Nilipata Supplementary kwa kipindi chote cha Miaka 4 Chuoni, hatimaye nitavaa joho hivi punde

Vitamin K

Senior Member
Dec 2, 2017
158
168
Waswahili(wahenga) walisema ''Mungu si Athumani" pia ''Mungu hamtupi mja wake"

Nilipata supp kwa kipindi chote cha miaka 4 nikiwa napambana na elimu yangu ya juu. Haikuwa jambo dogo hatimaye ndoto imetimia, ni furaha isiyokuwa na kifani. Sasa nimepita hatua moja na kuelekea hatua nyingine.

Nikiwa mwaka wa kwanza nilipata supp 1 kwenye semister ya kwanza, nilidhani ni utani huku nikijikumbusha record yangu ya nyuma kwenye juhudi za masomo, nikasema hii huenda ni bahati mbaya. Semister ya pili nikapambana sikuweza kupata supp kwenye hiyo semister, kwa hiyo mwaka wa1 nikawa na supp 1 tu ambayo niliifanya na kuchomoka.

Mwaka wa 2 niliingia nikiwa na dhamira ya kusoma kwa bidii ili nisipate supp lakini upepo ulinigeuka ikawa ni majanga zaidi ya mwaka wa 1, shule niliiona ni ngumu na chungu nikapata stress za hali juu, boom nikaliona si kitu tena.

Kwenye huo mwaka wa pili kwenye semister ya 1 nikaondoka na supp 1 na kwenye semister 2 nikaondoka na supp 2 jumla zikawa supp 3 kwenye mwaka wa 2. Nilizifanya hizo supp nikachomoka na supp 2 moja nikai-carry.

Mwaka wa 3 ukaingia, hapa niliamua kusoma bila stress kama ilivyokuwa mwaka wa 2, kama kawaida masomo ni magumu vilevile. Kwenye huu mwaka nikapata supp kwenye semister zote ambapo semister ya 1 nikapata supp 2 na semister ya 2 nikapata supp 2, jumla zikawa supp 4 huku nikiwa na carry over 1 ya mwaka wa 2. Nilizifanya hizi supp zote nikachomoa supp 4 nikacarry tena supp 1.

Nikaingia mwaka wa 4 na carry 1 huku nikiwa nashauku ya kusoma kwa bidii ili nizuie supp zingine lakini juhudi ziligonga mwamba, nikapata supp tena kwenye semister zote za mwaka wa mwisho. Kwenye semister ya 1 nikapata supp 1 na semister ya 2 nikapata supp 2, nikawa na jumla ya supp 4 nikijumlisha na ile carry over 1.

Baada ya kumaliza UE nilijijua masomo niliyofanya vibaya na nikaanza maandalizi mapema ya kujiandaa kuanzia masomo(carry over na supp ya semister ya 1) niliyosupp semister zilizopita huku nikijiandaa pia kwa yale masomo niliyofanya vibaya.

Matokeo yalipotoka nikakuta kweli kwenye yale masomo niliyofanya vibaya ndio nimefeli, hapo ndipo juhudi za maandalizi zikapamba moto.

Nilipanga ratiba ambayo kila siku lazima masomo yote 4 niyasome, ratiba ilianzia saa 2 asubuhi hadi saa 5 usiku, pakiwa na mapumziko muda wa lunch na kuanzia saa 10 jioni hadi saa 2 usiku.

Mungu si Athumani, hatimaye nilifanya mitihani nikafaulu na siku za karibuni nitagraduate pamoja na wenzangu ambao hawajahi kupata supp kwa kipindi chote cha miaka 4 chuoni.

WITO KWA WADOGO ZANGU MMNAOENDA KUANZA MASOMO HIVI KARIBUNI.
Imezoeleka chuo ni sehemu ya kula bata tena ikizingatia ukipata mkopo asilimia kubwa au asilimia zote na hapo boom linakuwa ni kutafuna tu kwa kula bata.

Unaweza kula bata na mambo yako hasa kitaaluma yakaenda vyema, na unaweza ukala bata ukasababisha mambo kwenda mrama, utajuta sana. Mwingine anaweza asiwe ni mtu wa bata na mambo yakaendelea kwenda mrama, hiyo pia ipo.

Raha kubwa chuoni ni kufaulu baada ya kuwa ushapata boom, supplementary zinauma sana japo mara nyingine zinatokea kama bahati mbaya. Jitahidini msome kwa bidii msipate supp.

Kuna suala la discontinuation(Disco), kila chuo kina sheria zake kuhusu hili suala la disco, kila mmoja anatakiwa azijue hizo sheria ili uweze kuzitekeleza ipasavyo na kuepuka disco.

Yapo mengi kuhusu maisha ya chuo, kulingana na chuo husika, kila mmoja atayajua zaidi akifika kwenye chuo alichochaguliwa
 
Hongera sana mkuu, supp nikawaida japo sio za kuzizoea,

Mimi nilipata moja mwaka wa tatu ,nikaichomoa,

Nikakutana na mwalimu hanipendi semister ya pili akanipa carry, na kwa sheria sikutakiwa kuvuka level , hivo nikasimama mwaka, kwasasa narudi nikiwa na ari na nguvu, naenda kihitimu nikiwa na amani,
 
Ahsante mkuu

Sapp sio poa kabisa mkuu mwaka wa kwanza sikupata sapp basi nikajiona na mimi kipanga mwaka waka wa pili niliona kila rangi mwisho wa mwaka nikawa nazo 3, mbili semister ya kwanza na moja semister ya pili nikaenda kusappua nikachomoa mbili moja naenda nayo mwaka wa tatu.
 
Hongera sana Kwa kumaliza masomo, pia umetoa ushauri mzuri,Kwa wanaotegemea kujoin huko,Kazi kwao kufanyia Kazi.

Maisha ya chuo ni free sana ila when it comes to masomo ,userious unahitajika kwani chochote utakachokifanya kina impact kwenye ufaulu wako, yaani sometimes hata attendance tu so ukidoji lecture,quiz duuh inakula kwako. Ila mleta uzi kama nakuona na kagentleman GPA kako, maana si Kwa kusapua hukoo
 
Supp zinauma sana, kwa awamu hii ya utawala walianza kutucheleweshea boom kisa tulipata supp
Sapp sio poa kabisa mkuu mwaka wa kwanza sikupata sapp basi nikajiona na mimi kipanga mwaka waka wa pili niliona kila rangi mwisho wa mwaka nikawa nazo 3, mbili semister ya kwanza na moja semister ya pili nikaenda kusappua nikachomoa mbili moja naenda nayo mwaka wa tatu.
 
Kweli kabisa mkuu, sisi baadhi ya malecture walikuwa wanatubana sana, ilikuwa ukichelewa hata dakika 2 baada ya yeye kuingia, anakuzuia huingii.

Kuhusu kaGPA si haba naweza kusomea master japo sitarajii kusoma tena
Hongera sana Kwa kumaliza masomo, pia umetoa ushauri mzuri,Kwa wanaotegemea kujoin huko,Kazi kwao kufanyia Kazi.

Maisha ya chuo ni free sana ila when it comes to masomo ,userious unahitajika kwani chochote utakachokifanya kina impact kwenye ufaulu wako, yaani sometimes hata attendance tu so ukidoji lecture,quiz duuh inakula kwako. Ila mleta uzi kama nakuona na kagentleman GPA kako, maana si Kwa kusapua hukoo
 
Kweli kabisa mkuu, sisi baadhi ya malecture walikuwa wanatubana sana, ilikuwa ukichelewa hata dakika 2 baada ya yeye kuingia, anakuzuia huingii.

Kuhusu kaGPA si haba naweza kusomea master japo sitarajii kusoma tena
Uko vzr mkuu, mtaani sometimes GPA siyo ishu saana, kuna malecturer wana sifa hao, nakumbuka sisi tulivokua tunakimbizana kuingia seminars, lecturer anaita majina inabidi uitike tena Kwa sauti , ukiingia wkt ashachukua attendance basi tena duuh
 
Waswahili(wahenga) walisema ''Mungu si Athumani" pia ''Mungu hamtupi mja wake"

Nilipata supp kwa kipindi chote cha miaka 4 nikiwa napambana na elimu yangu ya juu. Haikuwa jambo dogo hatimaye ndoto imetimia, ni furaha isiyokuwa na kifani. Sasa nimepita hatua moja na kuelekea hatua nyingine.

Nikiwa mwaka wa kwanza nilipata supp 1 kwenye semister ya kwanza, nilidhani ni utani huku nikijikumbusha record yangu ya nyuma kwenye juhudi za masomo, nikasema hii huenda ni bahati mbaya. Semister ya pili nikapambana sikuweza kupata supp kwenye hiyo semister, kwa hiyo mwaka wa1 nikawa na supp 1 tu ambayo niliifanya na kuchomoka.

Mwaka wa 2 niliingia nikiwa na dhamira ya kusoma kwa bidii ili nisipate supp lakini upepo ulinigeuka ikawa ni majanga zaidi ya mwaka wa 1, shule niliiona ni ngumu na chungu nikapata stress za hali juu, boom nikaliona si kitu tena.

Kwenye huo mwaka wa pili kwenye semister ya 1 nikaondoka na supp 1 na kwenye semister 2 nikaondoka na supp 2 jumla zikawa supp 3 kwenye mwaka wa 2. Nilizifanya hizo supp nikachomoka na supp 2 moja nikai-carry.

Mwaka wa 3 ukaingia, hapa niliamua kusoma bila stress kama ilivyokuwa mwaka wa 2, kama kawaida masomo ni magumu vilevile. Kwenye huu mwaka nikapata supp kwenye semister zote ambapo semister ya 1 nikapata supp 2 na semister ya 2 nikapata supp 2, jumla zikawa supp 4 huku nikiwa na carry over 1 ya mwaka wa 2. Nilizifanya hizi supp zote nikachomoa supp 4 nikacarry tena supp 1.

Nikaingia mwaka wa 4 na carry 1 huku nikiwa nashauku ya kusoma kwa bidii ili nizuie supp zingine lakini juhudi ziligonga mwamba, nikapata supp tena kwenye semister zote za mwaka wa mwisho. Kwenye semister ya 1 nikapata supp 1 na semister ya 2 nikapata supp 2, nikawa na jumla ya supp 4 nikijumlisha na ile carry over 1.

Baada ya kumaliza UE nilijijua masomo niliyofanya vibaya na nikaanza maandalizi mapema ya kujiandaa kuanzia masomo(carry over na supp ya semister ya 1) niliyosupp semister zilizopita huku nikijiandaa pia kwa yale masomo niliyofanya vibaya.

Matokeo yalipotoka nikakuta kweli kwenye yale masomo niliyofanya vibaya ndio nimefeli, hapo ndipo juhudi za maandalizi zikapamba moto.

Nilipanga ratiba ambayo kila siku lazima masomo yote 4 niyasome, ratiba ilianzia saa 2 asubuhi hadi saa 5 usiku, pakiwa na mapumziko muda wa lunch na kuanzia saa 10 jioni hadi saa 2 usiku.

Mungu si Athumani, hatimaye nilifanya mitihani nikafaulu na siku za karibuni nitagraduate pamoja na wenzangu ambao hawajahi kupata supp kwa kipindi chote cha miaka 4 chuoni.

WITO KWA WADOGO ZANGU MMNAOENDA KUANZA MASOMO HIVI KARIBUNI.
Imezoeleka chuo ni sehemu ya kula bata tena ikizingatia ukipata mkopo asilimia kubwa au asilimia zote na hapo boom linakuwa ni kutafuna tu kwa kula bata.

Unaweza kula bata na mambo yako hasa kitaaluma yakaenda vyema, na unaweza ukala bata ukasababisha mambo kwenda mrama, utajuta sana. Mwingine anaweza asiwe ni mtu wa bata na mambo yakaendelea kwenda mrama, hiyo pia ipo.

Raha kubwa chuoni ni kufaulu baada ya kuwa ushapata boom, supplementary zinauma sana japo mara nyingine zinatokea kama bahati mbaya. Jitahidini msome kwa bidii msipate supp.

Kuna suala la discontinuation(Disco), kila chuo kina sheria zake kuhusu hili suala la disco, kila mmoja anatakiwa azijue hizo sheria ili uweze kuzitekeleza ipasavyo na kuepuka disco.

Yapo mengi kuhusu maisha ya chuo, kulingana na chuo husika, kila mmoja atayajua zaidi akifika kwenye chuo alichochaguliwa
Wewe ni legend... Hongera sana mkuu
 
Kweli GPA si kitu ndio maana nimeamua hapa nilipofikia iwe kikomo cha kusoma na nipambane na maisha tu.

Malecture mara nyingine wanakuwa kikwazo sana ndio maana unaweza kukuta mtu anapata supp kila mara hata kama anajuhudi kwenye masomo

Back
Top Bottom