"Nilipogundua kuwa tumebaki wawili peke yetu..." | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Nilipogundua kuwa tumebaki wawili peke yetu..."

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Ndibalema, Feb 23, 2011.

 1. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.

  Muumini: "padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"

  Padri: "endelea"

  Muumini: "bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?"

  Padri: "utasamehewa"

  Muumimin: "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na hiyo?"

  Padre: "utasamehewa"

  Muumimi: "nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"

  Padre: "utasamehewa"

  Muumimin: "nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. Yesu atanisamehe na hilo?"

  Padre: ........"kimya"........!!!!

  Muumimi: "padri, Yesu atanisamehe kwa hilo?"

  Padre: - "kimya" !!.........

  Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka.

  Muumimi: "sasa baba mbona umenikimbia?"

  padri kwa taabu akajibu........

  "nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"

   
 2. M

  Mwang'ingo New Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mele Magobole!!!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huyo jamaa hapo lazima amuuwe huyo padri, maana ataogopa kuwa padri atatoa siri...huh!
   
 4. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,567
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  lazima atoke nduki hapo
   
 5. N

  Nothing4good Senior Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwanini thread zinarudiwa? Zinabadiliswa hedding zinachosha bana!
   
 6. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lekanjobe ni hii hapa usijali inachekesha bado
   
 7. VeniGan

  VeniGan Senior Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hahahaahahahaa 2ko wawaili...
   
 8. DavidHard

  DavidHard JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Huyo padri atauliwa na kisha huyo jamaa ataenda kuungama kwa asikofu
   
 9. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  duuuuh!!! huyu jamaa atawamaliza
   
Loading...