Nilipanga kusave laki 2, hatimaye nimesave laki 4 kwa mwezi. Nimefanikiwa kutumia Tsh 374,200/= kwa siku 28, ninaishi Geto.

Daaaahhh, pesa imekuwa tamu sana aisee kiasi kwamba hadi navunja kanuni niliyojiwekea.

Kipindi hiki nimefanikiwa kusave laki 1 na nusu, chini ya lengo la kusave angalau laki 3.

Nimegundua nikiendekeza ujinga siwezi kusogea hatua yoyote.

Kwa sasa nimepanga kusave laki 5 ili niweze kufidia magap ya nyuma. Endapo nikifuata mchanganuo huu lazima niweze kusave laki 5.

Mchanganuo:
Kwa siku natumia wastani wa Tsh 7,500/=

Kwa mwezi itakuwa 7,500 X 30 = 225,000/=.

Hii 7,500/= kwa siku afe kipa, afe beki tatu lazima niimaintain isizidi. Nimejaribu kuset nimeona kwa siku inakuwa chini ya 7,500/=, Hiyo inayobaki inakuwa akiba ya dharura ambapo naweza kutumia zaidi ya 7,500/=.

Kwa mwezi natenga 175,000/= kwa matumizi mengine kama vocha( 8,000/= kwa mwezi), Gesi, Unga wa kula na chochote kitakachotokea nje ya bajeti ya siku ambayo ni 7,500/=

NB: Msimamo, maamuzi sahihi, utekelezaji ndio mpango mzima.

Mungu ni mwema, hatimaye hii dhamira niliyoiweka mwezi uliopita imetimia.

Nimesave laki 5.

NB: Msimamo, maamuzi sahihi, utekelezaji ndio mpango mzima.
 
Mawazo mazuri...tukiwa na wa tz kama wewe tutasonga mbele kwakuwa naimani hata dogo unayeushi Nate anajifunza Vinci zaidi ya kusave ...kama unamshirikisha itamsaidia kujua iyo mambo
Sijamshirikisha ila kiasi ninachomuachia kwa matumizi yake hasa ya shule anakitumia vizuri hadi mambo mengine madogo madogo anajihudumia mwenyewe kutokana na akiba anayoweka kwenye hiyo hela
 
Una matumizi mabaya sana,yaani unaishi ghetto halafu umetumia zaidi ya laki 3 na 70 kwa mwezi?
Hapana mkuu.

Natumia kiasi kidogo tu. mfano mwezi uliopita(August/September) nimetumia 225000/= kwa matumizi yangu, nilitenga 175000/= kwa matumizi ya dharura nje na bajeti ambayo miongoni ni kusaidia ndugu akiomba kusaidiwa(kumbuka ndugu hakopeshwi hata kama atakuomba kwa mtindo wa kukopa, nikimpa naiweka kama Assist kwenye kumbukumbu zangu za matumizi), mchango kwenye idara kule ninakofanya kibarua( tuna utaratibu wa kufarijiana kwa michango kwa mwenzetu akipata tatizo kama kuugua ) na dharura zingine ndogo ndogo( maana hazikosekani )

Kwa mantiki hiyo lazima jumla ya matumizi ya mwezi yawe zaidi ya laki 3.
 
hongera kwa mpango wako wa kujitunzia akiba na hasa unapokuwa na lengo la uwekezaji.

mfano hata sisi tuliokopa mkopo tunaolipa kwa miaka 4 labda na hiyo pesa ukaitumia katika jambo linaloongeza kipato nje ya mshahara ni vizuri au ukadunduliza kama mshkaji.
ila inahitaji kuwa na NIDHAMU
Ahsante mkuu
 
Ubrazamen una nicost sana huku kupenda kupendeza huku kunafanya hatufikii malengo

Mapamban yanaendelea nikusave tu

Wale ambao desemba mnavunja vitu ntawafuata PM mnikopeshe
 
Hahaha hapo hata papuchi. .hatumii
Matumizi mengine hamishia huku.Maisha yenyewe mafupi ubahiri tu mwishowe upate ulcers bure sababu ya kushinda njaa

Mada maalumu ya walevi na wanywa pombe..
 
Ubrazamen una nicost sana huku kupenda kupendeza huku kunafanya hatufikii malengo

Mapamban yanaendelea nikusave tu

Wale ambao desemba mnavunja vitu ntawafuata PM mnikopeshe
Ukiamua kufanya jambo utaweza mkuu
 
Hongera, una save kwenye akauntu ya mshahara au nyingine? Kuna akauntu flani hivi sio fixed ila ni nzuri nakushauri ufungue hiyo
 
Nilikuwa nasave bank, kwenye statement yale makato yakawa yananiuma. Nikatengeneza kisanduku cha chuma kisichofunguliwa kwa urahisi kwa ajili ya saving, then nikatoa kahela kote nikahamishia kwenye kisanduku.
Kuna usiku mmoja ulikuwa mgumu! Nilikipasua pasua hicho kidude lakini nilichemka.
Sasa hivi nimeamua kumiliki nyundo kubwa na msumeno nisijekufa siku moja wakati hela ya tiba ipo.
 
Nafikiri ulibeti bela ikaenda ukaishiwa thats why ulitaka ubomoe
 
mkuu watu tumetofautiana, kwangu Mimi haya ni maisha ya kujitesa na kimaskini, tafta pesa kwa akili then pesa itakuelekeza jinsi ya kuitumia.....Huu upuuzi mm siwezi kuufanya natafta pesa na naitumia ipasavyo, na mpka nshafanya mambo mengi ya kimaendeleo lakini huwezi kuniambia huu upuuzi
Kwamba ku save ni upuuzi au nimeelewa tofauti bro
 
Back
Top Bottom