Nilipoteza laptop yangu imeokotwa na nimeletewa hadi nyumbani!!!

Sema tu laptop iliangukia katika mikono salama....ila hata huko USA kuna mikono ambayo ingeangukia ingebaki story tu....watu wanaiba mpaka mikate supermarket hukohuko USA sembuse washindwa kukwapua hiyo laptop. Hata hapa bongo wapo watu wasafi na wapo wachafu pia. And it's like this else where.
 
Hata Europe/USA mabegi na mzigo uliosahaulika wengi wanaita polisi kwasababu ya security, wanajua ni mtego. Hio ndio sababu kuu ukisahau mzigo airport au railway station utaupata tu.
Uko sahihi kabisa,nchi kama US sasa hivi wapo kwenye "High alert security" hasa hayo maeneo uliyoyataja hapo juu,since 9/11 terrorist attack,

Hata hiyo laptop ya mleta mada si ajabu Polisi walishaifanyia "full inspection" na baada ya kujiridhisha ndio wakairejesha kwa mwenyewe,ni ngumu sana kupoteza mzigo Airport.
 
ni ngumu sana kupoteza mzigo airpot.. hapo umemaanisha airpot za ughaibuni tu au airport zote?
 
Uaminifu si nje ya nchi tu hata huku kwetu upo

Nakumbuka mwaka 2000 nilisahau simu model ya Samsung R220 ndani ya dalala lakini ikiwa ndani ya mfuko wa matunda Mara nilipofika nyumbani Michenzani Zanzibar nilipiga simu na dreva akapokea na kunijulisha kuwa amepewa na abiria hiyo simu.
 
Nawaza tu....

Hivi inawezekana mtu ukabeba begi la laptop yako bila kuhisi kua begi limekua jepesi sana..!! so inamaana laptop haimo ndani ya begi?

Mpaka unafika huko uendako "unachukua begi na kulifungua" baada ya kulifungua ndio unagundua hakuna laptop!?

Kama ni laptop yako na umeizowea basi utakua tu na hisia ya uzito wake,so hata kabla ya kulifungua begi utajua tu kua laptop haimo sio mpaka ufungue begi ndio ujue..!!

Uaminifu nakubaliana na wewe kua upo kwa baadhi ya States in USA,hilo nina experience nalo,BUT hii story yako ni kama umeamua kuwanywesha watu CHAI ya ndimu tu mkuu.

Hata mimi niliwaza sana hili, lakini nikakumbuka kuwa mimi mwenyewe najaza vitu kibao kwenye begi ya Laptop ili kukwepa kutozwa elfu 22,000 na fastJet siku hizi kuna punguzo ni 11,000 lakini bado ni nyingi mkuu. Inawezekana ni scenario hiyo
 
Unaokota m bag halafu ndani unakuta kuna bomu limebakisha sec 5 kulipuka
 
Thank Jesus!
Nilikuwa nasafiri kutoka Phoenix Arizona kwenda Bakersfield California nikiwa airport nimekaa na laptop yangu nje ya begi lake. Baadae nikaondoka na begi ya komputa kumbe komputa yenyewe imebaki pale chini nilipokuwa nimeiweka.

Baada ya kufika katika jimbo la California nikiwa nyumbani kwa mwenyeji wangu, ndio nikasema ngoja nitoe laptop yangu niangalie emails kadhaa, kufungua begi la komputa hakukuwa na komputa ndani ya bag, ndipo nikakumbuka nitakuwa nimeiacha kule airport Arizona.

Namshukuru Mungu baada ya mawasiliano na watu wa airport ya Arizona waliniambia iliokotwa na kupelekwa kwenye "Lost and Found Department" na wakafanya mpango wa kuituma kutoka Arizona mpaka hapa California.

WAMENILETEA MPAKA MLANGONI! NIMEWAZA TU KWA SAUTI INGEKUWA IMEPOTELEA KWENYE VIWANJA VYETU VYA HUKO BONGO NINGEIPATA KWELI AU NDIO NINGEHESABU MAUMIVU??
Hamna bhana pale airport kwetu kuna vijana waaminifu sana wizi hakuna kabisa kama unabisha siku ukija njoo uiache hapo uone kama hawatakuletea
 
Sasa vipi unataraji kurud ktk asili yako... Huku kwa mabab zako... Embu kasahau ktk vijiji vingine huko USA utupe mrejesho pengine ni hapo Airport ukizingatia kun KAMERA
 
Niliokota cm kwenye daladala na sikuizima jamaa akapiga nikapokea acha aanze kunipolomoshea matusi? Oooh we K hiyo simu haitokufikisha popote fala mwizi cjui nini mara nini Duh!!!

mi nikamwambia kama unapajua sehemu furani njoo nikupe cm yako.jamaa akaja ila akaja na wazee kama watatu ili wanisombe eti nimemuibia cm yake.
Nashkuru mungu muonekano wangu uliniokoa.
Kuna siku mtu alisahau bahasha nilipoiona nikaamua kumpelekea office kwake jibu alilonipa nibaki kinywa wazi alisema kama ingekuwa hela ungeniletea na maneno kibao basi mie nikamjibu kuna doc muhimu kuliko fedha. Kuna binadamu hawana shukrani unaweza kutenda wema ikageuka karaha next time unaamua tofauti
 
ni ngumu sana kupoteza mzigo airpot.. hapo umemaanisha airpot za ughaibuni tu au airport zote?
Airport nyingi tu hua kuna uaminifu,na hili limezidi zaidi katika miaka ya hivi karibuni na hasa baada ya 9/11 terrorist attack,

Watu wamekua waoga sana kuchukua begi,laptop au mzigo wowote usiowahusu, coz unaweza ukachukua begi la mtu kumbe kuna bomu au madawa ya kulevya,hapo ukikamatwa nalo hakuna atakayekuamini kua eti huo mzigo sio wako! tuwe waangalifu sana na jambo hili.
 
Kuna siku mtu alisahau bahasha nilipoiona nikaamua kumpelekea office kwake jibu alilonipa nibaki kinywa wazi alisema kama ingekuwa hela ungeniletea na maneno kibao basi mie nikamjibu kuna doc muhimu kuliko fedha. Kuna binadamu hawana shukrani unaweza kutenda wema ikageuka karaha next time unaamua tofauti
kuna Mijitu inawaponza wengine.
 
Kuna siku mtu alisahau bahasha nilipoiona nikaamua kumpelekea office kwake jibu alilonipa nibaki kinywa wazi alisema kama ingekuwa hela ungeniletea na maneno kibao basi mie nikamjibu kuna doc muhimu kuliko fedha. Kuna binadamu hawana shukrani unaweza kutenda wema ikageuka karaha next time unaamua tofauti
Mkuu endelea tu na huo moyo wako wa uaminifu,usikatishwe tamaa na mtu mmoja tu,au usiihukumu jamii nzima kwa bad reaction ya mtu mmoja,tenda wema nenda zako usingoje shukrani,uaminifu ni moja ya siri kubwa sana katika kuyafikia mafanikio,keep it up Mkuu.
 
Waaminifu hawapo USA tu hata hapa wapo.
Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kufanya kazi bankX hapa Bongo kitengo cha Central Cash ambapo walikuwa wanapokea pesa toka Nchi mbalimbali duniani.
Ilitokea awamu fulani walifanya ENQUIRY ya USD 2,000,000/- badala yake kule USA wakajichanganya wakafanya REMITTANCE ya USD 5,000,000/- zikaja mpaka Bongo huku nyaraka zote zinaonesha clearance na APPROVAL ya 2M$ na Bank Wakadeclare vivyo hivyo! kufika Central cash walivyochana BUNDLES wakakuta mzigo upo EXCESS ya 3millions$ ikabidi wale wahudumu wa central cash unit WA DISCLOSE kwa uongozi Mzigo ukarudi USA!! Jamaa wa USA walishangaa sana!!! Je, wewe ungeweza?? kipindi bro ananihadithia haya hakuwa na nyumba wala mkokoteni nikatamani kumtemea mate usoni!!!
 
Back
Top Bottom