYA SERIKALI mfano polisi na hospitali ambao waliamua kughushi nyaraka kusudi Mimi niendelee kuwa na hatia???
 

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,578
2,000
Acha upoyoyo na porojo.

Zaidi shukukru Mungu kuwa umekoswakoswa na 30+ years in jail.

Tukienda kwa haki kabisa una makosa maana; ulikuwa na nia ya kufanya mapenzi na mwanafunzi na kwa maelezo yako inaonekana hata elimu yako ni majanga yaani; hujui hata binti/ mwanamke aliye mjamzito au la.

Any way, fungua kesi halafu wakushinde ili baada ya hapo; wakufungulie kesi nyingine ili ufungwe maisha kabisa jela kama wenzako akina Babu Seya sijui jina jingine ni Papi Kocha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom