Nilipeleka Posa kwa binti mrembo, nimeitwa Kisabengo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,034
50,956
Kwema Wakuu!

Tokea Tangazo la Walamba Asali kujitangaza kuwa Mzinga wa nyuki umejaa pomoni ukifurika asali, wakasema huu ndio wakati wa Kula masega ya asali na asali yake.

Nilidhamiria kujiunga na umoja wa familia za Walamba Asali kivyovyote.

Wapo walionibeza kuwa ninapenda mserereko, wengine wakanisema nitanyanyasika Kwa ufukara wangu, lakini nataka kuwaambia umasikini unanyanyasa zaidi kuliko kitu chochote hapa Duniani.

Nikaamua nichague pakuseka aidha kuteswa na umasikini au kuteswa na familia za walamba Asali.

Rafiki yangu mmoja mwanasiasa machachari yeye akaniambia, hawezi kujiingiza kwenye familia za walamba asali kwani hapendi Dharau, yeye akasema ni afadhali aendelee kuwalamba miguu na kuwasifia HAO walamba asali mpaka siku atakapopewa kacheo lolote, lahaula Bahati ya Mbwa IPO miguuni mwake akateuliwa kuwa DAS Huko Bara. Sasa hivi kapiga kimya ungedhani sio Yule aliyekuwa kwenye vipindi vya Luninga akibwabwaja kuwasifu walamba asali.

Taikon nikasema Acha niendelee kupambana na Hawa watoto wa kike wa walamba asali nikasema kwenye watoto Mia Moja siwezi kosa hata mmoja wa kumuoa.

Nilitongoza watoto kadha wakadha nikaambulia patupu kumbe utongozaji wa watoto wa walamba Asali ni tofauti na hawa watoto wa watengeneza Asali, unajua kwenye asali kuna michakato mpaka uione asali vile ilivyo, lazima uandae mzinga uuweke sehemu nzuri yenye miti au mimea inayozalisha Maua kwaajili ya uchavushaji ili nyuki wafanye Yao.

Ukae ukijua IPO tofauti ya mtengeneza Mzinga wa nyuki na Nyuki mwenyewe, Nyuki wakati anatengeneza asali hajui anatengeneza kwenye mzinga uliotengenezwa na Mtu.

Sasa asali akishatengeneza mwenye mzinga anakuja anasema Asali ni yake na nyuki Naye anasema Asali ni yake.
Wakienda mahakamani Nyuki anashindwa kesi Kwa sababu kafanya Uvamizi kwenye eneo la mwingine, hivyo atanyang'anywa asali na wakati mwingine atalipishwa Faini.

Hayo ndio Maisha ya Duniani, sikuwa tayari kujiweka kwenye nafasi ya Nyuki mtengeneza asali asiyeweza kutengeneza mzinga, na Kama atajijengea asali nje ya mzinga bado hataweza kutengeneza asali nyingi ataishia kuwa Masikini tuu. Na ikiwa atapata sehemu nzuri ya kutengeneza asali isiyo na mzinga huko atakutana na watu mwitu msitu na wawindaji haramu watamfukuza na kuichukua asali.
Anyway sijui naelezea haya yote kwaajili ya nini,

Tuendelee!
Utongozaji wa Watoto wa lamba asali unahitaji umahiri na haiba, Kwanza wanapenda midomo yako uwe laini yenye utamu wakijua nawe ni mwenzao, hapo nikaenda Kwa Wakwezi wa mnazi nikawaambia wanipe Mafuta ya nazi, nilipopewa nikarudi na kuyapaka mdomoni, midomo yangu ikawa laini Kama Ini, yenye kuvutia. Mbinu hii ikanifanya niopoe Mtoto wa kigogo mmoja ambaye nadhani hata hapa anapitaga pitaga, siku za nyuma alikuwa Rafiki yangu akijifanya Mpenzi wa maandiko yangu.

Nilifikiri upenzi wake katika Kazi zangu ungenirahisishia Kukubalika ukweni, lakini haikuwa hivyo.

Binti yake amesomea mambo ya Finance, Mimi ni Mwanafasihi tuu mcheza na Lugha.

Yeye kasomea Marekani tangu akiwa sekondari, Mimi tangu chekechekea nimesomea Mnarani Kwa Madam chitemo, shule msingi zayumba, chuo nikasomea Chuo kikubwa cha nchi yetu.

CV yangu hiyo wakati namueleza Baba Mkwe alinisifu Kwa kujitahidi kufika walau Chuo kikuu, akasema walau ninakiakili, kidogo tumaini la kulamba Asali likaanza kuchipua.

Siku Ile kwenye kile Kikao walikuwepo vigogo wengine ambao ni marafiki zake, mawaziri wakiwa wawili niliokuwa nawafahamu kupitia vyombo vya habari.

Baba Mkwe mlamba Asali akaniambia wenzako wanasomea Mambo ya Fedha ili wapate Fedha Kwa sababu Fedha ndio jawabu la mambo yote wewe unasomea Sijui Fasihi na upuuzi gani utakula Lugha au hiyo Fasihi?

Akaongeza, itaki mwanangu aolewe na Kisabengo, nikajiuliza Kimoyo moyo Kisabengo ndio nini hiko, au ndio Mimi.
Hapo kichwani nikawa najaribu kumchora kisabengo, Picha iliyokuja ni kakiumbe Kama Smigo aliyeigiza filamu ya Lord of the Ring.

Baba Mkwe akaniuliza Akaunti yangu inakiasi gani cha Fedha, kiukweli sikuwa na Fedha zozote kwenye Akaunti ya Benji isipokuwa Akaunti za laini za simu nilikuwa na kiasi cha elfu 70 hivi. Lakini Kwa Hali ilivyokuwa nikadanganya Nina milioni mbili na nusu.
Yule Mzee akacheka Sana Kwa Dharau huku Wale vigogo wengine wakimsaidia kucheka.

Kwa nini wanacheka, nikawa najiuliza.

Sasa milioni mbili ni pesa kweli Kwa kijana mwenye nguvu Kama wewe? Akaniuliza, Umesoma mpaka Shahada lakini huna akili za kupata pesa mpaka Akaunti yangu iwe imekauka hivyo, hata Kama umewekeza pesa kwenye miradi mingine lakini haiwezekan ubakiwe na kiasi kidogo hivyo. Akasema kisha akaongeza, umewekeza kwenye nini?

Kwanza Hali niliyokuwa muda Ile nilikuwa nimepandwa na hasira huku nikilengwa lengwa na machozi, million mbili zenyewe sina alafu wanaongea hivyo lakini nikajipa moyo, nikamjibu kuwa sina KAZI wala sina biashara ya maana isipokuwa uwindaji, niliposema uwindaji wakatazamani(hapo nikiwa namaanisha muwindaji wa mabinti za walamba Asali).

Wakaniuliza muwindaji wa nini au Nina kitalu cha uwindaji katika mapori ya nchi yetu. Nikasema ndio uwindaji wangu sio katika mapori Bali muwindaji wa wanyama Pori wanaoishi Mijini kwenye Majini makubwa.

Hapo nikawaona wakinitazama kwa umakini Sana, kisha Mkurugenzi wa Benji Fulani kubwa hapa nchini akasema, ushaanza Fasihi zako Bwana mdogo, embu ongea waziwazi usiongee Kwa mafumbo, walamba asali hatupendi Kona kona Wal kuumiza vichwa katika mambo yasiyohusiana na pesa.

Nikawaambia, ninahitaji kumuoa binti Yao Kwa sababu ninampenda Sana, Naye ananipenda.

Nyokonyoko! Binti yangu hawezi kuolewa kisabengo Kama wewe, ingefaa uondoke hapa usije ukapata madhara ukamsababishia Mama yako huzuni. Nenda Kisabengo Nenda.

Kabla sijaondoka nikajikuta naimba;

Mimi kisabengo, muwindaji wa mwituni
Mzee wa kitengo, keshaji la jijini,
Siogopi zenu mbengo, tafutaji pesa za Majini,
Kamata wote Fungo, Wanyaji chafua viini
Hata kiruka na ungo, kamataji la wachawi angani,
Nitawakata zenu shingo, chomaji za nyama za mashetani,
Pesa zenu za vibwengo, toaji kafara la kuzimuni,

Nikatokewa nduki barubaru Kama Subaru,
Mtoto wao nimeshampa Mimba nimemwambia aifiche mpaka ikuekue walau miezi sita.

Taikon na harakati za walamba Asali.

Kwa sasa nimejichimbia chimbo!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Moshi
 
Fasihi na ufasaha wake huku ukisadifu yale yote yaliyomo...Hongera sana kwa BANDIKO MATATA mkuu Robert Heriel kwani kama kawaida yako hujawahi kutuangusha...
 
Mkuu mbn upo kwenye hatua nzuri sana ujue ukitaka kuvuna asali lazima utingishe mzinga na hapo nyuki watakushambulia na ndio hapo utawalaza na moshi wa majani kwahio hio ni vinyuki tu tafta majani washa moto
 
😀😀😀

Nashukuru kupata ABC za wakongwe
 
Naona umeamua kumulika mchakato wa kipata wawakilishi wa green EALA....🤣
 
Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom