Nilisimamia show ya mafuta na lunch lakini bado niliachwa kituo cha basi

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Leo nimepita maeneo ya Mbalamwezi beach nikakumbuka kisa fulani kilichotokea 2012.

Nilipokuwa chuo mwaka wa kwanza, nilikuwa na kibaby flani cha kichaga. Alikuwa handsome balaa, ana gari (japo la kupewa na mama lakini gari ni gari), ana swaga, mrefu, anajua kudance (hiki kigezo kwangu muhimu). Yani dream guy.

Basi ile tumemaliza zetu mwaka wa kwanza ile June ndo tunaenda field. Mimi nilipata position Dar yeye alipata mkoa. Basi ndo tukaamua kuandaa kidate cha kuagana. Tukameet mwenge, haoo tukaenda kwanza Ubungo kumpeleka ndugu yake flani. Baada ya hapo tukasema twende Mbalamwezi, mara tukaingia petrol station akasema "Baby nimesahau wallet aisee halafu gari haina wese". Mtoto hapo nimekolea kimapenzi halafu wallet yangu ina laki moja na ushee, so nikamuuliza tuweke mafuta ya kiasi gani?. Akasema ya 30,000 yatatosha, nikatoa.

Tukatoka hapo haoo tukaenda Mbalamwezi. Tukaingia akasema "Mi sina hela we ndo boss so nakusikiliza". Nikamwambia tule tuu...Akaja mhudumu tukaorder mishkaki na chips na bia mbili zake na soda yangu (bill ilikuwa kama Elfu 40 na ushee, nikalipa mtoto wa kike). Tukala palee, tukapiga story wee...tukaenda beach tukaagana pale na maneno ya mahaba kibaooo...

Mimi nyumbani ilikuwa Ilala na yeye Tegeta. Kuondoka tukapanda kwenye gari kufika nje si ndo heeee baby ananishusha kituoni. Sikuamini macho, masikio wala pua yangu. Tena haoneshi wasiwasi wowote wala sura ya huruma. Akanikiss shavuni na kusema "Bye baby, ntakumiss sana sana". Yani niliishiwa nguvu lakini nilijivuta zangu nikachukua kipochi changu nikashuka nikaenda zangu kituoni. Kulikuwa na foleni ya hatari pale kwa Warioba, magari hayasogei hata kidogo upande huu wa kwenda morocco. Baada ya kama nusu saa or less ananitext "Baby yani huwezi amini nishafika home. Hamna hata foleni yani."

Yani hata kuniuliza kama nimepata gari hakuuliza. Nilikabwa na donge moja shingoni. Nitoe hela ya mafuta, nitoe hela ya lunch, halafu sipati hata a ride home?? Sio kwamba nilihesabu zile pesa au ziliniuma lakini jamani kweli ur girl anasimama kituoni kusubiri basi wakati unaweza kumpeleka home?...Yani siku ile ile nilimtoa moyoni na haikupita wiki nikabreakup nae bila sababu. Ilimsumbua sana kwani i was very rude, sitaki discussion. Sijawahi kumwambia ni kwanini tuliachana na sidhani kama anajua kosa lake au alifeel hata vibaya ile siku. Leo nimekumbuka na hasira ikanishika upya.

Nadhani alinifanya hata nichukie wanaume wenye magari (labda baba V tu). Akinisimamisha mtu na kigari chake huwa namchukia ghafla bila sababu. Hivi kweli kile ni kitendo cha kumfanyia umpendaye?
 
hahahaha dah jamaaa nimemkubali. very nice...this demostrates that katika kila date both sexes wanakuwa na expectation more so wen they pay the bill. sasa jamani msishangae pale mwanaume nagaramikia kidate alafu u act all suprised when i ask for ur papuchi.
 
Teh!hakufanya poa ila sema sijui kama anajua kuwa hakufanya poa nadhani ungekuwa na moyo wa subra labda mngekaa Sawa mapenzi magumu sana!!!!!
 
sasa kama gari la mama mbona mwanamke hakuliona hilo kabla ya hili tukio? sii angemkataa toka mwanzo kuwa i dnt date guys that drive their parent's cars.
wewe bwana gari kisu cha warembo haijalishi la mama au lako mwenyewe.
 
Alafu cku iyo mmekuja na mimi nilikuwepo pale. Nilikuwa nimekuja na bby wangu kupunga upepo. Niliwaona! Mlikuwa mmependezaje? Yan na uzuri wote huo jamaa hakujali? Yan cku ile nilikutamani uwe wangu hadi gf wangu alijua.
Hahaahah....ni wewe kumbe yule?...Heshima yako mkuu, baby wako ni kisuu
 
Back
Top Bottom