Nilipiga kelele na kuamsha majirani. Mpenzi wangu kaja usiku wa manane bila taarifa

kibla matata

JF-Expert Member
Mar 3, 2020
412
380
Usiku wa jana nimeangalia movie mpaka saa 7 za usiku, nikaacha kuangalia movie nikachukua simu yangu na kuanza kubeti. Nikiwa katika panga pangua ya mikeka yangu, na kusikilizia matokeo, naangalia muda ni saa tisa usiku, kumetulia hamna kelele za miziki wala sauti ya mtu ikisikika. Nachungulia nje kupitia dirishani naona giza nene umeme ulikuwa umekatika.

Mkojo ulinibana. Nitoke nje kukojoa, kwenye hili nyumba kuna korido ndefu kwa nje kuna mlimao, sasa wakati natoka nje kukojoa, ghafla nikaona mtu amevaa ushungi mweupe nikapiga kelele kwa nguvu: "Jamani jiiniiii, kuna jini uku uwiii".

Wakati napiga kelele yule mtu aliyesimama kwenye mlimao akawa anasema: "Ni mimi Kibla, usipige kelele" Kumuangalia vizuri ni demu wangu amekuja ghafla na ni usiku kama saa tisa hivi halafu hakunipa taarifa, pili hatujawasiliana kama miezi mitatu hivi.

Wakati najiandaa kumuuliza maswali mawili matatu, mama mwenye nyumba akawa ameamka na majirani kama wanne hivi.

Wakafika eneo la tukio na kuanza kunihoji wewe vipi mbona unatuamsha usiku huu, ulikuwa unapiga kelele za nini, nikaeelezea yakaisha wakawa wameenda kulala na mimi nikamchukua demu wangu tukaenda kulala.
 
Back
Top Bottom