Nilisimuliwa stori ifuatayo kuhusu mabasi ya mwendokasi huko Urusi ya Kisovieti

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
EDIT: The heading of this post was "Under Penalty of Perjury". Pana mtu asiyetumia ustaarabu aliyebadilisha kichwa hicho cha habari bila idhini yangu, huku akiacha kichwa cha habari alichokiweka bila kuweka jina lake au taarifa kwamba ni yeye aliyebadilisha kichwa cha habari.

UNDER PENALTY OF PERJURY

Nilisimuliwa stori ifuatayo kuhusu mabasi ya mwendokasi huko Urusi ya Kisovieti.


Wakati taifa la Urusi ya kikomunisti likiendelea kupambana ili kujenga taifa lenye uchumi wa kijamaa, liliamua kuleta mabasi ya kubeba abiria ("transit") nchini kwao.

Tofauti na ilivyokuwa kwa nchi zingine, Urusi iliamua kuweka dereva tu kwenye gari, ambaye kazi yake ilikuwa ni kuendesha gari, kupakia na kushusha abiria. Haikuwa kazi yake kukata tiketi.

Vituo vya kukatia tiketi kwa abiria vilikuwa nje ya basi kwenye vituo maalum. Aghalabu, tiketi nyingi zilikuwa ni za msimu. Unakata tiketi yako, na kuendelea kupanda gari mpaka muda wa tiketi utakapoisha. Unanunua tena, maisha yanaendelea.

Tatizo lilikuwa kwamba, madereva hawakuwa na wajibu hata wa kukagua nani ana tiketi, nani hana tiketi.

Miezi ya mwanzoni, watu wengi, hasa vijana, walipanda magari yale bure. Hakukuwa na konda wala mkaguzi. Walienda wanakotaka, bila kulipa. Wale waliokuwa wakilipa, walionekana ni mazumbukuku, ulimwengu uko huku.

Siku moja serikali ya kisovieti ya Urusi iliweka wakaguzi wa ghafla kwenye vituo vyote. Unaposhuka, unaonyesha tiketi yako halali, au unakamatwa, na kupakiwa kwenye karandinga, safari ya kwenda kwenye Gulag, Siberia.

Rundo la "wajanja" waliishia Siberia, vivi hivi wakijiona.

Toka siku hiyo, ilichukua vizazi kadhaa heshima na adabu. Hakuna wakaguzi, hakuna kondakta, ni dereva tu, na abiria wote wa kwenye mabasi ya Russia walikuwa ni wenye kuheshimu STK: Sheria, Taratibu na Kanuni; zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

Hadithi Hii Inatufundisha Nini?:

Sworn declaration - Wikipedia

Badala ya michakato (Business Processes) mingi kuhusisha viambatisho vingi vya "UHAKIKI WA TAARIFA", itoshe kwa mtuma maombi/mjaza fomu kutoa tamko under penalty of perjury, kwamba "I declare (or certify, verify, or state) under penalty of perjury that the foregoing is true and correct. Executed on (date)".

Hii itaharakisha utendaji uende haraka, na kupunguza urasimu na umangimeza.
 
Back
Top Bottom