IBRA wa PILI
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 1,447
- 2,285
Siku hiyo kulikuwa na mechi ya Simba na Yanga, mechi hiyo iliisha kwa Simba kushinda goli 1 kwa nunge goli la MK14.
Ilikuwa ni mida ya saa kumi ndio kulikuwa na hiyo mechi hapo palikuwa ni lodge na bar ya mshua na Mimi ndio msimamizi au meneja wa hapo.
Wakati nipo bize nikitazama mpira huo walikuja wageni fulani na gari mimi sikuwaona ilo nilijua baadae nilikuwa bize na mpira mpaka wanachukua vyumba wahudumu ndio walishughulika nao.
Mechi ikaisha nipo na furaha kwa Simba chama langu kushinda na siku ikapita saaafi.
Sasa siku fulani mida ya saa moja jioni ilikuwa kama mwezi wa 11 au 12 ilipita karibu miezi mitatu hivi toka hilo tukio, nimetoka saloon naelekea apo lodge hiyo ni tarehe 7 tarehe ambayo wasimamizi wa guest inakuwa ni tarehe ya mwisho kwenda kulipia kodi ya mapato ya mwezi uliopita.
Na siku hiyo nilitoka kulipia kitabu manispaa ila tulikuwa na guest 2 zote hizo mimi ndio huwa naenda kulipia lazima ubebe kitabu cha wageni, wakati nimetoka kulipia pale manispaa ya Songea Mjini nilipoondoka guest ya kwanza ipo bombambili inabidi nipite hapo niache kitabu mi sikupita nikaona ntakileta baadae nikanyosha kuelekea ambako ndio hua nashinda
vitabu vipo kwenye begi ile kufika nikaacha begi kaunta nikasepa na mizunguko yangu.
Jioni iyo saa moja ndio natoka saloon kunyoa narudi nakuta gari tatu zipo pale ndani Toyota mayai nyeupe 2 na moja ni IST kijivu.
Nikapita zangu huwani sina ili wala lile nikaona kupitia dirisha muhudumu kabananishwa anaulizwa iki kitabu cha wapi mbona namba tofauti mnatumia vitabu viwili sio??
Kakosa jibu ameduwaa tu yule askari mkali kinyama jina lake maarufu LUKUBA sijui muhehe sjui mbena
Basi bana nikaona kumbe ishu ni kitabu ngoja niende nikawaelekeze nikajua wakaguzi tu wa vitabu nikaingia pale akamuuliza muhudumu
Meneja yupo wapi aliponiona akasema uyu hapa akaniuliza
Kitabu cha gest kipo wapi?? iki sio na manatumia vitabu viwili
Kumbe muhudumu alipoenda kwenye beg langu akachukua tu kitabu bila kuangalia na kuwaletea alafu beg lilikua na kitabu kingne cha gest iyo nyingne sasa ye alijua cha pale ndio akaleta.
Mi nikamwambia afande kitabu iki kakosea iki sio cha hapa mim nilijisahau Leo siku ya kulipia iki kitabu ilibdi nipitishe gest flani
akahamaki we brother mpumbavu acha ujanja brother Sawa kabla ya kuja uku unapita pale kivipi usahau acha masihara cha hapa kikwapi nikaenda kuchukua bana nipo na askari yupo na mtutu ananifata nyuma yule askari aliniambia dogo kua mkweli na usiseme uongo Sawa usiogope nikamwambia aina shida bro apo sijui tatizo kubwa ni nini mpaka mitutu.
nikaleta kitabu wakaangalia majina ya watu wao yalikuapo ila ya uongo sio ya ukwli na muda ule wateja walioingia awakuandikwa, na wahudumu usipokuepo wanapiga kwa mtindo huu awaandiki jina pesa kapuni mpaka ufatilie sasa iyo siku ndio ukawa msala.
Afande akasema meneja mzembe, we Dada bahati yako tungeondoka na wewe ila kaja uyu tunaondoka nae we utabaki du mungu wangu nakwenda selo,
saa moja jioni iyo nikajipa moyo sina kosa ntarudi bana.
Nikaingizwa kwenye IST tulikua na afande mmoja anaitwa victor pande la mtu black ivi kaenda hewani akasema meneja usihofu bana wala akuna shida.
yule afande mkali wakaingia gari nyingne nikawaona na jamaa flani ivi wamepigwa pingu wapo wawili usoni sikuwaona vizuri, safari mpaka kituo kikuu songea nikaingizwa kaunta pale nikawekwa chini nika ambiwa nivue viatu mkanda nikabizi na simu na kila kitu kilichopo mfukoni mwangu nikafanya ivyo nikaa kaa pale chini nilivaa soksi azikukakuka vizuri bana harufu iliyotoka hapo ilisamba pale pote nasikia askari nini hiki sijui mmoja akasema mhm kuna dogo kavua kiatu kachafua hewa.....ilikua balaa
Tuendelee kwenye point nika andika majina yangu pale kaunta afande yule aliuliza uyu ana kesi gani yule afande mnoko akajbu kuiba na kuvunja nikashangaa Mimi kuiba na kuvunja lini,
then nikapelekwa mahabusu for the first time katika maisha yangu jamaa walinipokea oya umekula msosi hapana sijala wakaniletea msosi bana
Ulikua ugali na dagaa bwana uo ugali ata bodingi school sikuwai ona wakati nasoma kummmke uji maunga unga tupu mboga dagaa maji chumvi mchuzi kibao aise ulinishinda kula nikasema hapana nimeshiba bana si ulisema ujala nikajbu Amna shida.
Ndani mahabusu nilimkuta bro wangu mtoto wa mama mkubwa upande mwingine wa uko kama unavyojua ndugu sometimes mkionana ndio apo apo alikua ana kesi yake ila sikuijua baadae niliijua.
nae ananishangaa dogo vipi umekula mtaji nini wa louge nikamwambia hapana bro ila nime andikiwa kesi ya kuiba na kuvunja
Sielewi chochote hapa,
tukatulia pale piga stori kidogo wanaletwa wazurulaji ma boda boda mpaka kukajaa mule ndani kuna muda watu wakamaindi ahaa umu tumejaa afande tunajibana
afande akasema sogeeni chooni uko watu wakagoma,
bana afande akasema msinizoee Sawa akaingia akatandika mtu kofi paaaa watu wakanywea wakasogea vile vichumba vimejaa.
naiti iyo, sasa nikajilaza sakafuni kichwa ukutani naangalia bati usingiz Amna jamaa wengne wapo na story tu kusogeza masaa pale ukutani nilipoweka kichwa walinipanda kunguni kichwani uzuri sikua na nywele kubwa nikawatoa wote nikalala katikati kwa kujibana ukuta nikauacha mbali yule bro wangu alinipa kopo la maji lina maji ndani ndio kama mto unaweka kichwani,
Apo nawaza watakuja sasa ivi kunitoa kimya.
Tumelala tupo ka biskuti ivi
Kumbe mshua alifika kunifata kituoni, uyu ni mshua wangu mkubwa ila sio baba mzazi na awajatoka tumbo moja na dingi ye kamuoa mama yangu mkubwa ambae ndio toka nitoke na mama yangu mzazi.
Alivyofika pale kaunta akauliza jina langu ibrahim akatajiwa ila Mimi niliandika jina la pili la babu na sio la baba hua najichanganya sana na uyu dingi nafikir alikua analijua jina la mzee wangu la kwanza tu akauliza ana kesi gani wakamwambia kuvunja na kuiba akaona haaaa sio yeye uyu kuiba na kuvunja wapi na wapi akasepa kwenda vituo vingine kunisaka.
Tena siku iyo usiku kulikua na mpira wa uefa juve na Manchester united afande baadae akaja akasema oya nyie wale wa mpira Manchester wamesinda 2-1 apo nikajua saa sita sasa ndio muda mpira unaisha ulianza SAA 4...............
Pause kidogo Ntarudi kuimaliza