Nilipoyaona haya nilijua Magufuli hawezi kusaidia maskini, alichowafanyia Watanzania ni kuwafanya mafukara zaidi

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,760
6,294
Habari wana JF,

Mnamo mwaka 2015 JPM alijipigia chapuo sana kuwa ni Rais wa wanyonge. Sikuelewa sana, nikasema ngoja nijipe muda nione.

Baada ya mwaka mmoja tu nikaona dalili za wanyonge kuumizwa sana, huku akidai ananyoosha nchi. Sikuelewa!

Hapa chini nakudadavulia mambo ambayo yanaonesha JPM alivyowafukarisha hoi bin taaban hata wale waliokuwa nacho kidogo.

1. Aliongeza makato ya bodi ya mikopo (HESLB) kutoka 8% hadi 15% kila mwezi
Mshahara hajaongeza hata tone, anadai anajenga reli, na kununua ndege. Hivi jamani, Rais hujaongeza mshahara wa mtumishi, unaongeza vipi makato? Naombeni mnisaidie kushangaa! Mshahara hutaki kuongeza, bado unawaongezea makato kweli?

Chini ya JPM, aliyekuwa anapokea laki 3, kwa makato haya amefanywa kupokea laki 1 na pointi.

(maskini amekuwa fukara, hoi bin taaban).

2. Alipandisha kilo ya sukari kutoka 1,800/- ya jk hadi sh. 2,500/- au zaidi
Wananchi wakiwa wanyonge vile vile kaingia kazuia kuingizwa sukari, bila hesabu wala maarifa. Matokeo yake sukari ikapungua, bei ikashuti. Kaanza kukimbizana na watu ma-godown huko. Ovyo kabisa!

Mwisho wa siku anatangaza eti bei elekezi eti sh. 2,500/- Nisaidieni kushangaa!

Hivi umekuta bei 1,800/- kwa kg, yeye jpm miaka miwili tu ikawa mara mbili sh. 3,000/-

Yani iko hivi hela ambayo maskini alikuwa ananunua kg 2, leo ananunua kg 1 tu imeisha.

(waliokuwa maskini amewafanya mafukara, hoi bin taaban)

3. Alizuia minada ya mazao kama mbaazi, korosho, ufuta n.k.
Akawapekekea jeshi watu wa kusini kuchukua korosho zao. Matokeo yake, bei ya mbaazi ikashuka kutoka sh 1500/- kwa kg hadi sh. 200/- kwa kg zikakosa wanunuzi, hasara kwa maskini.

Korosho zilivyobebwa hakuna ajuaye. Jeshi kwenye mambo ya kiraia, huwezi kuhoji. Wengine wakaishia kuambiwa korosho zao zilikuwa eti mbovu. Mpaka leo hawana kitu. Hawana hela na uendelezaji wa mashamba msimu mpya umekuwa mgumu.

(maskini mkulima amefanywa fukara, hoi bin taaban)

4. Bomoa bomoa ya nyumba DSM (Kimara), na huko Moro bila fidia kwa sheria ya mwaka 1938/50.
Huyu JPM aliacha sheria za miaka ya 80, za road reserve kuwa mita 60. Akachukua sheria ya kikoloni road reserve mita 120.

Kabomoa mpaka ambako barabara haitapita. Waliokuwa na nyumba, wakabaki nje na maskini hatari. Kwa maisha yale yale

(maskini akafanywa, fukara hoi bin taaban)

5. Hatoi ajira
Toka ameingia madarakani ni madaktari elfu 3 na ushee na walimu baadhi wa sayansi ndio waliajiriwa.

Yani mzazi kasomesha mtoto, kwa kujikamua, enzi za jk walimu walikuwa hawaombi ajira, ilikuwa ukimaliza ualimu degree, au cheti/diploma, unasubiri kupangiwa kituo. Ukatae mwenyewe kazi. Ila leo soma, maliza ng'ombe za wazazi, na kazi JPM hatoi.

(maskini amekuwa fukara zaidi, hoi bin taaban)

6. Hakuwajengea walioharibikiwa nyumba na tetemeko la Kagera pamoja na kukusanya michango kila pembe ya dunia.
Maskini wa Kagera, akaambiwa hajaletewa tetemeko.

(maskini akawa fukara, hoi bin taaban)

7. Kikokotoo cha pensheni ya wastaafu.
Akaleta kikotoo eti ukistaafu zile hela ulizohifadhi, upewe kiduchu. Yani ufanye kazi miaka 60, uzeeke. Wkt unataka hela yako, jpm anasema chukua kiduchu. Huko nyuma wastaafu walikuwa wanapewa mara moja 75% ya hela , yeye akasema wapewe 25% tu.

(hapa maskini mstaafu anapunguziwa hata jasho lake la kwenda kupumzikia). Fukara, hoi bin taaban.

8. Kahawa huko kagera alikuta wanauza kilo 2500/-, kazuia wa Uganda wasije kuinunua. Ikashuka bei hadi sh 1000/-

Maskini akawa fukara zaidi, hoi bin taaban chini ya JPM.

Kwa ufupi:
Wakulima hoi bin taaban
Wafanyakazi hoi bin taaban
Wastaafu hoi bin taaban
Waliomaliza vyuo hoi bin taaban
Wafanyabiashara hoi bin taaban
Wavuvi hoi bin taaban

Eti huyu anataka mi5 tena!! Afanye nini?

Huyu ni rais wa wanyonge gani?

Ongezea wengine walio hoi bin taaban
 
Habari wana JF,

Mnamo mwaka 2015 JPM alijipigia chapuo sana kuwa ni Rais wa wanyonge. Sikuelewa sana, nikasema ngoja nijipe muda nione...

Mungu akimchagua mtu, hakuna mwanadamu anayeweza kumwangamiza. Halafu mtu akichaguliwa na Mungu lazima atafanyiwa kila aina ya ubaya kutaka kumwangamiza. Sauli aliyekuwa mfalme alianza kumuwinda Daudi kwa kutumia majeshi yake na mara kadha Sauli alimkosa Daudi kwa kumrushia mkuki na kumpiga mshale.

Hata Yusufu kwa kuwa alichaguliwa na Mungu ndugu zake walimtupa kwenye shimo refu lakini Mungu alimuokoa hivyo akamfanya kuwa waziri wa Misri. Danieli alitupwa kwenye tundu la simba wenye njaa ila Mungu alimlinda akatoka salama na akawa kiongozi mkuu katika nchi ya Babeli. Mtu akichaguliwa na Mungu hawezi kuzuiliwa na mwanadamu
 
Ndio.

Akaiacha KATORO pale jirani yake. Na Geita mjini pia akaiacha. Kaendeleza kijiji chake.

Mwakani anajimegea mkoa Mpya kama akishinda.

Kakwambia nani kwamba anataka kujimegea Mkoa mpya akishinda mwakani!! Mikoa iliyo pakana na Chato ni: Geita,Kagera na Kigoma - si alisema atahamia Mkoa wa Kagera akistaafu,sasa huo Mkoa wa ziada una ulazima gani au sehemu ya Karagwe hipo kwenye mpango huo?
 
Ambacho mkulu amekosea ni kuacha kulainisha vyuma katika kipindi hiki.

Yani angeachia watu wadokoe national cake kidogo wapate japo ile icing sugar (HELA) kupooza machungu mbona kiulaini wangempa kura. Sasa ye kakaza hadi sasa na wahuni wanasubiria 28 hapo wamtie Pipe Range kwenye sanduku 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom