saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,131
- 6,130
Jana wakati waziri wa ujenzi na uchukuzi anahitimisha hoja zake kimsing iangetueleza mpango wa kujenga barabara kuunganisha wilaya zetu na mikoa kuliko kuelezea mradi wa SGR. Huu mradi ni wazi watanzania wengi hawajaufurahia kwani hauwagusi watanzania wengi unapitia sehemu chache sana kulinganisha na ukubwa nchi yetu. Ushahidi ni kuwa ni km hakuna wabunge walioujadili, asilimia 96 walijadili barabara zilizo katika maeneo yao. Rais aliyejua mahitaji ya watanzania ni Jakaya Mrisho Kikwete. Mwaka 2010 alikuja na ajenda ya kuunganisha mikoa kupitia makao makuu ya mikoa. Vilevile aliunganisha nchi yetu na nchi za jirani kupitia mipaka yetu.
Kiukweli kwa mtazamo wangu matrilioni yaliyopelekwa kujenda SGR yangetumika kuunganisha wilaya zetu na kumalizia kuunganisha mikoa iliyobaki. Kwa mfano kwa mkoa wa Morogoro ijengwe barabara ya Ifakara-Kilombero-Mahenge-Malinyi-Mwaya na kuunganisha Morogoro - Songea na Njombe. Ijengwe Barabara ya Handeni-Kiteto-Kondoa. Same-Simanjiro-Arusha. Barabara ya Karatu-Mbulu-Haydom-Nduguti-Gumanga-Ibaga-Sibiti-Meatu-Lalago-Kolandoto na Lalago-Maswa. Barabara nyingine muhimu kama ya Karatu-Matala-Meatu. Barabara ya nafikiri Kilindi-Turiani-Dumila-Kilosa
Hii ni mifano michahe ninayoweza kuitoa. Hizi barabara zingegusa maisha ya watanzania moja kwa moja Tanzania yetu ingependeza sana. Matrilioni yanayotumika kujenga SGR yangeelekezwa ktk hizi na zingine zinazofanana na hizi.