Nilipoteza laptop yangu imeokotwa na nimeletewa hadi nyumbani!!!

Boloyoung

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
682
652
Thank Jesus!
Nilikuwa nasafiri kutoka Phoenix Arizona kwenda Bakersfield California nikiwa airport nimekaa na laptop yangu nje ya begi lake. Baadae nikaondoka na begi ya komputa kumbe komputa yenyewe imebaki pale chini nilipokuwa nimeiweka.

Baada ya kufika katika jimbo la California nikiwa nyumbani kwa mwenyeji wangu, ndio nikasema ngoja nitoe laptop yangu niangalie emails kadhaa, kufungua begi la komputa hakukuwa na komputa ndani ya bag, ndipo nikakumbuka nitakuwa nimeiacha kule airport Arizona.

Namshukuru Mungu baada ya mawasiliano na watu wa airport ya Arizona waliniambia iliokotwa na kupelekwa kwenye "Lost and Found Department" na wakafanya mpango wa kuituma kutoka Arizona mpaka hapa California.

WAMENILETEA MPAKA MLANGONI! NIMEWAZA TU KWA SAUTI INGEKUWA IMEPOTELEA KWENYE VIWANJA VYETU VYA HUKO BONGO NINGEIPATA KWELI AU NDIO NINGEHESABU MAUMIVU??
 
Niliposoma kichwa cha habari nikajua sio Tanzania.
Hebu acheni kujidharau. Bado kuna watu wana imani. Hiki nachoandika kimetokeam Dare-Salaam, last month. Kuna Mtu ( sitaji jisnia kulinda identity yake hasa akiona humu' alichukua bajaji niani tu wala si mtu anayemjua akasahau Laptop yake hawajuani na hakumfikisha njiani hivyo hata nyumbani kwa huyo mtu hakufahamu. Huyo mtu akaenda maeneo alikochukua bajaji wakasema wanamfahamu lakini hapaki pale. Alifuatalia nifupishe akampata huyo wa bajaji akakuta laptop yake intact. Na yule wabajaji akasema walipofungua ndio wakakuta Jina la Ofisi kwa kuwa ni mbali akawa anajikusanya atafute hela ya mafuta akaipeleke. Inaweza kuwa watu wabaya wengi lakini malaika pia Tanzania wapo. Hongerah sana Dreva wa Bajaji!
 
Asante kwa kutupatia na sisi mfano mzuri kaka sio wa TZ wote majuha
 
Mimi binafsi nilishawahi kusahau iPhone mpya na Samsung Tab kwenye Bajaj maeneo ya Kijitonyama. Nilikuwa nakutana na watu kwa maongezi pale Mesuma Hotel. Kutokana na foleni kali ya jioni nikaamua kupaki gari na kusimamisha Bajaj pale Break point ya zamani opposite millennium tower.
Nilipofika Mesuma katika haraka zangu wakati namlipa Dereva wa Bajaj simu na Tab nikaviweka kwenye kiti ili nitoe wallet kiurahisi. Nilipomaliza kumlipa nikashuka na kuendelea na ratiba nyingine.

Nilipofika juu kule ndio jamaa yangu mmoja ananiuliza mbona nakupigia simu kwenye private number yako hupokei!!!??? Hamadiiiiii ndio nashtuka na kupiga yowe.
Likanijia wazo fasta....nikaipiga ile namba yangu haraka. Nilipiga Kama mara 10 ndio jamaa akapokea. Nikamueleza nimesahau simu kwenye Bajaj yake,akaniambia alishafika Lugalo anaenda Tegeta. Nikamuomba na kumsihi sana. Huwezi amini Jamaa alinirudishia vitu vyangu mpaka pale Mesuma na nikamtoa na hela nzuri tu ya Shukrani. Mungu ni mwema ukimtumainia.
 
Back
Top Bottom