Nilionyeshwa picha hii ndotoni

Khalifavinnie

JF-Expert Member
May 19, 2017
2,759
2,307
Mnamo saa sita ya jana nioliota ndoto mbili zenye kufanana zikipishana kama dakika45 tano hivi,naeleza kwa ufupi ndoto ya kwanza niliota nikiwa nimekaa kitini mbele ya mlango wa chumba changu chini ya ule mlango kulilua na uwazi kidogo nikaona mikono kama ya kitu ikitokeza chini hivi kama inataka kuingia ndani,nikafungua nitizame ni nini nikaona kitu kama kimtu hivi kidogo sana kifupi ila ni mithili ya mtu kamili kikimbia kilikua na rangi ya kijani...

nikajaribu kukifuata kwa nyuma kilipofika mlango wa kutokea nje maana ilikuwa ni kama kordo na mbele kuna mlango wa kwenda nje kikasimama nikaogopa na kurudi ndani mbio sikufaam kama niko ndotoni kufika ndani nikashtuka nikatahamaki sana sikuamini kama ilikua ndoto wakati nazubaazubaa kujiuliza ghafla nikajikuta tena nimelala nikaamua kutoka nje ilikuwa giza sana usiku...

kuna kimtu tena kifupi sura siikumbuki kikaja kinanidai kitabu hapo nikiwa tena ndotoni ila sijajua nazani real life,nikaingia ndani na kutoa kile kitabu na kuweza kumpatia kitabub kile kile kama nilikifaamu flani hivi,kile kimtu kikapoke na kuanza kunifunulia page kadhaa ikafikia page flani akakomea na kunionesha kwa dakika kadhaa sasa sikujielewa kama naota au ni kweli nikajitaidi kukalili pale kuliluwa na maandishi kadhaa ila nimesahu na mpangilio wa picha ambao nilipata kunakili picha moja tu nyingine nimesahau..picha yenywe ni hii hapa chini...
IMG_20190325_125303.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnamo saa sita ya jana nioliota ndoto mbili zenye kufanana zikipishana kama dakika45 tano hivi,naeleza kwa ufupi ndoto ya kwanza niliota nikiwa nimekaa kitini mbele ya mlango wa chumba changu chini ya ule mlango kulilua na uwazi kidogo nikaona mikono kama ya kitu ikitokeza chini hivi kama inataka kuingia ndani,nikafungua nitizame ni nini nikaona kitu kama kimtu hivi kidogo sana kifupi ila ni mithili ya mtu kamili kikimbia kilikua na rangi ya kijani...

nikajaribu kukifuata kwa nyuma kilipofika mlango wa kutokea nje maana ilikuwa ni kama kordo na mbele kuna mlango wa kwenda nje kikasimama nikaogopa na kurudi ndani mbio sikufaam kama niko ndotoni kufika ndani nikashtuka nikatahamaki sana sikuamini kama ilikua ndoto wakati nazubaazubaa kujiuliza ghafla nikajikuta tena nimelala nikaamua kutoka nje ilikuwa giza sana usiku...

kuna kimtu tena kifupi sura siikumbuki kikaja kinanidai kitabu hapo nikiwa tena ndotoni ila sijajua nazani real life,nikaingia ndani na kutoa kile kitabu na kuweza kumpatia kitabub kile kile kama nilikifaamu flani hivi,kile kimtu kikapoke na kuanza kunifunulia page kadhaa ikafikia page flani akakomea na kunionesha kwa dakika kadhaa sasa sikujielewa kama naota au ni kweli nikajitaidi kukalili pale kuliluwa na maandishi kadhaa ila nimesahu na mpangilio wa picha ambao nilipata kunakili picha moja tu nyingine nimesahau..picha yenywe ni hii hapa chini...View attachment 1053616

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati unaota ulikuwa una njaa au umeshiba pomoni mkuu?

CC Zero IQ
 
Mkuu Jana kinywaji ulikinunua Kwa bei ya punguzo au ya kawaida.
Isijekuwa ulikuwa unamuota makonda akikufungulia kinywaji bila kujijua
 
Mbavu zangu!!! Watu tunaota mpaka tunafika mbinguni tunaulizwa maswali halafu tunarudishwa. Ukirudi unamuuliza mwezio hivi nilikuwa nimefariki?? Je, ungekuwa unaota nyoka kuanzia January mpaka Dec. si ungeenda kwa waganga? Wenzio yanatutokea ndo tunalala na Rosari na maji ya baraka.
 
Hiyo ya kwanza ni chama tawala kinavyowarubuni watanganyika kwenye chaguzi, ulivyokifukuza na kukatia tamaa njiani inaonyesha tabia ya watanganyika kujifanya wanakichukia sana ilhali kila uchaguzi ukifika kinarudi tena( hapa inaungia ndoto ya pili), kitendo cha kumpa kitabu(maarifa) inaonesha ujinga ulivyo mtaji kwa wanasiasa so ulimkabidhi ufahamu. Hiyo picha ya mtu ni watz, mmea wa kijani ni wakulima ambao wamenyang'anywa elimu na kimtu cha kijani hivyo jikaze kuichagua tena mwakani maana hamna namna. Natania tu kisiasa

kote hakufai
 
Mbavu zangu!!! Watu tunaota mpaka tunafika mbinguni tunaulizwa maswali halafu tunarudishwa. Ukirudi unamuuliza mwezio hivi nilikuwa nimefariki?? Je, ungekuwa unaota nyoka kuanzia January mpaka Dec. si ungeenda kwa waganga? Wenzio yanatutokea ndo tunalala na Rosari na maji ya baraka.
Rozari na maji vinazuia ubongo kufanya kazi wakati binadamu amelala au mimi ndio sijaelewa?
 
Rozari na maji vinazuia ubongo kufanya kazi wakati binadamu amelala au mimi ndio sijaelewa?
Vitu vyote huenda kwa imani. Imani yangu inanisaidia kupigana na hizo ndoto. Hata nikiziota naamuka nasoma Rosali usingizi unakuja.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom