Dx and Rx
JF-Expert Member
- Jul 16, 2017
- 1,303
- 3,085
Mwezi uliopita nilisoma uzi humu ukielezea njia mbali mbali za kujiwekea akiba katika kipato anachopata mtu kwa kazi husika hasa kwa mwezi kama ilivyozoeleka kwa watu walioajiriwa.
Watu walifunguka kwa njia mbalimbali jinsi wanavyosave pesa zao za ujira baada ya mwezi, wengine wakasema wanatumia njia ya vibubu kusave na zinginezo.
Nilihamasika sana nikafikiria sana, kwa nini na mimi nisifanye hivyo...nikaangalia kipato changu ninachopata kwa kibarua changu, nikagundua ninaweza kusave laki 2 kwa mwezi(kwa makadirio ya chini).
Katika kufanikisha hilo nikaanza kucontrol kiasi cha matumizi kila siku, nikaanza kuandika kiasi cha hela kwa kila kitu ninachotumia, kila jioni nakokotoa jumla ya hela niliyoitumia kwa siku nzima na kuiandika kwenye doxc. Hapa kwenye doxc nimeamua kutumia soft copy, nimedownload App ya Microsoft Word ambayo naweza kuandika taarifa zote za matumizi(hii ndio njia bora zaidi kuliko diary/note book). Popote nikiwa kwenye mizunguko nikitumia hata Sh 100/= naingia kwenye file langu kwenye simu naiandika na kuisave.
Tangu nianze kutunza hizi kumbukumbu tarehe 22/3/2019, leo ni siku ya 28 na nimefanya mahesabu ya jumla nikakuta nimetumia jumla ya Tsh 374,200/= huku nikibakiwa na laki 4 kwenye account ambayo tayari imekutwa na kiasi kingine cha ujira.
Sasa najiwekea lengo la kusave laki 3 ili jumla iwe laki 7 baada ya mwezi kuisha(yaani kwa miezi 2 iwe jumla laki 7 niliyoisave), hapa malengo yangu ni kusave kwa muda wa miezi 10, endapo nikifanikiwa nitakuwa na jumla ya 3,000,000/=(kwa makadirio ya chini nikizingatia na Emmergency ambazo zinaweza kutokea), kwa kiasi hicho nitaweza kufungua kijiwe cha biashara yoyote nitakayoona inafaa.
Haya hapa chini ndio matumizi yangu ya muhimu na mara kwa mara:
1. Nauli(kwenda na kurudi kibaruani)
2. Nauli ya dogo(kwenda na kurudi shule), naishi na mdogo wangu namsomesha QT
3. Chakula cha mchana nikiwa kibaruani
4. Mahitaji madogo madogo kwa ajili ya chakula cha jioni
5. Vocha(2000/= kwa wiki)
6. Bili ya maji
7. Gesi(natumia mtungi mdogo, zaidi ya miezi 2)
8. Umeme(Luku)
9. Mengineyo kulingana jinsi yatakavyojitokeza kwa siku husika.
Nimeleta uzi huu kwa lengo la kupeana hamasa katika suala zima la kumanage hela.
NB: Mali bila daftari hupotea bila habari.
UPDATES 1.
Mungu ni mwema!
Kwa mara nyingine tena nimefanikiwa kusave laki 4, nimetumia TSh 591,300/= kwa siku 28.
UPDATES 2.
Mungu ni mwema!
Safari inaendelea, kwa mara nyingine tena nimefanikiwa kusave laki 4.
Kipindi hiki kilikuwa kigumu kidogo, nimetumia zaidi ya Laki 5 kwa matumizi mbalimbali.
Endapo nisingejikaza nisingeweza kusave kiasi nilichotaka maana ilihitaji kuwa na roho ya korosho sometimes..
UPDATES 3.
Ule msemo wa tumia pesa ikuzoee naona umepisha hodi hapa.
Kipindi hiki mambo yalikuwa mengi, nimejitahidi kusave Laki 1, chini ya lengo nililojiwekea lakusave angalau Laki 3.
Hakika hii safari ya saving inahitaji ujasiri mkubwa sana. Uvumilivu na kuweka tamaa pembeni ndio msingi wake
UPDATES 4.
Daaaahhh, pesa imekuwa tamu sana aisee kiasi kwamba hadi navunja kanuni niliyojiwekea.
Kipindi hiki nimefanikiwa kusave laki 1 na nusu, chini ya lengo la kusave angalau laki 3.
Nimegundua nikiendekeza ujinga siwezi kusogea hatua yoyote.
Kwa sasa nimepanga kusave laki 5 ili niweze kufidia magap ya nyuma. Endapo nikifuata mchanganuo huu lazima niweze kusave laki 5.
Mchanganuo:
Kwa siku natumia wastani wa Tsh 7,500/=
Kwa mwezi itakuwa 7,500 X 30 = 225,000/=.
Hii 7,500/= kwa siku afe kipa, afe beki tatu lazima niimaintain isizidi. Nimejaribu kuset nimeona kwa siku inakuwa chini ya 7,500/=, Hiyo inayobaki inakuwa akiba ya dharura ambapo naweza kutumia zaidi ya 7,500/=.
Kwa mwezi natenga 175,000/= kwa matumizi mengine kama vocha( 8,000/= kwa mwezi), Gesi, Unga wa kula na chochote kitakachotokea nje ya bajeti ya siku ambayo ni 7,500/=
UPDATES 5.
Nimesave laki 5 kutokana na kutekeleza mchanganuo niliouweka kwenye updates namba 4
NB: Msimamo, maamuzi sahihi, utekelezaji ndio mpango mzima.