Nilipokea rushwa ya CCM bila kujua na niliisaidia kushinda bila kujua sasa nifanyaje

Mkubwa ndevu

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,045
358
Ndugu zangu leo naungama hali ya kuwa nimefunga ramadhani ya 25, huu ninaosema ni ukweli mtupu mimi ni kijana wa miaka 22 najua mtashangazwa vp niliisaidia CCM kwenye uchaguzi wa 2005.

Niliandikishwa kupiga kura hali ya kuwa sijatimiza umri wa miaka 18 lakini haikuwa makosa yangu nilipelekwa na mmoja ya wazazi wangu kwa lengo la kuisaidia CCM ishinde huku waindikishaji wakielewa fika kuwa sijatimiza miaka 18.

Na la pili kuhusu kupokea rushwa nimefunguliwa duka na mzazi wangu ila mwaka jana TRA hawakuja kunidai kodi zao {angalizo sio kwamba sipendi kulipa kodi au silipi mpaka nifatwe bt nakua mgumu kulipa sababu sioni kodi zangu zinapotumika}

Sikujua kwanini lakini leo nimegundua kuwa ulikuwa uchaguzi mwaka jana ndio maana hawakuja kudai ili kuwe na urahisi wa kushinda au siko sahihi ndugu zangu

Kwa kuanzia nenda kalipe kodi uliyokwepa mwaka jana. Hili la kuisaidia ccm umesamehewa kwa masharti ya kutorudia tena mchezo huo na uanze mara moja kushirikiana na wanamageuzi.

Kwa kuisaidia ccm mwaka 2005, malipizi yako njoo Igunga tukupe majukumu ya kuhakikisha ccm inaangukia pua

Kalipe kodi na jifunze kua na utaratibu huo.
Kuhusu kuisaidia ccm kushinda kutokana na rushwa,wapo wengi sana kwakua walikua hawajitambui au ni kutokana na kutojua thaman ya kura.
Ni vizuri umejitambua kua ulipotea.karibu sana kwa wanamageuzi wa kweli.TANZANIA BILA CCM ITAWEZEKANA.

Nenda katoe zaka, saidia maskini, kalipe kodi, usipokee rushwa, saidia chama cho chote unachopenda kishinde, tumia democrasia, mtumikie Allah siku zote. Trust in Jesus that you be SAVED.

Endelea kutokulipa kodi cuz haina faida kwako, maisha yanazidi kuwa magumu tu, wanafaidi akina jairo na masaburi wenzake tu. Hlo la kuisaidia ccm nadhani adhabu umeshaipata kwa ugumu wa maisha unaouface.

pole sana kwa kuwa natamaa ndogo ndogo kwa kuwa umekuwa sasa fanya maamuzi yako sahihi..

umesamehewa kuhusu kuwasaidia magamba kuhusu kodi usilipe utasaidia kina jairo na luhanjo wazidi kuvimbisha masaburi

Uliyafanya hayo ukiwa mdogo tena kwa kurubuniwa. Sasa umekuwa mkubwa na KUIKUA UNAACHA

kama mtu ana hamu ya kukasirika. Asikilize kipindi cha jahazi , jinsi kibonde anavyolamba minduku ya watawala kwa kujifanya mjuaji wa kila kitu. Nilimsikiliza jana kidogo nilie. Samahani kwa off topic

nice confession boy! jitahidi kuombea nchi yako. swala la kodi kwangu sawa tu na usilipe hadi nchi itakapo kombolewa..

Ulimsaidia kilaza gani wa ccm mpaka akashinda?inabidi huwe muwazi kwa ata unapoenda kwa padri kutubu lazima utaje zambi zako wazi wazi kama kuzini,kuiba kusema uongo nk.sasa tuambie mbunge ulimpigia kura nani na bado yupo mjengoni au aliangushwa na nguvu ya umma.

Ndugu zangu leo naungama hali ya kuwa nimefunga ramadhani ya 25, huu ninaosema ni ukweli mtupu mimi ni kijana wa miaka 22 najua mtashangazwa vp niliisaidia CCM kwenye uchaguzi wa 2005.

Niliandikishwa kupiga kura hali ya kuwa sijatimiza umri wa miaka 18 lakini haikuwa makosa yangu nilipelekwa na mmoja ya wazazi wangu kwa lengo la kuisaidia CCM ishinde huku waindikishaji wakielewa fika kuwa sijatimiza miaka 18.

Na la pili kuhusu kupokea rushwa nimefunguliwa duka na mzazi wangu ila mwaka jana TRA hawakuja kunidai kodi zao {angalizo sio kwamba sipendi kulipa kodi au silipi mpaka nifatwe bt nakua mgumu kulipa sababu sioni kodi zangu zinapotumika}

Sikujua kwanini lakini leo nimegundua kuwa ulikuwa uchaguzi mwaka jana ndio maana hawakuja kudai ili kuwe na urahisi wa kushinda au siko sahihi ndugu zangu

zakayo (wa kwenye biblia) alipogundua amewaibia watu aliungama na kuwarudishia mara mbili..fanya hivyo nawe utakuwa huru kweli

Kwa kuanzia nenda kalipe kodi uliyokwepa mwaka jana. Hili la kuisaidia ccm umesamehewa kwa masharti ya kutorudia tena mchezo huo na uanze mara moja kushirikiana na wanamageuzi.

Mkuu nakupa five, huu mchango wako unamfaa huyo dogo.

Ukimaliza kuungama hili la kuisaidia CCM kushinda mwaka 2005 usisahau kuungama na hili la kuwadanganya wana JF. kama mwaka 2005 ulikuwa na miaka 18inakuaje leo uwe na miaka 22? Isije ikawa unaomba msamaha kwa kosa ambalo haukulifanya

Kawafungulie kesi wazaz wako. Msaada wa kisheria utapata.

Ndugu zangu leo naungama hali ya kuwa nimefunga ramadhani ya 25, huu ninaosema ni ukweli mtupu mimi ni kijana wa miaka 22 najua mtashangazwa vp niliisaidia CCM kwenye uchaguzi wa 2005.

Niliandikishwa kupiga kura hali ya kuwa sijatimiza umri wa miaka 18 lakini haikuwa makosa yangu nilipelekwa na mmoja ya wazazi wangu kwa lengo la kuisaidia CCM ishinde huku waindikishaji wakielewa fika kuwa sijatimiza miaka 18.

Na la pili kuhusu kupokea rushwa nimefunguliwa duka na mzazi wangu ila mwaka jana TRA hawakuja kunidai kodi zao {angalizo sio kwamba sipendi kulipa kodi au silipi mpaka nifatwe bt nakua mgumu kulipa sababu sioni kodi zangu zinapotumika}

Sikujua kwanini lakini leo nimegundua kuwa ulikuwa uchaguzi mwaka jana ndio maana hawakuja kudai ili kuwe na urahisi wa kushinda au siko sahihi ndugu zangu

Basi hao wazazi wako ni wajinga,tena wapuuzi sana. hawakukuelimisha hadi leo hii walikuwa na maana gani. na wewe pia akili yako ni sawa na ya baba yako, kwa nini usingeenda kumuuliza huyo mzazi wako alifanya hivyo kwa ajili gani. kumbe basi wewe ni mtoto wa nyoka unaetaka kugeuka kenge.

Ukimaliza kuungama hili la kuisaidia CCM kushinda mwaka 2005 usisahau kuungama na hili la kuwadanganya wana JF. kama mwaka 2005 ulikuwa na miaka 18inakuaje leo uwe na miaka 22? Isije ikawa unaomba msamaha kwa kosa ambalo haukulifanya

Huyu ni ngumu sana kumuelewa, Sidhani km amechanganya kati ya 2010 na 2005,

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom