Niliowapenda walinikataa, ambao sikuwapenda ndio walionikubali

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,147
33,302
Mapenzi ni imani ya ajabu kidogo. Mambo ya ajabu kwangu katika ulimwengu wa Mapenzi Ni hivi.
Wanawake wote ambao Mimi niliwapenda kwa dhati ya Moyo wangu na kutamani kuwa nao kwa mapenzi na uaminifu mkubwa sikuweza kuwapata, licha ya wengi hata kunisifu kwa upole na utulivu wangu. Lakini ajabu ninapopeleka Ombi la mahusiano hutokea sintofahamu nyingi na mwisho kutokubaliana. Hata Kama mwanzo tulikua tunaenda vizuri.

Ajabu wale wanadada ambao sikuvutiwa nao haijalishi Wana haiba gani, walitokea kunipenda Sana na hata kwa kuonesha alama zote za kunipenda, shida inakuja Mimi nakuwa sijapenda.

Hali hii ilinitesa Sana kwani baadhi yao kila wakinionesha green light Mimi nilikuwa sioneshi hisia zozote.
Mwisho wa siku niliambulia maneno ya kashfa mfano:
-Unaemtaka hajazaliwa bado
-Subiri malaika utawapata
-Mchagua Nazi Sana mwisho huchagua koroma. N.k
Kashfa hizi nilipewa na hawa ambao sikuwatilia maanani.

Elimu nilivyopata na nilichojifunza.

Wise men mmoja aliniambia, ukitaka kufurahia mapenzi na usiishi kwa presha chukua, oa, au anzisha mahusiano na mtu anaekupenda yeye zaidi kuliko unaempenda wewe zaidi. Kwa sababu unaempenda wewe bila yeye kukupenda itakua unalazimisha penzi hivyo kupelekea kukubuluza, kukutesa na kukudharau.

Lakini anaekupenda atakuwa anakupenda kwa dhati na atajitahidi kutokukuudhi ila unaempenda Kama hakupendi ndo mwanzo wa kukusaliti Mara kwa mara.

Ni heri uwe na mpenzi asie na mvuto lakini anakupenda utaenjoy,
Ni mbaya uwe na mpenzi mwenye mvuto lakini hakupendi utateseka.
 
Mi nimekutana na soul mate hapo unasemaje mweka mada ulieitwa mchagua nazi..?
 
Ukiwa na mpenzi anakupenda Sana...alafu wewe huvutiwi nae...Utamtesa TU Dada wawatu...TAFUTA mtakae pendana...
 
Mimi naona Bora wote mpendane hayo Mambo ya yeye akupende Sana sidhani Kama ni Sawa maana mwisho wa picha utamuumiza tu..tafuta akupendae nawe umpende.
 
Ukiwa na.mpnz anakupenda Sana...alafu wewe huvutiwi nae...Utamtesa TU Dada wawatu...TAFUTA mtakae pendana...
Hapana nilikuja kugundua kuwa nilikua nateswa na akili,hisia na mawazo ya kitoto.
Unajua wakati wa utoto tulikua au huwa tunaumba vitu vyetu akilini,lakini kadri unavyokua unaanza kuona sio halisi.
Kwa mfano wakati ule mtu wa nawaza utakuja kuwa na mke wa Aina fulani,nyumba ya Aina fulani,ndugu zako watakua na maisha fulani na vitu mbalimbali.

So nilipoona ninaowataka Mimi siwapati nukakubali matokeo na kuanza kuwatilia maanani hao waliokua wananipenda mm siwapendi mwisho wa siku nukawa nazoea,na upendo ukaanza kuja.
Ila simaanishi kuwa nilikua natamani wasichana warembo Sana, hapana.

Kwa mfano nilikua Napenda wasichana walioonekana Kama wachaMungu Sana,na wait walikua wananiona mm Kama mpenda (totoz)wasichana Sana ndio hapo tukawa tunapishana.kumbe sikua hivyo.

Basi miaka ilipokwenda wengine tukikutana baadae walionesha kujilaumu kwa nini walinikataa na kunipa sababu kuwa walidhani nataka kuwachezea tu.walijilaumu na wengine kuniomba samahani na majuto.
 
Mimi naona Bora wote mpendane hayo Mambo ya yeye akupende Sana sidhani Kama ni Sawa maana mwisho wa picha utamuumiza tu..tafuta akupendae nawe umpende.
Na Kama umpendae hakupendi utafanyaje?
Mwisho wa siku unabadilisha gia angani.
 
Ninaempenda anaweza kunichomesha mahindi kwa tochi,yaani nikatoka mtaani kwao nina sensa ya mbu wote,ila kuna mtoto wa watu ambae simpendi kiviile yaani ukimshtua ni kama umemchelewesha chapu kwa haraka huyu hapa,huwa nimemsave AMBULANCE, full kimulimuli a.k.a ZIMAMOTO
 
Unae mtaka haumpati, utampata wapi anae kutaka haumtaki haumpi nafasi

Fidq
 
Hata Kama Dem umemmaindi,ukikomaa Sana,kumfukuzia humpati,Ila ukifukuzia kiutani utani Kama huna mpango nae,utamkula kwa ulainiii,
Ila binafsi,sijawahi na Wala sitoamini kwamba Kuna Dem anamzimia men,hasa Hawa black wenzetu hapana,bado kwanza
Dem anaweza kaa na wewe ukajiachia Sana,kumbe hakupendi hata kidogo,mifano tumeona kwa ndugu na jamaa zetu.
Hata Mimi Sina Imani na mwanamke yeyote hata aseme ananipenda vipi,nakuona kibaka tu kwangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom